Bajeti ya Serikali na mpango wa maendeleo wa Taifa kwa mwaka 2021/22: Serikali inatarajia kukusanya na kutumia jumla ya Sh. trilioni 36.26

Bajeti ya Serikali na mpango wa maendeleo wa Taifa kwa mwaka 2021/22: Serikali inatarajia kukusanya na kutumia jumla ya Sh. trilioni 36.26

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
SERIKALI imesema katika mwaka wa fedha 2021/22 inatarajiwa kukusanya na kutumia Sh. trilioni 36.26, sawa na ongezeko la asilimia 4.0 ya bajeti ya mwaka 2020/21 ya Sh. trilioni 34.88.

Maeneo ya kipaumbele mwaka huu ni kuchochea uchumi shindani na shirikishi, kuimarisha uwezo wa uzalishaji viwandani na utoaji huduma, kukuza biashara, kuchochea maendeleo ya watu na kuendeleza rasilimali watu.

Jana, Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Mwigulu Nchemba akiwasilishabBungeni mapendekezo ya mwongozo wa maandalizi ya mpango, bajeti ya serikali na mpango wa maendeleo wa taifa kwa mwaka 2021/22, alisema serikali inatarajia kukusanya na kutumia jumlaya Sh. trilioni 36.26.

Mwigulu aliwasilisha mapendekezo hayo, kwa niaba ya Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango, na kusema:

“Ongezeko hilo linatokana na mahitaji ya mfuko mkuu wa serikali ikijumuisha malipo ya deni la serikali, mahitaji ya upandishwaji wa madaraja ya watumishi na ajira mpya.

“Na mahitaji ya Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA), Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA).”

Kupitia mpango wa maendeleo wa miaka mitatu, serikali imejikita zaidi katika kukuza uchumi wa nchi kupitia sekta za viwanda, biashara na uwekezaji.

Kwenye mapendekezo hayo, maeneo yaliyozingatiwa katika mpango huo ni kiwango cha ukuaji wa uchumi kwa mwaka, mapato ya ndani ikijumuisha mapato ya halmashauri kuongezeka, mfumuko wa bei kuendelea kubaki katika wigo wa tarakimu moja, akiba ya fedha za kigeni kukidhi mahitaji na sekta binafsi kuzalisha ajira mpya zipatazo milioni nane.

Aidha, Dk. Mwigulu aliwasilisha Mapendekezo ya Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa miaka mitano wa mwaka 2021/22-2025/26.

Akizungumzia mpango wa kitaifa wa 2021/22 pamoja na mwongozo wa bajeti ya mwaka huo wa fedha, Waziri Mwigulu, alisema katika eneo la kuchochea uchumi shindani na shirikishi, litajumuisha miradi itakayojikita katika kujenga jamii yenye uwezo wa kushindana kikanda na kimataifa na kuimarisha utulivu wa uchumi.

“Pia litajikita katika kuimarisha mazingira ya biashara na uwekezaji, kuimarisha uvumbuzi na uhawilishaji wa teknolojia kutoka nje na kuendeleza miundombinu na huduma katika maeneo ya reli, barabara, madaraja, usafiri wa majini, usafiri wa anga, TEHAMA (Teknolojia ya Habari na Mawasiliano), nishati, bandari na viwanja vya ndege.

Vile vile, alisema katika kuimarisha uwezo wa uzalishaji viwandani eneo hilo litajumuisha kuendeleza viwanda vya uzalishaji wa dawa kwa matumizi ya binadamu, miradi ya viwanda inayolenga kuongeza thamani ya mazao ya kilimo, mifugo, uvuvi na madini.

Katika kukuza biashara, alibainisha kuwa eneo hilo litajumuisha programu za kuimarisha masoko ya ndani na kutumia fursa za masoko ya kikanda na kimataifa.

Kuhusu kuchochea maendeleo ya watu, alisema eneo hilo litajumuisha utekekelezaji inaojikita katika kuboresha maisha ya watu ikiwemo kuboresha elimu na mafunzo katika ngazi zote; afya na ustawi wa jamii, kinga ya jamii, huduma za maji na usafi wa mazingira; mipango miji, na nyumba na maendeleo ya makazi.

Alisema pia eneo lingine la kuendeleza rasilimali watu litajumuisha programu na mikakati inayolenga kuendeleza ujuzi wa rasilimali watu nchini, kuanzia ngazi za elimu ya awali hadi elimu ya juu ikiwemo kuwawezesha vijana kujiajiri.

Alisema pia mpango na mwongozo huo, utajumuisha miradi ya kielelezo inayoendelea ambayo utekelezaji wake unatarajiwa kuwa na matokeo makubwa na ya haraka katika uchumi.
 
Matrilioni😂 😂 😂 vyanzo vipi vya makusanyo?

Vitambulisho vya wamachinga?

Au bado wapo wale wa kusema dipipii!?

Au za kubrashia viatu zinataifishwa?

Au pesa za beberu dhidi ya Diportivo?

Hii inachekesha hata mabeberu wenyewe wako very cautious na huu uchumi uliotetereshwa na games za Deportivo!

Yetu macho! 5 tena!

Everyday is Saturday................................😎
 
Dr. Mpango ni kitu gani kimemkuta mpaka kashindwa kuwasikisha mpango wake wa Mwaka?
 
Hadi wauza mchicha mnawakamua Kodi, Tena mnawabambukizia

Wanaongeza pesa kwa Tanapa, tawa na ncca ili iwe rahisi kuziiba au kubadilisha matumizi.... Wanaacha kuongeza ruzuku ktk kilimo Au kuongeza miradi ya uzalishaji wa mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi inayo msaidia raia moja kwa moja...

Nchi bado ipo chini ya wakoloni weusi...
 
Hongera serikali.

Hongera Rais wetu.

Hivi nani alitarajia nchi yetu itakua na neema kiasi hiki.

Yaani mwendo wa matrillion tu.

Kweli awamu zilizopita mafisadi yaliiba sana.

Haya matrillion yote yalikua yanaenda kwao.

Jamani Tanzania ya Magufuli neema tupu isipokua kwa wapiga dili Yaani lazima waumie tu maana mianya imeziba kabisa
 
Back
Top Bottom