Balaa la kuazimisha gari!!!

Aisee nimekumbuka miaka hiyo Tabora nyumba za jeshi zilikuwa zinaitwa majumba ishirini. Major mmoja alienda kozi ya mwaka mzima gari yake kaiacha pale pale kwake (Zile nyumba parking ipo ndani ya nyumba) Gari alimkabidhi jirani meja mwingine awe anaenda kuipasha tu. Siku hiyo kaenda kupasha gari akakuta mke Wa yule meja nae kasafiri wapo watoto tu wadogo akawaambia wafungue geti anaenda kutengeneza gari. Kumbe kaenda nalo Ipuli huko kulewa akapiga mzinga gari haitamaniki. Ilibidi waivute mpaka nyumbani na jamaa aligharamia kila kitu mpaka gari ikarudi barabarani. Sijui kwanini walevi wanagonga sana mizinga wakiwa na gari za watu ila wakiwa na gari zao wanakuwa makini sana.

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Dah nmerud home jion wife ananibia kalikwangua gari kidogo alipokuwa analitoa nje …….nlikaa nje kama lisaa hasira zipungue nsije mchenjia…..inauma sana wazeee[emoji28][emoji28] simuachii tena ndinga
Hivi mbona gari likikwanguliwa wamiliki huwa wanakasirika Kama mashetani yanawapanda Ni Nini Yani, mbona huwa wanafoka hivi.?
 
Hivi mbona gari likikwanguliwa wamiliki huwa wanakasirika Kama mashetani yanawapanda Ni Nini Yani, mbona huwa wanafoka hivi.?
Lako likikwanguliwa fundi rangi akakwambia inabidi mlango/upande mzima upigwe rangi upya na gharama yake ni afutatu utajisikiaje?
 
Unapokuwa na dharau na mali ya mtu tegemea kupata nayo ajali. Unatakiwa uheshimu mali ya mtu kama vile mwanaume anavyoheshimu Pumbu zake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…