Bakari Shime aliwahi kufanikiwa katika lipi ?

Bakari Shime aliwahi kufanikiwa katika lipi ?

Mapendekezo - Bakari Shime afukuzwe kazi , apewe kocha mwenye uwezo .
 
Kuboronga kwa Serengeti Boys kwenye michuano ya vijana hakuwezi kupita tu hivi hivi kama upepo bila kujadiliwa .

Mafanikio ya timu yoyote ya soka kwa kiwango kikubwa huchangiwa na kocha wa timu husika , ikumbukwe pia kwamba ubovu wa kocha waweza kuchangia kuboronga kwa timu.

Leo sina mengi sana , nimeangalia wale vijana wakicheza na Niger kupitia ZBC2 , Nikashangaa na kujiuliza walifikaje kwenye michuano Mikubwa kama ile , wakati natafakari nikagundua kwamba walitokea JUU YA MEZA .

Baada ya hapo nikaanza kufuatilia mafanikio ya kocha wake aitwaye Bakari Shime , kiukweli mpaka sasa sijaona mafanikio ya mtu huyu kiasi cha kupewa kazi ya kufundisha timu hii , Shime aliyewahi kufundisha JKT RUVU ( niko tayari kusahihishwa ) , timu inayopanda na kushuka ligi kuu hana na wala hajawahi kuwa na uwezo wa kufundisha soka , kama kuna anayefahamu mafanikio yake atuwekee hapa.

Inakuwaje mtu asiye na sifa yoyote kukabidhiwa timu ya Taifa ? Ukiangalia wale vijana walivyokuwa wanacheza utagundua jambo moja tu , kwamba waliambiwa wakishinda watapata hela na kwenda kombe la dunia , baaaasi !!!! Wala hawakuambiwa wacheze vipi ili washinde , hata kupiga mpira juu hawakuweza !

Ni kweli kwamba wapo wanaoshinda mamilioni ya hela kwa Kubeti , baada ya kutumia tsh 500 , lakini si kwenye soka , soka inataka uwekezaji wa kweli hasa , Wachezaji waandaliwe kwa kiwango cha juu tena chini ya Mwl anayejua aliyezungukwa na historia yenye mafanikio haswa , haya mambo ya Bahatisha Ndulute hayatatufikisha popote , ni bora kujitoa kuliko kudhalilishwa mara kwa mara .

Natanguliza uzalendo , asanteni .
Walitokea juu ya meza? Mafanikio ya Shime ni pamoja na kufika kwenye hii machuano
 
Bakari shime moja ya makocha watazanzania bora kabisa kwa wakati huu, mtoa mada huenda umeanza kuifatilia Serengeti juzi ila kama ungeanza kuangalia toka zamani usingesema hivyo. Shime katusaidia tumepita timu nyingi ngumu zenye investment ya kutosha kama south Africa. Africa kuna nchi zaidi ya 50 ila tumekua mmojawapo kati ya timu nane tu zilizoingia fainali ya mashindano. Heb tujifunze kuapreciate mambo mazuri
 
Tunakushukuru kwa kumremba Bakari Shime , lakini kwa bahati mbaya soka inataka ushindi na wala si porojo .
 
Back
Top Bottom