Bakili Muluzi: Rais wa pili wa Malawi mwanamapinduzi na mwanamageuzi wa kweli

Mr Dudumizi

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2020
Posts
7,971
Reaction score
14,538
Niaje waungwana.

Leo katika historia ya nchi tunazopeana nazo mpaka, ningependa nikuletee hostoria ya nchi ya Malawi chini ya uongozi wa mwana mapinduzi wa kweli, mwana mageuzi ya uchumi na maendeleo ya nchi hiyo. Na si mungine, ni muheshimiwa Bakili Muluzi.

Mhe. Bakili ambae jina lake halisi ni Elson Bakili Muluzi, kutoka kabila la wayao, alizaliwa 17 March 1943, huko Machinga, Nyasaland ambayo kwasasa inajulikana kama Malawi.

Baada ya elimu, Bakili Muluzi alikuwa kati ya vijana machachari mno ambao walipambana na mfumo wa kibeberu uliokuwa unaongozwa na serikali ya kingereza, chini ya malkia Elizabeth.

Baada ya uhuru, nchi hiyo iliongozwa na mpigania uhuru wa nchi hiyo hayati Hastings Kamuzu Banda ambae baadae aligeuka na kuwa dekteta hatari nchini Malawi. Ndugu Muluzi alichaguliwa na raisi Banda kuwa miongoni mwa mawaziri wake.

Baadae Muluzi alijiuzulu uwaziri chini ya serikali ya Banda, baada ya raisi Banda kuanza kuiongoza Malawi kwa mkono wa chuma. Banda alianza kufuta vyama vyote vya siasa ili aongoze yeye tu maisha yake yote. Hili lilifanywa na viongozi wengi waliopigania uhuru miaka ile including baba wa taifa letu hayati Julius Nyerere, hayati mzee Kaunda, hayati mzee Kenyata nk.

Inasemekana raisi Banda alifikia hatua ya kula viuno mpaka vya wenza wa mawaziri wake.
Yani waziri unatumwa nje ya nchi, halafu huku nyuma Banda anamtafuna mama chanja wako, na ukijifanya kutaka kujua kuhusu swala hilo, unatupwa ndani, unapotezwa au kuuwawa kabisa. Nchi nzima ilimuogopa raisi Banda. Hakuna aliethubutu kufungua kinywa chake kuhoji uendeshaji wa serikali yake, wala vitendo vyake. Wananchi waliishi kama kuku wenye mdondo, wasijue kesho yao itakuaje.

Raisi Banda akawa dikteta jeuri na kiburi mpaka kufikia hatua ya kugombana na hayati baba wa taifa mhe. Julius Nyerere, baada ya Banda kudai kwamba maeneo yote ya Tanzania yaliopo pembezoni mwa ziwa Nyasa kama vile mkoa wa Ruvuma nk ni sehemu za Malawi, hivyo siku Malawi ikizihitaji sehemu hizo itazichukua iwe ni kwa nguvu au maelewano. Hapo ndo vita ya mpaka kati ya Tanzania na Malawi ikazuka rasmi baada ya Nyerere nae kumuahidi mzee Banda kuwa akithubutu kufanya kile anachofikiria, basi atakuwa ameigawa yeye mwenyewe nchi yake kwa Tanzania, kwani tutaitwanga Malawi na kuichukua yote kuifanya ni sehemu ya Tanzania na Kamuzu Banda atashushwa cheo ili kuwa mkuu wa wilaya tu wa Nyerere (kwa huruma yake) Nyerere. Banda kusikia hivyo akanywea.

Baada ya mfumo wa vyama vingi kurudi kwa kasi barani Afrika na viongozi wa nchi hizo kubanwa kisawa sawa na mabeberu ili waruhusu mifumo ya demokrasia katika nchi zao. Raisi Banda hakuwa na chaguo lingine zaidi ya kukubaliana na mfumo huo kwa shingo upande huku akitegemea mfumo wake kumbeba katika chaguzi mbali mbali ambazo zingefanyika nchini kwake.

Mwaka 1994 ukafanyika uchaguzi wa vyama vingi ambapo kati ya wagombea wa uraisi alikuwepo kiongozi machachari wa chama cha upinzani cha UDF ndugu Bakili Muluzi na wagombea wa vyama vingine. Katika kinyanganyiro hicho mzee Banda alikuwa na uhakika wa kushinda kupitia mfumo wake alioutengeneza mwenyewe ili hata akishindwa, umtangaze yeye mshindi.

Katika hali iliyowashangaza wengi, mzee Banda akajikuta kaangukia pua vibaya mno kwa kupata kura chache ambazo zilisababisha ugumu wa mfumo wake kumbeba.

