BAKITA acheni upotoshaji, Decoder ni King’amuzi, Transmitter ni Kisimbuzi

BAKITA acheni upotoshaji, Decoder ni King’amuzi, Transmitter ni Kisimbuzi

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2013
Posts
38,920
Reaction score
44,970
Nimeshangaa kusikia eti wanaojiita wataalam wa Kiswahili wakisema kwamba Tafsiri ya neno ‘Decoder’ ni ‘Kisimbuzi’, huo ni uongo wa wazi kabisa.

‘King’amuzi’ ni neno lililonyumbuliwa kutoka kwenye neno ‘ng’amua’ , kung’amua maana yake ni ‘Ku-decode’ , na hivyo kitu kinachofanya hiyo kazi ya ‘Ku-decode’ ndio kinaitwa ‘Decoder’, kwa kiswahili ni ‘King’amuzi’.

‘Kisimbuzi’ ni neno lililonyumbulishwa kimtambuka zaidi kutoka kwenye neno ‘Sambaza’ , kusambaza maana yake ni ‘Ku-transmit’ (au spread , mfano Ku-spread radiowaves) , na hivyo kitu kinachofanya kazi ya ‘Ku-transmit’ ndio kinaitwa ‘ Transmitter’ , Kwa kiswahili ni ‘Kisambazaji’ au kwa neno lililotoholewa ili matamshi yawe mazuri ndio tunaita ‘Kisimbuzi’ badala ya ‘Kisambazaji’.

Huko BAKITA wamejaa vilaza sana
AE946500-67C5-4652-BB44-D80D976F81BD.jpeg

Hii ni Transmitter (Kisambazaji / Kisimbuzi) kinachosambaza mawimbi ya Radio)

3C3226B4-2383-4306-ADA9-D80B385B8551.jpeg

Hiki ndio king’amuzi kinachofanya kazi ya kung’amua (decode) mawimbi yaliyotumwa na Kisimbuzi na kisha kupokelewa na dish ili kupeleka taarifa sahihi za video na sauti kwenda kwenye screen na spika za TV.
 
Nimeshangaa kusikia eti wanaojiita wataalam wa Kiswahili wakisema kwamba Tafsiri ya neno ‘Decoder’ ni ‘Kisimbuzi’, huo ni uongo wa wazi kabisa.



Huko BAKITA wamejaa vikaza sana
Wewe ndiye yule unayehojiwa na Phillip wa Clouds?

Kuanzia leo nimekuteua kuwa Mkuu wa BAKITA. Kawasafishe hao Vilaza.
 
Hawa hawachelewagi kujaribu neno ambalo limekwisha ingia kwenye matumizi na kuzoeleka. Mfano neno WASHIKA DAU likwisha zoeleka kwenye matumizi ndio wanaibuka na WADAU.

Neno Live kwa matangazo ya Moja kwa Moja lilikwishazoeleka wanakuja na la kiarabu MUBASHARA tena refu kuliko Lile la kiingereza hadi linafunika graphics
 
Uandishi wako ni mzuri sana.Umeandika kiswahili safi kabisa,na mpangilio wa maneno.Wewe lazima utakuwa ni msomi wa kiwango cha juu kabisa.Nimesoma uzi huu,nimejifunza mengi sana.
 
Alichosema ndio hicho kwa niaba ya Baraza, kwamba Decoder ni Kisimbuzi
C&P
Tunapohama kutoka analojia kwenda digiti neno 'king'amuzi' limeshamiri sana. Ndipo majuzi kupitia Radio One kwenye kipindi cha lugha ya kiswahili Jumamosi waendesha kipindi wakawa wanajadili haya.

King'amuzi ni detector. Mfano vile vibao vinavyotumika kupapasia sehemu za vizuizi na kwenye maofisi ni ving'amuzi. Vinang'amua uwepo wa kitu kisicho cha kawaida na ndio maana vinatoa mlio.

Decoder (codec)-code-decode ni kutafsiri toka mfumo mmoja kwenda mwingine mfano mawimbi ya analojia kwenda digiti. Na kiswahili chake kutokana na wataalam ni kisimbuzi. Linatokana na neno 'simba'-ficha. Halafu 'simbua'. Hivyo kifaa cha kusimbua kuitwa kisimbuzi.

Tusibanange lugha yaeu adhimu kwa hisia binafsi..., tuiache BAKITA waliokabidhiwa jukumu hilo lituongoze kwa kuzingatia mawazo ya wengi.
 
Back
Top Bottom