Fundisi Muhapa
JF-Expert Member
- Nov 25, 2013
- 4,422
- 2,112
Kuna neno Mwanaharamu. Kuna siku lilileta mtafaruku Redio one. BAKITA wakisistiza ndio neno sahihi kwa aliezaliwa nje ya ndoa, Mtangazaji wa redio one akilipotezea na kudai linadhalilisha baadhi ya watu.
Hivi vyombo vya habari vina unafiki mkubwa sana na ndio vinatupoteza. Wanafata tu matakwa ya bosi zao mara nyingi.
Mwaka 2001 nilihudhuria hafla ya walemavu iliyoandaliwa na Mengi huko Tanga Mkonge hotel. Alisisitiza sana kutotumia neno 'mlemavu' pekee na kushauri 'mtu mwenye ulemavu'...... ukitafakari, haina mantiki. Vyombo vyake vikaanza kutamka hivyo na hadi leo limeshika kasi. Hata Albino ni yeye alishauri wasiitwe zeru zeru... UNAFIKI!
Kujaribu kutumia lugha za nje, sio tu tunadhalilisha walemavu bali pia na jamii nzima kwani tunaonekana malimbukeni.