Bajeti Wizara ya Viwanda na Biashara 2024/2025

Bajeti Wizara ya Viwanda na Biashara 2024/2025

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Jumla Kuu - Tsh. 110,899,722,000

Matumizi ya kawaida - Tsh. 81,115,206,000
1. Mishahara - Tsh. 68,352,946,000
2. Mengineyo - Tsh. 12,762,260,000

Matumizi ya Maendeleo - Tsh. 29,784,516,000

Katika mwaka 2024/2025, vipaumbele vikuu vya Wizara ni sita (6). Aidha, vipaumbele hivyo vitatekelezwa na shughuli mbalimbali za Wizara.

Katika mwaka 2024/2025, vipaumbele vikuu vya Wizara ni kama ifuatavyo:-

i. Kuendelea na utekelezaji wa miradi ya kielelezo na kimkakati;

ii. Kuimarisha uwezo wa uzalishaji viwandani na utoaji huduma kwa kuimarisha miundombinu na mazingira wezeshi;

iii. Kuboresha mazingira ya uwekezaji viwandani na ufanyaji biashara;

iv. Kuchochea maendeleo ya watu kwa kuboresha miradi na programu katika sekta za Kiuchumi na kijamii inayohusisha elimu na mafunzo ya ujuzi;

v. Kufanya intelijensia ya masoko ya bidhaa na huduma zinazozalishwa nchini kwenye masoko ya kimkakati na ya kimataifa; na

vi. Kuchochea ukuaji wa Sekta binafsi nchini.
 

Attachments

Back
Top Bottom