Haya ndio matatizo ya jazba! Mimi lilidhani baada ya kuusoma waraka wa wenzao Wakatoliki hawa nao wangekuja na waraka ulioboreshwa zaidi ili kujenga kitu kimoja. Sasa waraka huu wa Shura ya Maimamu haujengi chochote. Unabomoa. Sasa ndio wakati wa watu kama Kingunge Ngombale Mwiru kuzungumza. Wanataka kutupeleka wapi hawa???
Si kweli kuwa tabaka mbili hizi zilizokuwa zikijengwa kimyakimya zina matatizo sawwsawa. Utakuwa ni unafiki kwa Waislamu kuorodhesha UFISADI tu kuwa ndio tatizo kwao. Ufisadi wameusema na matatizo mengine yanayowakabili wameyasema. Kwani suala la mahakama ya Kadhi halikuongelewi na wasio waislamu?
Matatizo waliyoyaona Waislamu kuwa kwao ni matatizo yeyote anaetaka umoja wa Taifa hana budi kuyasikiliza na kuyatafutia utatuzi sio kuyakebehi kwani kufanya hivyo kutaleta mgawanyiko sio utengamano.