Bakili Muluzi akaandika historia ya raisi mpya wa Malawi kutoka kabila dogo la wayao ambao sio wengi kama wachewa. Pia raisi mpya na mwanzo mpya baada ya nchi hiyo kuwa chini ya uongozi wa kidikteta kwa takriban miaka zaidi ya 30, huku nchi hiyo ikiwa imejazwa viongozi wa serikali, jeshi, polisi, mahakama na bunge kutoka upande mmoja wa kabila la mtawala (Kamuzu Banda)

Baada ya Muluzi kuingia akawa na kazi ya:
1. Kufungua uchumi uliodumazwa na kufubazwa na uongozi wa mzee Banda.
2. Kuunganisha wananchi wa Malawi kwa kuchanga makabila katika sehemu ambazo kabila la mzee Banda lilionekana kujazwa huko hata kam waliojazwa hawana elimu wala sifa za kuwa huko. Hii ni pamoja na serikalini, jeshini, mahakamani, bungeni, maofisini, polisi nk.

3. Akaruhusu sekta binafsi kujisimamia zenyewe bila kuingiliwa na serikali, lakini kwa kufuata sheria za nchi (hii nahisi aliitoa kwa mzee ruhusa)
4. Wafanyabiashara waliokuwa wanazuiwa kuagiza, au kuleta vitu kutoka nje nao wakaruhusiwa kuagiza au kuleta vitu kutoka nje (hii pia nafikiri ni mzee Mwinyi legacy)

Nchi ikaanza kuchangamka, wananchi wakaanza kuwa huru, maendeleo yakaingia Malawi, wafanyabiashara kutoka Tanzania haswa mikoa ya Mbeya na Ruvuma wakaanza kuingia Malawi kufanya biashara bila buguza yoyote. Na wa Malawi wakaanza kuja Tanzania pia kufanya biashara zao.

Ule urafiki na udugu wetu uliokuwa umeanza kufifia baada ya Banda kupiga mkwara wa kuivamia Tanzania, ukaanza kurudi tena. Hela mitaani ikaanza kuonekana, unea onea ya polisi na jeshi kwa raia ikakoma. Mahakama zikawa huru, bunge huru na wananchi huru.

Kamuzu Banda akapata presha akifikiri labda atafungwa na Muluzi kutokana na unyama aliofanya kwa nchi yake. Lakini wala haikuwa hivyo. Muluzi ali focus katika kujenga, kuiimarisha na kuiletea maendeleo nchi yake. Banda ile hali ilimtesa sana maana hakuwa tena na mtu wa kumpigia propaganda za kuwafubaza wamalawi kama alivyokuwa madarakani. Mabaya yake yote yalijulikana. Vyombo vya habari havikuogopa tena kuandika ushenzi aliokuwa anaufanya.

Matokeo yake mzee wa watu akajifia na stress za kuzomewa na kutupiwa vidale vya lawama kila alipokwenda, togauti na wapigania uhuru wenzake ambao waliheshimiwa na kuthaminiwa.

Bakili Muluzi aliiongoza Malawi kwa miaka 10, kutoka 1994 hadi 2004 akaacha nchi ikiwa yenye mifumo mizuri ya kiuongozi kuanzia mahakama, bunge, na serikali.

Alipotoka akaingia kijana wake Bingu Mutharika ambae, yeye muda mfupi tu wa uongozi wake akagombana na mtangulizi wake (Muluzi) na kuanza kuirudisha nchi kimya kimya katika utawala ule ule wa Kamuzu Banda.

Yeye Mutharika alienda mbali kwa kutoka katika chama cha aliemuachia madaraka (Muluzi) ambae alimpigia debe ili awe raisi baadae yake. Mutharika alianza udikteta uchwara kwa kuanzisha chama chake akiwa madarakani (katiba yao inaruhusu) na kuanzisha chama chake.

Hakuishia hapo, bali alimtupa ndani hata aliekuwa boss wake wa chama, na raisi wake, ambae pia alimchagua kugombea nafasi yake ya uraisi (Muluzi). Baada ya kumtupa Muluzi ndani akaendesha nchi hiyo kwa mkono wa chuma kimya kimya, na kuhakikisha kila mtu anamuogopa, hadi alipopatwa na umauti wa ghafla mwaka 2012, wakati akikimbizwa Afrika Kusini kwa ajili ya matibabu kutokana na ugonjwa wa mshituko wa moyo.
Screenshot_20250515_133633_Samsung Internet.jpg
 
Moderators naombeni hiyo picha muiweke katika mtazamo mzuri na iwe kwa juu.
Natanguliza shukrani kwenu.
 
