BAKWATA: Hatuutambui waraka wa Waislamu

Mbalamwezi

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2007
Posts
800
Reaction score
172
Bakwata imetangaza leo kuwa haiutambui waraka uliotolewa na Shura ya Maimamu jana.

Imesema hakuna mantiki kwa waislamu kuupinga waraka uliotolewa na Wakristo, halafu waislamu hao hao nao waamue kutoa wao. Watakuwa wametenda jema lipi kama waliona wakristo wamekosea?
 

Hata ule wa wakatoliki haukuwa wa Wakristo wote! Ngoma droo!
 







Sijasoma Nyaraka hizo, lakini hizi hotuba za uzinduzi wa nyaraka hizo mbili zinaonyesha tofauti kubwa sana katika maudhui yao. Ingawa zote zimetolewa na viongozi wa dini kwa waumini wao, moja ina utaifa zaidi na nyingine ina udini zaidi.


Katika hotuba yake, Sheikh Ramadhan Sanze amedai kuwa mwaka 1992 serikali ilikubaliana na makanisa kuwa itawapendelea wakristo nchini. Hili ni jambo la ajabu sana na nadhani linaweza kusababisha msuguano usiokuwa wa lazima na serikali kwa maana tamko hilo linaweza kuchukuliwa kuwa lina lengo la kuleta uchochezi bila msingi wowote. Akumbuke kuwa mwaka huyo 1992 wakati wa serikali ya Mwinyi ndipo kulikuwa na matukio mengi ya kidini kama vile uvunjaji wa bucha za nguruwe. Sidhani kama ni kweli kuwa Rais Mwinyi wakati ule aligeuka na kuahidi kuwapendelea eti wakristo kwa gharama ya kuwadidimiza waislamu.

Naweza kuelewa kwa nini BAKWATA haitaki kuutambua waraka huo.
 

Bakwata ni CCM, wanataka watu wakae kimya ili ufisadi wao uendelee.
 

Usitegemee lolote la kimaendeleo la waislam litaletwa na Bakwata...Bakwata ni Taasis ya CCM/Serikali...Viongozi wake wanachaguliwa na Usalama wa Taifa/Viongozi wa Serikali...
Hawajafanya lolote tangu 1967 ilipoundwa...Walivyonavyo sasa ...Serikali ya Nyerere ilipora kutoka Taasis Rasmi ya waislam na kuwapa Bakwata....!!! Vingine wameuza....Walivyonavyo vimedumazwa...!!!

Kichuguu...Endelea kutaja mengine yaliyotokea wakati huo...!!!
 
Vilevile tukumbuke hawa Shura ya Maimamu ni taasisi ndogo ya kidini (NGO) na wanachama wake ni wanaharakati wachache lakini wenye uwezo wa kufanya kampeni ya nguvu.

Jambo la kufuatilia ni kujua ufadhili wao unatoka wapi? Source of their funding!
 
Hata ule wa wakatoliki haukuwa wa Wakristo wote!...
Unatakiwa utambue mantiki ya hii post, ni kwamba hakuna jumuiya yoyote ya Kikatoliki iliyoupinga ule wa Kikatoliki, ila hapa Jumuiya mojawapo ya Kiislamu ie Bakwata, imeupinga waraka wa Jumuiya nyingine ya Kiislamu. Nadhani utakuwa umegundua kwa nini mleta mada ameamua kuiweka humu !
 
Haya yote yanatokea kwa sababu Serikali iko njia panda.

Sasa ni wakati wa serikali kuamka!!!!
 
Vilevile tukumbuke hawa Shura ya Maimamu ni taasisi ndogo ya kidini (NGO) na wanachama wake ni wanaharakati wachache lakini wenye uwezo wa kufanya kampeni ya nguvu.

