BAKITA, Kwanini wasiitwe Zeruzeru?

Kuna neno Mwanaharamu. Kuna siku lilileta mtafaruku Redio one. BAKITA wakisistiza ndio neno sahihi kwa aliezaliwa nje ya ndoa, Mtangazaji wa redio one akilipotezea na kudai linadhalilisha baadhi ya watu.

Hivi vyombo vya habari vina unafiki mkubwa sana na ndio vinatupoteza. Wanafata tu matakwa ya bosi zao mara nyingi.

Mwaka 2001 nilihudhuria hafla ya walemavu iliyoandaliwa na Mengi huko Tanga Mkonge hotel. Alisisitiza sana kutotumia neno 'mlemavu' pekee na kushauri 'mtu mwenye ulemavu'...... ukitafakari, haina mantiki. Vyombo vyake vikaanza kutamka hivyo na hadi leo limeshika kasi. Hata Albino ni yeye alishauri wasiitwe zeru zeru... UNAFIKI!

Kujaribu kutumia lugha za nje, sio tu tunadhalilisha walemavu bali pia na jamii nzima kwani tunaonekana malimbukeni.
 
Lakini inaenda mbali zaidi......
Asilimia kubwa ya jamii zetu Tz na Afrika kwa ujumla wanaona ufahari kutumia majina ya kizungu au kiarabu ama kutokana na dini au elimu walonayo..... yote hiyo ni ulimbukeni kudhani cha jirani ni bora wakati "Titi la mama latosha".....
 


Mkuu nimefarijika saana na Weledi wako katika jambo hili. Laiti kama Watanzania wote wangekua na Weledi kama huu, tusingekua watu Wakuburuzwa au Malembukeni.
 
MZIMU asante. Pia siku hizi wazazi wengi wanapenda kuitwa DADDY/MAMMY. Baba/mama haina tena ladha. Labda ni hizi shule za mchepuo wa kiingereza.

Hilo albino na hayo mengine ni kielelezo tu cha kama jamii/taifa tulipofikia katika kudharau vya kwetu. Kwa hakika haitunufaishi.
 
Last edited by a moderator:
Kuna wakati niliambiwa huko mkoa kwamba watu wenye ulemavu wa miguu tuliozea kuwaita vilema nao hawalitaki hilo jina wanataka waitwe majeruhi wa vita.

I see! nimecheka sana! Majeraha wa vita! So, ni MASHUJAA!
 

kumwita MTU kama hapo pekundu ni kumfananisha na kitu..(ki) kijiko,kisu, kiti, kikombe nk...iwe hivi kipofu=ASIYEONA, kiziwi=ASIYE SIKIA, bubu=ASIYE SEMA mtiririko uwe hivyo....
 
kumwita MTU kama hapo pekundu ni kumfananisha na kitu..(ki) kijiko,kisu, kiti, kikombe nk...iwe hivi kipofu=ASIYEONA, kiziwi=ASIYE SIKIA, bubu=ASIYE SEMA mtiririko uwe hivyo....

Hayo ndioa maneno sahihi ya kiswahili. Sasa hiyo tafsiri yako unaitoa wapi?
 
Mzimu, hapo yanakuja maswala ya language attitude Zeruzeru ni neno la kiswahili tena fasaha (nakubaliana na wewe) ila kimtazamo lipo hasi kwa kiasi furani ukilinganisha na neno Albino (ingawa la kiingereza) lipo neutral, hata upande wa neno kiwete lipo hasi ukilinganisha na mremavu wa miguu, Kwa mtazamo wangu naona neno Albino tulikope na kulitumia kama neno la kiswahili, kwenye lugha inakubarika tu. (borrowing)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…