Moderator Kero hii nimeiweka jukwaa hili ili kila mtu aione.
Nimekua nikisumbuliwa sana na hili jina Albino wakati tangu nazaliwa karibia nusu karne sasa, Neno sahihi la kiswahili ni Zeruzeru. Sijaona ubaya wa neno hilo jamani. Albino sio neno la kiswahili, ni neno la kingereza.
Swali langu, ni kwanini BAKITA = BARAZA LA KISWAHILI TANZANIA, Wamekaa kimya tu kwa upotoshaji huu mkubwa sana.
Kumbe wengi huwa mnakereka kama mie, eti wanaita mlemavu wa ngozi, sasa sijui nikiwa nina tatizo la ngozi la kuzaliwa nalo inakuaje. Wanaharakati ndio wanaharibu mambo yote kwa kuwa lile ndio jina sahihi kabisa kama linavyotamkwa kwa kithungu Albino na kiswahili ni zeruzeru. Kikubwa kama binadamu tunatakiwa tumtambue kwa jina lake ila tunapowaelezea kama kundi maalumu kutokana na tatizo lao inabidi tuseme zeruzeru au kiwete (kinachofanyika ni kusema tafsiri ya maneno yale yale ambayo wanayakwepa na ndio maana Nyerere aliwahi kusema ukitukanwa kwa kiswahili unakasirika lakini tusi lilelile likitolewa kwa lugha ya wenzetu huonyeshi kukasirika japo umelielewa)
HAya bwana mambo yataenda hivi;
- watoto-watu wenye umri pungufu
- wazee-wenye umri uliopea
- watu wazima-umri wa kati
- vilema-majeruhi wa kudumu
- wanawake-wazalisha "watoto"
- Wanaume -wasababishi "watoto"
- na upuuzi mwingineo.!
Kama neno kiwete nalo siku hiz linazunguushwa mpaka basi dah bakita wanzingua hawana msimamo
Jana nimesikia itv viziwi wanawaita walemavu wa masikio