Bajeti ya Kenya ni Tsh. Trilioni 78, Tanzania ni Tsh. Trilioni 34 na Uganda Tsh. Trilioni 30

Bajeti ya Kenya ni Tsh. Trilioni 78, Tanzania ni Tsh. Trilioni 34 na Uganda Tsh. Trilioni 30

Nyamsusa JB

JF-Expert Member
Joined
Jul 9, 2015
Posts
567
Reaction score
1,564
Kwa Bajeti hizi za Africa Mashariki Kenya itazidi kupaa sana. Bajeti ya Kenya ni takriban mara mbili ya Bajeti ya Tanzania. Ukijumlisha Bajeti ya Tanzania na Uganda bado haifikii Bajeti ya Kenya.

Hii inaonyesha Kenya inaweza Kuendelea mara Mbili zaidi ya Tanzania na Uganda. Nadhani kuna kitu Tanzania tunahitaji kufanya. Kenya hawezi kua na Bajeti mara mbili kutuzidi wakati sisi Tanzania tuna Mambo mengi wezeshi kuwazidi.

Imeniumiza Roho sana hii.
 
Tanzania, bado tunasumbuliwa na fikira za kijamaa (ujamaa wa Nyerere) ambazo haziko mbali sana na ujima! Inahitajika mkakati kabambe wa kufutilia mbali fikira za kijima ambapo ni pamoja na kusikia watu wanajivunia kuitwa 'wanyonge', kujisifu kuwa ni 'matajiri' huku unafungia wenye mitaji na teknolojia milango, nk
 
Wakenya wanatuzidi utapeli na huku Sisi tumezubaa..

Mfano asilimia 80 ya watalii wetu wanapitia Kenya...

Tungekuwa wajanja tungeifanya KIA kuwa the biggest Transit Airport in Africa...
Ingesaidia mno watalii wanakuja wanatua kwanza KIA halafu ndo wanaamua kwenda Kenya au Dar au Zanzibar...

Hili kufanyika linahitaji brains sio blah blah
 
Wakenya wanatuzidi utapeli na huku Sisi tumezubaa..

Mfano asilimia 80 ya watalii wetu wanapitia Kenya...
Hawawezi kufikiri kama hivi watu wapo kwa ajili ya matumbo yao,hawawazi ya mbele
 
Bajeti kubwa haiimaanishi kwamba ndio inaleta maendeleo. Kenya wanabandika manamba makubwa kwa sababu kwa sehemu kubwa wanatumia Expenditure-Driven budget yaani sehemu kubwa wanapanga bajeti kwa ajili ya matumizi zaidi kuliko maendeleo na kulipa madeni pia. Mpaka ninapoandika hapa Kenya inakopa zaidi ya nchi zote ukimjulisha kwa pamoja hapa Afrika mashariki ili kujazilishia bajeti yao.

Binafsi naamini tupaswa kuwa na bajeti isiyozidi trilioni 30 maana uwezo wa ukusanyaji wetu wa mapato ni trilioni 25 tu. Tuwe na bajeti inayotokana na mapato zaidi (Revenue-Driven budget) halafu tufanye miradi michache ila ipate uwekezaji mkubwa na serikali ipunguze gharama za uendeshaji ikiwemo kuyaondoa mashirika ya umma yanayojishughulisha na biashara kama ATCL, wao wajikite ktk kutoa huduma tu.

Wakenya kiujumla wana akili ndogo sana kichwani. Kama asingekuwa Mwl. Julius Nyerere na sera mbovu baada ya vita dhidi ya Uganda sisi tulipaswa kuwa nchi yenye uchumi mkubwa ukanda huu wa Afrika mashariki. Edwin Mtei alijitoa nafasi yake kama waziri wa fedha baada ya Mwl kukataa sera ambazo Rais Ali Mwinyi na Rais Benjamini Mkapa walikuja kuzitekeleza baadae na nchi ikasimama kidogo kuliko tulivyozidi kupotea.
 
Back
Top Bottom