PreGE2025 Bakari Kimwanga, achukua fomu kutetea nafasi yake ya udiwani kata ya Makuruml

PreGE2025 Bakari Kimwanga, achukua fomu kutetea nafasi yake ya udiwani kata ya Makuruml

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Aliyekuwa Diwani wa Kata ya Makurumla,Bakari Kimwanga, amechukua fomu kitetea nafasi hiyo ambayo ameiongoza kwa miaka mitano iliyopita

Leo Juni 29,2025 amekabidhiwa fomu na Katibu wa Kata wa CCM Makurumla, Omari Suleiman Bakari.

Akizungumza baada ya kukabidhi fomu hiyo, Kimwanga ambaye pia ni mwanahabari na Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Dar es Salaam, amesema kuwa anajivunia kazi kubwa aliyoifanya kwa miaka mitano na sasa anaomba fursa kwenye kukamilisha maeneo yaliyobaki ili kujenga jamii yenye ustawi.

"Ninamaliza miaka mitano ya mafanikio ambapo sisi Makurumla tumefanikiwa kutekeleza miradi ya zaidi ya bilioni 18 ikiwamo barabara, kituo cha afya na elimu.

Soma Pia: Uzi maalum wa wanaotia nia kugombea Ubunge Uchaguzi Mkuu 2025​

"Miaka mitano ijayo tunakwenda kujenga kata yenye kasi zaidi na muonekano mkubwa wa maendeleo kwa jamii, wana Makurumla na wana CCM ni watu wema sana nyakati zote tumekuwa pamoja na Mungu akipenda ikiwa chama itawapendeza jina likarudi kwenye uteuzi sina shaka na maamuzi yao kwangu na chama chetu ni ushindi," amesema Kimwanga.

Screenshot 2025-06-29 165434.png
 
Back
Top Bottom