Kweli nimeingia kwenye huu mchezo na huu mchezo unatumia akili, sio akili Peke yake tu, kuna MB kuna ku deposit kiasi cha hela kuendelea kuzungusha hizo machine. Mbaya zaidi, tuna mbunge mwenye kujua hiki kitu huko bungeni, haitoshi tuna Naibu Waziri, Naibu kijana wa juzijuzi anajua kizazi chetu kilivyoathirika na kamari na wengi wao ni waraaibu wa kamari online, wanaoweka mikeka, na wanaoumia hasa ni wale wa upande wa michezo ya kubahatisha; Online Casino.
Waheshimiwa licha ya madini, utalii na mengineyo sekta hii ya kubeti ni chanzo kipya cha mapato ya serekali kisichochukuwa uhai wa mtanzania yoyote kama bodaboda na wachimbaji wa madini ambao taarifa zao vifo vyao huwekwa hadharani kila uchwao hadi sasa, tofouti na waraibu wa kamari wa nchi zengine.
Waheshimiwa, je, vijana waendelee kubeti wakiamini wanaweza kutoboa au wauze bangi, mirungi au madawa kabisa ama tuwasapoti kutokana na ukuaji wa tekenolojia kwenye chanzo hichi cha mapato?
Tuna jambo la kufanya kuanzia TRA mnapochukua kodi za kamari, mitandao ya simu, hadi sisi wasimamizi serekali kwa kuu. Michezo ya kubashiri, mpira wa miguu na upande wa betting online hasa casino, kutokana na ukosefu wa Internet imara, bora isiruhusiwe kwanza nchini mwetu Tanzania hadi tutapokuwa na Internet imara kwa mchezaji.
Unakuta mtu ameweka hela yake amepigwa round kadhaa,muda anakula Internet inakata! Nani anawajibika hapa? Na hili nalo tukaliangalie kabla vijana wetu hawajaanza kuchukua hatua mbaya zaidi kutokana na uraibu wa kamari.