Bakwata uislaam huo mmeutoa wapi? Kumbukeni moto ni mkali sana mtaenda chomwa

Bakwata uislaam huo mmeutoa wapi? Kumbukeni moto ni mkali sana mtaenda chomwa

AbuuMaryam

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2015
Posts
2,577
Reaction score
4,637
Nayaandika haya nikiwa na uchungu mkubwa rohoni mwangu. Nikiangalia wale walio pewa mamlaka ya usimamizi wa sheria ya Allah wanafanya mambo mazito ya kumuasi Allah na kudhulumu watu.

Kwanza nibainishe mimi sio mtu wa kuendeshwa na mihemko ya kiharakati... Sina chuki juu ya bakwata na nawaheshimu sana kwa sababu ndio chombo tegemewa cha kuwasemea waislaam nchini na kuisimamisha sheria ya allah. .. Lazima tukitii na tukiheshimu bila shaka. .. Na nakitii na kukiheshimu chombo hiki.

Bakwata mashaa allah, allah amejaalia kwa serikali hii kuruhusu waislaam kujihukumia mambo yao msingi ya kijamii yenyewe na mifumo ya kidola ikazitambua na kuzirasimisha sheria hizo(ndoa, talaka na mirathi). . . Na hukumu itakayotolewa na bakwata kwenye masuala hayo mahakama za nchi haziwezi ingilia.

Tumshukuru allah kwa hilo.. . Ni jambo mlilolipigania kwa muda mrefu kupata mahakama ya qadhi, ili waislaam tujihukumie mambo yetu wenyewe bila kuingiliwa kwenye ibada hizo.

Kumbe bhanaa wenzetu bakwata na baadhi viongozi wake waliliangalia kwa jicho la kimaslahi(la kiupigaji) . .. Mcheni allah nyie watu.. . Adhabu ya allah ni chungu. ..hamtookoka na viremba vyenu wala vyeti vyenu vya thanawy mlivyovipatia tanga.

Mathalani. .. Kwenye masuala ya ndoa. .. Siku zote ukiona suala hilo limefika kwa qadhi ujue mletaji ni mwanamke(mke).

Kwa sababu kisheria mwanaume hapati shida amepewa mamlaka, yakimkera anaacha tu(talaka).

Ila mwanamke hana uwezo wa kutoa talaka, suluhisho lake ni kwa qadhi.

Na kwa mfumo wenu wa uendeshaji qadhi mmemuweka kuanzia wilaya kisha mkoa kisha taifa.

Lakini wa kumpata huyo qadhi sasa ndio unaleta ukakasi.

Binti akiwa na tatizo kwenye ndoa yake na mumewe anabidi aanzie shauri lake bakwata kata ili lifike kwa qadhi wa wilaya.

Huko kata sasa eti binti maskini anatozwa kuanzia sh. 15,000/- ili tu shauri lake lifunguliwe na lisikilizwe.

Tujue kabisa ofisi ya bakwata kata haina mamlaka ya kusikiliza na kuiamua kesi ili watapoteza tu muda wako ila mwisho wa siku utapewa barua uende bakwata wilayani.

Ukifika bakwata wilaya kabla hawajakusikiliza lolote... Nenda kadeposit sh. 30,000/-.

Ila kumbuka mwenye mamlaka ya kusikiliza na kuamua ni qadhi na si bakwata(si sheikh wa wilaya wala katibu wake). . . Ila hela yako wanaitaka.

Kwahiyo mwisho wa siku lazima upelekwe kwa qadhi.

Sijajua na hadi kufika huko kwa qadhi nako inabidi utoe kiasi gani!

Kinachoniuma roho sio hela wanayoipiga.

Ila ni huyu mwanamke aliyepeleka kesi huko. .. Kumbuka kisheria ya kiislaam mwanamke anatakiwa akae nyumbani na watoto alee familia na amtii mumewe tu. .. Suala ya kufanya kazi limeruhusiwa kwa mwanamke ila inatiliwa nguvu zaidi asifanye kazi.

Anayemhudumia mwanamke ni mumewe.

Sasa fikiria mwanamke amegombana na mumewe anayemhudumia. .. Ikafikia hatua anahitaji msaada kutoka kwenu bakwata. .. Lakini ninyi mnamchaji over shs. 45,000/- ili apate huduma na msaada wenu ili apate haki yake.

Sasa hiyo hela anaitoa wapi mdhaifu huyu. ..? Badala ya kumsaidia kumpa haki yake mnamuongezea matatizo?

