Nimeshangaa kusikia eti wanaojiita wataalam wa Kiswahili wakisema kwamba Tafsiri ya neno ‘Decoder’ ni ‘Kisimbuzi’, huo ni uongo wa wazi kabisa.
‘King’amuzi’ ni neno lililonyumbuliwa kutoka kwenye neno ‘ng’amua’ , kung’amua maana yake ni ‘Ku-decode’ , na hivyo kitu kinachofanya hiyo kazi ya ‘Ku-decode’ ndio kinaitwa ‘Decoder’, kwa kiswahili ni ‘King’amuzi’.
‘Kisimbuzi’ ni neno lililonyumbulishwa kimtambuka zaidi kutoka kwenye neno ‘Sambaza’ , kusambaza maana yake ni ‘Ku-transmit’ (au spread , mfano Ku-spread radiowaves) , na hivyo kitu kinachofanya kazi ya ‘Ku-transmit’ ndio kinaitwa ‘ Transmitter’ , Kwa kiswahili ni ‘Kisambazaji’ au kwa neno lililotoholewa ili matamshi yawe mazuri ndio tunaita ‘Kisimbuzi’ badala ya ‘Kisambazaji’.
Huko BAKITA wamejaa vilaza sana
View attachment 2559159
Hii ni Transmitter (Kisambazaji / Kisimbuzi) kinachosambaza mawimbi ya Radio)
View attachment 2559161
Hiki ndio king’amuzi kinachofanya kazi ya kung’amua (decode) mawimbi yaliyotumwa na Kisimbuzi na kisha kupokelewa na dish ili kupeleka taarifa sahihi za video na sauti kwenda kwenye screen na spika za TV.