Bajeti ya 2015/2016 kipimo tosha kwa waziri wa fedha

Bajeti ya 2015/2016 kipimo tosha kwa waziri wa fedha

ego

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2013
Posts
1,620
Reaction score
1,407
Shilingi ya Tanzania imekuwa ikishuka thamani kila mwaka lakini hivi karibuni shilingi hii imeonekana kuporomoka na sio kushuka kwa kawaida.

Kiuchumi, kushuka kwa thamani ya shilingi ni ishara ya kutokuwa na wataalamu wenye uwezo wa kudhibiti uchumi wetu hasa bajeti. Bajeti ndio nyenzo kuu ya kudhibiti thamani ya shilingi au ndio nyenzo kuu ya kudhibiti uchumi wa nchi.

Tulimsikia Gavana wa Benki Kuu akitoa maelezo juu ya kushuka kwa thamani ya shilingi yetu ambayo ki mtizamo ni maelezo ya kweli miongoni mwa sababu nyingine lakini ni aibu kwa nchi inayotengeneza bajeti na katika kutekeleza bajeti hiyo shilingi inaporomoka.

Ni vigezo vipi mnavitumia kutengeneza bajeti kama kuitekeleza bajeti yenu tunafilisika? Bajeti hii nadhani iwe ni kipimo kwa waziri na wataalamu wake kama kweli they are serious na uchumi wetu.
 
Nikiri Mm si mchumi. Lakini kama hauna mauzo ya kutosha nje ili upate foreign currency. Zaidi matumiz ya serikali ni makubwa mno hasa manunuzi ya magari, furniture, safari zisizo na tija nje ya nchi
 
unaweza kuwa si mchumi mwenye cheti ukawa mchumi kwa ideas lakini yupo mwingine anaweza kuwa na cheti cha uchumi lakini hawezi kuunganisha maisha ya kawaida na theory za uchumi.

kushuka kwa shilingi kunalinganisha imports na exports.

pale nchi inapokuwa ina matumizi makubwa kutoka nje kuliko mauzo yake ya nje fedha yake inaporoka lakini ukiuza nje sana kuliko mahitaji yako ya kutoka nje uchumi wa nchi unaimarika nafedha yake inapanda bei.

hapa ndipo penye wajibu wa waziri wa fedha kudhibiti mahitaji yetu ya nje kwa mwaka yasizidi manunuzi na fedha yetu ikaporomoka.

haya anatakiwa kuyafanya kupitia viwango vya kodi ingawa serikali nzima inatakiwa kuhusika kuweka mikakati maana yeye akitumia kodi kudhibiti uchumi bila jitihada za sekita nyingine kuangalia jinsi gani wananchi hawa wanapata mahitaji yao kutoka ndani ya nchi inakuwa kazi ngumu.

mbali na viwango vya kodi ni lazima yeye a set kiwango cha fedha kinachotakiwa kununua bidhaa nje ambacho kiko katika safe side kulingana na uwezo wetu wa exports na hicho ndicho wizara zinazotaka utekeleza miradi ya kutegemea imports zibanwe kubaki humomhumo.

lakini yawezekana wataalamu wetu wanaangalia uwiano wa matumizi na mapato tu bila idea ya kuthibiti uchumi wetu.

Nikiri Mm si mchumi. Lakini kama hauna mauzo ya kutosha nje ili upate foreign currency. Zaidi matumiz ya serikali ni makubwa mno hasa manunuzi ya magari, furniture, safari zisizo na tija nje ya nchi
 
Back
Top Bottom