Balaa la zawadi

Balaa la zawadi

Roca fella

JF-Expert Member
Joined
May 13, 2023
Posts
2,077
Reaction score
4,152
Basi akanilaumu sana akatoa lawama za kutosha, ya kwamba kwanini nilimtendea vile, lakini haikuwa kosa ni moja wapo ya kutekeleza jambo husika.

Turudi nyuma kwenye stori za maisha yetu ya kila kukicha, hapo awali niliwahi kupanga chumba katika moja ya jiji nchini tanzania, katika hiyo nyumba lipata jirani mwema, lakini wema wake kwangu ulivuka mipaka.

Ile tabia ya kumzoea mtu kwa pupa, kumlazimisha akuletee zawadi, mara akuletee hiki na kile, huyu jirani alikuwa ni binti wa makamo kwa wakati ule ni miaka 22 - 29, tabia yake ilidumu kwa muda mrefu nami nikiwa nampa ahadi za uongo na chenga za hapa na pale.

Moja siku nikaamua kumletea huyu binti zawadi yake, kuepusha usumbufu usio na msingi, basi baada ya mishe mishe na harakati za kusaka dow, nikapitia kwa duka, nikamchukulia zawadi ya chupi kwa jozi kadhaa,

Nikaenda ghetto kupoa kiana, kufika nikamgongea mlango si unaelewa surprise tena.

Mlango ukafunguliwa na libaba kwa makamo miaka 55 - 65, nikampa ile zawadi huku nikimwelekeza mhusika wa ile zawadi, kesho yake binti ananijia kwa lawama kuwa nimemharibia mahusiano yake na yule libaba, alichunguza ile zawadi akaona chupi kwa jozi, alipaniki sana, ugomvi ukazuka, ameachwa na yule libaba ni sponsor wake, anamwezesha kwa mambo lukuki.

Nikamweleza, kwani si ulitaka zawadi, me nimekuletea zawadi kosa langu wapi lipo..? Sikuwa na nafasi ya kubishana na yule binti, nikaingia ghetto nikatengeneza msokoto nikawasha bangi ili nilipue kichwa. Kuna kesi zingine hutakiwi kutatua.

Wenye tabia za kuomba zawadi au wapinga mizinga hebu punguzeni speed mlionayo, itawa cost sana later.
 
Hizo italic zinakanganya,
Watu wataishi umeandika shairi
 
Itakuwa ulilipua bila kula,kilichokutuma upeleke mzigo wa chupi Kwa manzi wa makamo bila kumtaarifu ni Nini?Next time kula msosi wa maana Ndio uvute msuba,la sivyo kuna siku utavaa boksa kichwani.
 
Itakuwa ulilipua bila kula,kilichokutuma upeleke mzigo wa chupi Kwa manzi wa makamo bila kumtaarifu ni Nini?Next time kula msosi wa maana Ndio uvute msuba,la sivyo kuna siku utavaa boksa kichwani.
Sure sure bro... Lakini msuba Mimi nina umudu, na haini changanyi ubongo. 😄🤠
 
Back
Top Bottom