Niaje waungwana.

Leo katika historia ya nchi tunazopeana nazo mpaka, ningependa nikuletee hostoria ya nchi ya Malawi chini ya uongozi wa mwana mapinduzi wa kweli, mwana mageuzi ya uchumi na maendeleo ya nchi hiyo. Na si mungine, ni muheshimiwa Bakili Muluzi.

Mhe. Bakili ambae jina lake halisi ni Elson Bakili Muluzi, kutoka kabila la wayao, alizaliwa 17 March 1943, huko Machinga, Nyasaland ambayo kwasasa inajulikana kama Malawi.

Baada ya elimu, Bakili Muluzi alikuwa kati ya vijana machachari mno ambao walipambana na mfumo wa kibeberu uliokuwa unaongozwa na serikali ya kingereza, chini ya malkia Elizabeth.

Baada ya uhuru, nchi hiyo iliongozwa na mpigania uhuru wa nchi hiyo hayati Hastings Kamuzu Banda ambae baadae aligeuka na kuwa dekteta hatari nchini Malawi. Ndugu Muluzi alichaguliwa na raisi Banda kuwa miongoni mwa mawaziri wake.

Baadae Muluzi alijiuzulu uwaziri chini ya serikali ya Banda, baada ya raisi Banda kuanza kuiongoza Malawi kwa mkono wa chuma. Banda alianza kufuta vyama vyote vya siasa ili aongoze yeye tu maisha yake yote. Hili lilifanywa na viongozi wengi waliopigania uhuru miaka ile including baba wa taifa letu hayati Julius Nyerere, hayati mzee Kaunda, hayati mzee Kenyata nk.

Inasemekana raisi Banda alifikia hatua ya kula viuno mpaka vya wenza wa mawaziri wake.
Yani waziri unatumwa nje ya nchi, halafu huku nyuma Banda anamtafuna mama chanja wako, na ukijifanya kutaka kujua kuhusu swala hilo, unatupwa ndani, unapotezwa au kuuwawa kabisa. Nchi nzima ilimuogopa raisi Banda. Hakuna aliethubutu kufungua kinywa chake kuhoji uendeshaji wa serikali yake, wala vitendo vyake. Wananchi waliishi kama kuku wenye mdondo, wasijue kesho yao itakuaje.

Raisi Banda akawa dikteta jeuri na kiburi mpaka kufikia hatua ya kugombana na hayati baba wa taifa mhe. Julius Nyerere, baada ya Banda kudai kwamba maeneo yote ya Tanzania yaliopo pembezoni mwa ziwa Nyasa kama vile mkoa wa Ruvuma nk ni sehemu za Malawi, hivyo siku Malawi ikizihitaji sehemu hizo itazichukua iwe ni kwa nguvu au maelewano. Hapo ndo vita ya mpaka kati ya Tanzania na Malawi ikazuka rasmi baada ya Nyerere nae kumuahidi mzee Banda kuwa akithubutu kufanya kile anachofikiria, basi atakuwa ameigawa yeye mwenyewe nchi yake kwa Tanzania, kwani tutaitwanga Malawi na kuichukua yote kuifanya ni sehemu ya Tanzania na Kamuzu Banda atashushwa cheo ili kuwa mkuu wa wilaya tu wa Nyerere (kwa huruma yake) Nyerere. Banda kusikia hivyo akanywea.

Baada ya mfumo wa vyama vingi kurudi kwa kasi barani Afrika na viongozi wa nchi hizo kubanwa kisawa sawa na mabeberu ili waruhusu mifumo ya demokrasia katika nchi zao. Raisi Banda hakuwa na chaguo lingine zaidi ya kukubaliana na mfumo huo kwa shingo upande huku akitegemea mfumo wake kumbeba katika chaguzi mbali mbali ambazo zingefanyika nchini kwake.

Mwaka 1994 ukafanyika uchaguzi wa vyama vingi ambapo kati ya wagombea wa uraisi alikuwepo kiongozi machachari wa chama cha upinzani cha UDF ndugu Bakili Muluzi na wagombea wa vyama vingine. Katika kinyanganyiro hicho mzee Banda alikuwa na uhakika wa kushinda kupitia mfumo wake alioutengeneza mwenyewe ili hata akishindwa, umtangaze yeye mshindi.

Katika hali iliyowashangaza wengi, mzee Banda akajikuta kaangukia pua vibaya mno kwa kupata kura chache ambazo zilisababisha ugumu wa mfumo wake kumbeba.

