bajeti ya music wa gari

Ingekuwa vizuri wewe ukasewma bajeti yako uliyoweka kwa ajili ya kazi hiyo. Then ndo wadau wakushauri kulingana na bajeti yako.
Mkuu nahitaji mziki wa kawaida sana hivyo bajeti yangu n laki 2.
 
Leo pale Sinza nimembiwa kufunga sabwoofer pekee huku kwenye buti ya babywoka yangu gharama yake ni 200,000. Dah, nimeghairi.
 
Linapokuja suala la kusikiliza music system aisee tusidanganyane hakuna kuhitaji Mziki mdogo sijui wakatikati labda Kama unalenga upande wa sauti(volume) lakini suala la Mziki ni mtambuka Yani hakuna asiependa kusikia sound nzuri (deep bass, quality sorrounding n k) hivyo msikilizaji anatamani asikie kilakitu kilichotengenezwa studio na producer, Sasa hapo shida NDIPO inapoanza maana kusikia kila kitu ni garama, Mziki unabebwa na sauti ya chini (lower herts/Hz) ambazo ni bass inayoanzia hz15 Hadi Hz60 , Sasa garama inakuwa kubwa kupata speaker(subwoofer) inayokokotoa kuanzia Hz15/20-50 kadri Hz zinapokua chache NDIPO iyo Bei ya speaker inapokuwa juu

Sasa najalibu kucheza na mtoa post kuwa hapo anahofia bajeti yake tu sio kweli kuwa haitaji Mziki Quality😁

Njia fupi nunua subwoofer yenye watts kuanzia 400rms Hadi 700 hii Ni kwa NCHI 12" (size ya iyo spk) nunua mbili Kisha mtafute fundi box aziweke box moja.

Nunua amplifier kulingana na Spk zako mfano Kama umenunua Pioneer mbili zenye 400rms watts basi nunua amplifier yenye KUTOA kila channel 400watts mfano Kama amplifier Ina 1600watts ikiwa ni 4channel basi kila channel inatoa 400watts .

Nunua Pre-amp(equalizer) hii nikuchakata mgawanyo wa mfumo wa Mziki Yani sub bass, bass, mid, mid hi na super hi(nunua ya band7(Sana)
PATA redio(head unit) nzuri yenye chaguo(option ) za kisasa Kama flash, memory, Bluetooth, n. K.

Mtafute fundi MZURI akupe ushauri kabla ya vyote,
 
Aloo kuna wajomba huko kenya, uarubuni, ujerumani wanakufungia gari mziki una subwoofer mpaka 4 na kila moja inatema sio chini 800 watts rms sio poa aisee, uko tandale mziki unasikika posta mamaeeee

Hivi mziki mkubwa hau athiri performance ya gari?

Hasa hizi zenye engine ndogo mfano 1500cc
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…