PostGE2025 BAKWATA Tabora: Wahadhiri wa Kiislamu wasitoe tena matamko. Maelekezo yatahusu ofisi ya BAKWATA

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

McLaren

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2025
Posts
1,170
Reaction score
3,743
Baraza Kuu la Waislam Tanzania (BAKWATA) mkoa wa Tabora limepiga marufuku wahubiri na wahadhiri wa kiislamu kutoa matamko yanayoweza kuzua taharuki kufuatia vurugu zilizotokea wakati na baada ya uchaguzi wa Oktoba 29.

Akizungumza wakati wa sherehe za Watoto waliohitimu mafunzo ya Quran Mkoani Tabora Shekhe wa mkoa Ibrahimu Mavumbi amesema maelekezo ya dini yatatolewa tu kupitia ofisi ya BAKWATA.

"Kwa sasa hivi waumini na wahadhiri wa dini ya kiislaamu wasitoe maelekezo ya aina yoyote wala matamko ambayo yatapelekea taharuki kwa Umma wa kiislaamu na wakazi wa mkoa wa Tabora, kama kutakuwa na maelekezo ya Waislamu basi yatahusu ofisi ya BAKWATA" amesema Shekhe Mavumbi

Walipaswa kusema BAKWATA haihusiki na tamko la kukatana vichwa. Mwisho.

Shehe yule akisema mimi sio member wa BAKWATA BAKWATA wataaibika na marufuku uchwara yao.

Shehe Ponda, kwa mfano, hakubaliani na BAKWATA. Yeye yuko SHURA YA MAIMAMU.

Na hii ndio bifu ya Shehe Ponda maisha yake yote. Kwamba si lazima kila Muislam awe chawa wa BAKWATA, chini ya BAKWATA, na Chawa wa CCM.

Mbinu kuu mojawapo ya utawala wa CCM na serikali, ni kumwambia yeyote anaelalamika kwa lolote, kikundi chako ni nini, na kiongozi wenu ni nani.

Mama Ntilie wakisimama kupinga kodi ya supu ya Manispaa wanaambiwa mleteni Mwenyekiti Wapika Supu. Basi wanakuwa wanadili na mchemsha supu mmoja nchi nzima. Kazi kwisha. Wakishin 8thdwa kummudu Rais wa Wauza Supu wanamu-ULIMBOKA.

Gen Z wamesoma historia ya Dr Ulimboka , wameshashtukia chezo. Hakuna Mwenyekiti wa Gen Z wa kufanya nae maridhiano!!
 
Baraza Kuu la Waislam Tanzania (BAKWATA) mkoa wa Tabora limepiga marufuku wahubiri na wahadhiri wa kiislamu kutoa matamko yanayoweza kuzua taharuki kufuatia vurugu zilizotokea wakati na baada ya uchaguzi wa Oktoba 29.

Akizungumza wakati wa sherehe za Watoto waliohitimu mafunzo ya Quran Mkoani Tabora Shekhe wa mkoa Ibrahimu Mavumbi amesema maelekezo ya dini yatatolewa tu kupitia ofisi ya BAKWATA.

"Kwa sasa hivi waumini na wahadhiri wa dini ya kiislaamu wasitoe maelekezo ya aina yoyote wala matamko ambayo yatapelekea taharuki kwa Umma wa kiislaamu na wakazi wa mkoa wa Tabora, kama kutakuwa na maelekezo ya Waislamu basi yatahusu ofisi ya BAKWATA" amesema Shekhe Mavumbi

Naona kingwendu na chamia na chawa wameona miti yote inatereza hivyo wanajarabu kupoza mambo
 
Baraza Kuu la Waislam Tanzania (BAKWATA) mkoa wa Tabora limepiga marufuku wahubiri na wahadhiri wa kiislamu kutoa matamko yanayoweza kuzua taharuki kufuatia vurugu zilizotokea wakati na baada ya uchaguzi wa Oktoba 29.

Akizungumza wakati wa sherehe za Watoto waliohitimu mafunzo ya Quran Mkoani Tabora Shekhe wa mkoa Ibrahimu Mavumbi amesema maelekezo ya dini yatatolewa tu kupitia ofisi ya BAKWATA.

"Kwa sasa hivi waumini na wahadhiri wa dini ya kiislaamu wasitoe maelekezo ya aina yoyote wala matamko ambayo yatapelekea taharuki kwa Umma wa kiislaamu na wakazi wa mkoa wa Tabora, kama kutakuwa na maelekezo ya Waislamu basi yatahusu ofisi ya BAKWATA" amesema Shekhe Mavumbi

WATOE TU MATAMKO ILI UPUMBAVU WAO UZIDI KUJILIKANA MBELE HATA YA WAISLAMU WENZAO ...MAANA SISI TUKISEMA UKWELI TUNAONE KANA TUNA CHUKI NA HIYO DINI ILA SASA WAISLAMU WENYEWE WAMEANZA KUSHIHUDIA ..
 
Shida ya sisi waislamu ni BAKWATA.......inakuwaje wakatoliki, wasabato, KKKT, Waanglikana na wakristo wengine waunde taasisi zao wenyewe??
Lakini serikali ikaunda BAKWATA mwaka 1968 ili kiwe chombo cha waislamu.
Kifupi BAKWATA ni tawi la serikali ya CCM.
Zanzibar Mufti huteuliwa na Raisi na sio waislamu.
Huko huko Zanzibar viongozi wa kikristo huchaguliwa na wakristo wenyewe sio na Raisi.
Kuna shida kubwa kwetu!
 
Back
Top Bottom