Bakili Muluzi akaandika historia ya raisi mpya wa Malawi kutoka kabila dogo la wayao ambao sio wengi kama wachewa. Pia raisi mpya na mwanzo mpya baada ya nchi hiyo kuwa chini ya uongozi wa kidikteta kwa takriban miaka zaidi ya 30, huku nchi hiyo ikiwa imejazwa viongozi wa serikali, jeshi, polisi, mahakama na bunge kutoka upande mmoja wa kabila la mtawala (Kamuzu Banda)

Baada ya Muluzi kuingia akawa na kazi ya:
1. Kufungua uchumi uliodumazwa na kufubazwa na uongozi wa mzee Banda.
2. Kuunganisha wananchi wa Malawi kwa kuchanga makabila katika sehemu ambazo kabila la mzee Banda lilionekana kujazwa huko hata kam waliojazwa hawana elimu wala sifa za kuwa huko. Hii ni pamoja na serikalini, jeshini, mahakamani, bungeni, maofisini, polisi nk.

3. Akaruhusu sekta binafsi kujisimamia zenyewe bila kuingiliwa na serikali, lakini kwa kufuata sheria za nchi (hii nahisi aliitoa kwa mzee ruhusa)
4. Wafanyabiashara waliokuwa wanazuiwa kuagiza, au kuleta vitu kutoka nje nao wakaruhusiwa kuagiza au kuleta vitu kutoka nje (hii pia nafikiri ni mzee Mwinye legacy)

Nchi ikaanza kuchangamka, wananchi wakaanza kuwa huru, maendeleo yakaingia Malawi, wafanyabiashara kutoka Tanzania haswa mikoa ya Mbeya na Ruvuma wakaanza kuingia Malawi kufanya biashara bila buguza yoyote. Na wa Malawi wakaanza kuja Tanzania pia kufanya biashara zao.

Ule urafiki na udugu wetu uliokuwa umeanza kufifia baada ya Banda kupiga mkwara wa kuivamia Tanzania ukaanza kurudi tena. Hela mitaani ikaanza kuonekana, unea onea ya polisi na jeshi kwa raia ikakoma. Mahakama zikawa huru, bunge huru na wananchi huru.

Kamuzu Banda akapata presha akifikiri labda atafungwa na Muluzi kutokana na unyama aliofanya kwa nchi yake. Lakini wala haikuwa hivyo. Muluzi ali focus katika kujenga, kuiimarisha na kuiletea maendeleo nchi yake. Banda ile hali ilimtesa sana maana hakuwa tena na mtu wa kumpigia propaganda za kuwafubaza wamalawi kama alivyokuwa madarakani. Mabaya yake yote yalijulikana. Vyombo vya habari havikuogopa tena kuandika ushenzi aliokuwa anaufanya.

Matokeo yake mzee wa watu akajifia na stress za kuzomewa na kutupiwa vidale vya lawama kila alipokwenda, togauti na wapigania uhuru wenzake ambao waliheshimiwa na kuthaminiwa.

Bakili Muluzi aliiongoza Malawi kwa miaka 10, kutoka 1994 hadi 2004 akaacha nchi ikiwa yenye mifumo mizuri ya kiuongozi kuanzia mahakama, bunge, na serikali.

Alipotoka akaingia kijana wake Bingu Mutharika ambae, yeye muda mfupi tu wa uongozi wake akagombana na mtangulizi wake (Muluzi) na kuanza kuirudisha nchi kimya kimya katika utawala ule ule wa Kamuzu Banda.

Yeye Mutharika alienda mbali kwa kutoka katika chama cha aliemuachia madaraka (Muluzi) ambae alimpigia debe ili awe raisi baadae yake. Mutharika alianza udikteta uchwara kwa kuanzisha chama chake akiwa madarakani (katiba yao inaruhusu) na kuanzisha chama chake.

Hakuishia hapo, bali alimtupa ndani hata aliekuwa boss wake wa chama, na raisi wake, ambae pia alimchagua kugombea nafasi yake ya uraisi (Muluzi). Baada ya kumtupa Muluzi ndani akaendesha nchi hiyo kwa mkono wa chuma kimya kimya, na kuhakikisha kila mtu anamuogopa, hadi alipopatwa na umauti wa ghafla mwaka 2012, wakati akikibizwa Afrika kusini kwa ajili ya matibabu kutokana na ugonjwa wa mshituko wa moyo.View attachment 3334637
Safi kabisa Mdudukuzi,Banda akijiita president wa muyaya(Raisi wa maisha)
 
Asante mkuu Kimwakaleli, Banda alijiona kuwa yeye ndio alfa na umega wa Malawi. Ndiomaana alipong'olewa hakuishi tena kwa amani, mpaka alipofariki.
 
Back
Top Bottom