IamMrLiverpool
JF-Expert Member
- Apr 27, 2014
- 4,362
- 6,274
Aisee nimekumbuka miaka hiyo Tabora nyumba za jeshi zilikuwa zinaitwa majumba ishirini. Major mmoja alienda kozi ya mwaka mzima gari yake kaiacha pale pale kwake (Zile nyumba parking ipo ndani ya nyumba) Gari alimkabidhi jirani meja mwingine awe anaenda kuipasha tu. Siku hiyo kaenda kupasha gari akakuta mke Wa yule meja nae kasafiri wapo watoto tu wadogo akawaambia wafungue geti anaenda kutengeneza gari. Kumbe kaenda nalo Ipuli huko kulewa akapiga mzinga gari haitamaniki. Ilibidi waivute mpaka nyumbani na jamaa aligharamia kila kitu mpaka gari ikarudi barabarani. Sijui kwanini walevi wanagonga sana mizinga wakiwa na gari za watu ila wakiwa na gari zao wanakuwa makini sana.
Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app