Bajeti ya 1.5 ninaweza kufuga kuku wa mayai

kitokololoo

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2018
Posts
704
Reaction score
818
Wajasiriamali habari zenu poleni na majukum ya kitaifa....Nina kiasi cha milioni moja na nusu bajeti hii naweza kuwalisha kuku na madawa mpaka watakapo anza kutaga?

Pesa ya kununua vifaranga ninayo tayari. Pia banda lipo safi kabisa pia vyombo vya kuwalishia vipo tayari nacho omba kuuliza?

Kwa kiasi hiki cha fedha milioni moja na nusu ninaweza kuwalisha na kuwahudumia madawa vifaranga wa kuku wa mayai mia moja mpaka vikaanza kutanga?
 
Kwa kuku mia inatosha kwa sharti la kwamba vyombo na miundo mbinu kama maboksi ya kutagia e.t.c tayari vipo
 
Jipange 6.5 trion kwenye SG huko rufiji tutakula nyasi safari hii
 
Dah....kifaranga mmoja anahitaji wastani wa Tshs 9,000/ kwa chakula na madawa hadi aanze kutaga... hii haijumuishi gharama nyingine Kama Kodi ya Banda, bill za maji/umeme, vyombo vya kulishia nk....
Swali:
Ukiwa na 1.5m unahitaji vifaranga wangapi? Jibu lako liwe kwenye makumi ya karibu...[emoji41]
 
Sijakuelewa lakini nilichokiona hapa ni kuwa ukiwa na kiasi cha fedha ambacho unakitegemea kitakuwezesha kwenye jambo hasa la ufugaji unatakiwa ujiandae vizuri kisaikolojia maana pesa unaweza iandaa lakini katika ufugaji ulichoshauriwa na utakachokutana nacho unapoanza kufuga ni tofauti mambo ni mengi yanaweza jitokeza hasa magonjwa kwenye kuku au gharama za vyakula vya kuku kupanda na nk lakini yote kwa yote maisha ni kupambana wacha nianze hivyo hivyo.
 
Ndugu inatosha na chenji inabaki, nunua mahindi hata gunia kumi uwe unayasaga mwenyewe chakula cha kuku na kununua gradients za kuchanganyia mwenyewe utakuwa unatumia si zaidi ya laki mbili kwa mwezi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…