Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepitisha bajeti ya Wizara ya Ujenzi kwa mwaka wa fedha 2025/26 ya Shilingi trilioni 2.28, ikiwa ni ongezeko la takribani asilimia 28.89 kutoka trilioni 1.769 ya mwaka 2024/25. Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega, amesema bajeti hiyo inalenga kuharakisha utekelezaji wa miradi ya kimkakati ya maendeleo.
Soma, Pia: Mbunge wa Sumve apinga Bajeti ya Ujenzi, adai kuchoshwa na Uongo wa Miaka mingi
Maelezo: Bajeti hii imepitishwa na Bunge tarehe 6 Mei 2025, ikiwa na vipaumbele katika sekta ya ujenzi wa miundombinu ya barabara na madaraja. Malipo kwa wakandarasi wa ndani na nje wanaotekeleza miradi ya barabara, Utekelezaji wa miradi 81 ya dharura yenye thamani ya TSh bilioni 559.6 (ikiwa 70 zinatekelezwa na wakandarasi wazawa), Kuendeleza ujenzi wa barabara ya Mtwara–Mingoyo–Masasi,
Pia, Matumizi ya kawaida ya wizara na taasisi zake yakiwa ni TSh bilioni 90.47, huku TSh trilioni 2.19 zikielekezwa kwenye miradi ya maendeleo.