Jambo la kufuatilia ni kujua ufadhili wao unatoka wapi? Source of their funding!
Kakalende mi nakuunga mkono.. TAFADHALI WANAJAMVI MWENYE INFORMATION KUHUSU HII TAASISI NA UFADHILI WAKE AWEKE JAMVINI.tunaweza kuwa tunapambana na mapapa hatujui.Anyway kama miongozo ni kwa ajili ya uchaguzi mkuu..meaning kuchagua viongozi waadilifu, ni vipi hawa wenzetu waislamu wawe kama wanajazba na hasira kwa wakristo huku wakijifanya eti ni muongozo..kwa mfano sheikh ponda anasema'Akizindua Muongozo huo, Sheikh Ponda alisema wamefikia hatua hiyo kwa vile Waislamu ni jamii iliyodhulumiwa, ambayo inahitaji ukombozi na uhuru.
waislamu wamedhulumiwa na nani? wamedhulumiwa na wakristo au mafisadi ?, kwani ni wasiseme watanzania wamedhulumiwa?mbona walaka wa wakatoliki umejumuisha watanzania wote?
“Lakusikitisha Waislamu leo wanadai uhuru kutoka kwa ndugu zao weusi,” alisema Sheikh Ponda.

hawa ndugu weusi wanaoongelewa hapa ni akina nani?
Jamani nionavyo mimi waislamu wamekuwa wa kulaumu kwamba wanaonewa..
sasa si swala la mafisadi tena bali ni ugomvi wao kwa wakristo, kuna sehemu nimesoma katika quotation kwamba ..eti serikali imetia saini na wakristo kuwapendelea.. that is nosense!!
mimi ninachosema badala ya waislamu kukaa na kulalamika wanaonewa ni bora wakafikiria kuithamini zaidi ELIMU DUNIA na kuacha kuendekeza hiyo wanayoiita elimu akhera..tunahitaji maprofessa wengi wa kiislamu..ukweli ni kwamba bila elimu hakuna maendeleo na bila maendeleo siku zote level yako itakuwa ya chini, na utaona unaonewa.
tunahitaji wawekeze zaidi kwenye mahospitali, mashule, vyuo n.k na siyo vinginevyo.
 
Vilevile tukumbuke hawa Shura ya Maimamu ni taasisi ndogo ya kidini (NGO) na wanachama wake ni wanaharakati wachache lakini wenye uwezo wa kufanya kampeni ya nguvu.

Jambo la kufuatilia ni kujua ufadhili wao unatoka wapi? Source of their funding!

Shura haina the so called wafadhili...Ndio maana wameamua kuuza waraka kwa Sh.2000, kufidia gharama zao...otherwise wangetoa bure kama wakatoliki...!!!
 

Sinkala,

Tambua kuwa Ukatoliki sio Dini bali ni dhehebu katika ukristu.Elewa ndani ya ukristu kuna Walutheri, Waanglicana, wasabato, n.k n.k

Sasa je unataarifa kuwa KKKT na Anglican wanataka kutoa waraka zao kila mmoja?
 
Nimekuwa najiuliza siku zote huko Tanzania. Je Bakwata ina wafuasi wowote ukilinganisha na jumuiya nyingine za waislamu huko Tanzania especially Tanzania Bara.

Mimi naona kuna Jumuiya kama Baraza Kuu, Shura ya maimamu .n.k Hizi zina misimamo ya kidini sana katika kutetea haki za waislamu na uislamu.

Kwanini Serikali ya TZ inaikumbatia Bakwata? Kuna agenda gani kwa serikali?
 

Hili linajulikana kuwa Tanzania Udini hi suala linalohusu Uislamu. Mbona tumshasoma Thread nyingi hapa pale anapochaguliwa Muislamu kwenye Post nyeti. Au tunasahau kuwa kila siku tunaimba Uislamu CC ya CCM. Huu ni double standard iwapo Waislamu wanatowa madai yao basi na tuangalie na kuona kuna ukweli kiasi gani au nini chanzo cha hali hiyo.
TANZANIA HII UDINI NI UISLAMU
 
Vilevile tukumbuke hawa Shura ya Maimamu ni taasisi ndogo ya kidini (NGO) na wanachama wake ni wanaharakati wachache lakini wenye uwezo wa kufanya kampeni ya nguvu.

Jambo la kufuatilia ni kujua ufadhili wao unatoka wapi? Source of their funding!

Tukishajuwa iweje? Kwani kipi walichofanya kibaya? Nguvu ya hoja ndio inayoleta kukubalika na wala sio nani aliefadhili. BAKWATA wanafadhiliwa na Serikali lakini hawana hoja kwa Waislamu walichoweka mbele ni ngawira kutoka kwa JK.
 

NI rahisi kununuliwa kwani wote ni njaa tupu hakuna suala la dini pale!
 
hawa ndugu zetu inabidi wawe makini sana manake mtu akiwapinga wataanza hata kumuita kafiri!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…