Uislaam wenu mmeutoa kwa sheitwaani gani?

Mbona hata hamumuogopi allah... Hivi hata mtume angekuwa anafanya huu upumbavu wenu. .. Huu uislaam usingefika hapa ulipo.

Mtume amesema "zichengueni haki za madhaifu wawili hawa, nao ni wanawake na mayatima".

Lakini ninyi mnashiriki kuwakandamiza.

Mcheni allah ndugu zangu.

Mtafanya waukimbie uislaam na waulalamikie uislaam kwa tamaa zenu za maisha ya dunia yasiyo chochote.

Mnatupeleka wapi nyie watu msiomuogopa Allah.

Mna tofauti gani na wapiga dili wa Richmond na wala rushwa.

Nyinyi mtachomwa kwa kudhulumu mali za watu kwa kuzila pasipo haki.

Kama mlitaka kipato mngekuwa na subra mkamsikiliza huyo dhaifu alafu mwisho mtwangeni hizo gharama mwanaume. .. Ila mwanamke mnamuonea anazipata wapi?

Akiwa hana maana yake akaendelee kumuasi allah kwa zinaa kwa mlolongo wenu kwa kudhulumu watu.

mwisho:
Nitoe tanbihi nyingine... Uislaam na sheria zake hazina shida kabisa wala hazina kasoro.

Na ukizifuata na zikasimamishwa vizuri kwa uadilifu utaupenda na kuufurahia uislaam. .. Uta enjoy na kujivunia kuwa muislaam.

Ila hawa wapiga dili hawa ndio wanaouchafua uislaam.

Nimuombe mufti.. . Baraza lako unalojitahidi kulisafisha na kulirudisha kwa umma... Kuna watu wa maslahi wanakuangusha.. . Wanalichafua baraza kwa tamaa zao za matumbo... Mijitu imejaza vitambi njaa zimewajaa hawana hofu ya allah... Adhabu ya allah yawangoja wasipotubu. .. Allah awaongoze.
 
Hizi nasaha zako zingekuwa ni nzuri laiti kama ungelizifikisha mahali husika na sio kuja kulaumu mtandaoni.

Kwa BAKWATA hizi ni nasaha zako kwao, na kwa sisi wengine utatufanya tuzidi kuwaona wapigaji tu, kama ulivyosema.

Au ulitaka tujifunze nini kwa haya uliyoyasema?
 
Hizi nasaha zako zingekuwa ni nzuri laiti kama ungelizifikisha mahali husika na sio kuja kulaumu mtandaoni.

Kwa BAKWATA hizi ni nasaha zako kwao, na kwa sisi wengine utatufanya tuzidi kuwaona wapigaji tu, kama ulivyosema.

Au ulitaka tujifunze nini kwa haya uliyoyasema?
Hivi mkuu ulitaka akalalamike wapi? je unawajuwa members wote waliopo humu ni akina nani?
 
Hizi nasaha zako zingekuwa ni nzuri laiti kama ungelizifikisha mahali husika na sio kuja kulaumu mtandaoni.

Kwa BAKWATA hizi ni nasaha zako kwao, na kwa sisi wengine utatufanya tuzidi kuwaona wapigaji tu, kama ulivyosema.

Au ulitaka tujifunze nini kwa haya uliyoyasema?
TUACHE dhulma. ..
 
Hizi nasaha zako zingekuwa ni nzuri laiti kama ungelizifikisha mahali husika na sio kuja kulaumu mtandaoni.

Kwa BAKWATA hizi ni nasaha zako kwao, na kwa sisi wengine utatufanya tuzidi kuwaona wapigaji tu, kama ulivyosema.

Au ulitaka tujifunze nini kwa haya uliyoyasema?
Wewe ni nani mpaka upange mada za kuandikwa humu na zisizotakiwa kuandikwa?
 
Hivi mkuu ulitaka akalalamike wapi? je unawajuwa members wote waliopo humu ni akina nani?
Wewe ndiye unaona hana sehemu nyingine ya kulalamikia ila hapa.

Je unauhakika kuwa hao wahusika wapo humu? na kama unauhakika kwa nini asiwa PM ili ujumbe uwafikie.

Nauliza tena kunafaida gani ya yeye kutuambia haya aliyosema, zaidi ya kutufanya kuzidi kuwaona wapigaji?

Hebu soma comments za wadau ujionee.
 
Una uhakika kuwa huo utaratibu wa kutoa fedha ndiyo utaratibu uliyowekwa na Bakwata?
 
Back
Top Bottom