Balaa: Nisha amfanyia bethidei mume wa mtu

Balaa: Nisha amfanyia bethidei mume wa mtu

Gumzo

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2012
Posts
211
Reaction score
8


USIOMBE yakukute! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya kusikia kisa cha aliyewahi kuwa mpenzi wa mwanamuziki wa TAKEU, Nice Lucas Mkenda ‘Mr. Nice’, Lulu John (mwenye blauzi nyekundu) anayedai kumfumania mumewe (siyo Mr. Nice), Risasi Mchanganyiko linafunguka.
Lulu alidai kumfumania bwana’ke Abdulatif Salum na mwanamke ambaye jina halikupatika kwenye gesti moja iliyopo Kinondoni B jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki iliyopita.
SINEMA ILIKUWA HIVI
Kwa mujibu wa Lulu, akiwa kwenye mihangahiko ya kusaka bingo, alitonywa na mtu wake wa karibu kuwa mumewe Abdulatif yupo kwenye nyumba hiyo ya wageni akiigagadua amri ya sita nje ya mkataba.
Lulu, baada ya kuthibitishiwa kuwa mumewe anacheza ‘nje kapu’ ndipo akakodi bodaboda fasta na kuwahi eneo la tukio kwani naye siyo mgeni wa uwanja huo wa mechi za kitandani.
Alidai kuwa ilimchukua dakika 12 tu kutoka Kijitonyama, Dar anakoishi na mumewe hadi eneo la tukio.
MPAKA CHUMBANI
Aliendelea kusema kuwa baada ya kutimba mahali hapo alikwenda moja kwa zote hadi kwenye chumba walichojichimbia wawili hao na kuanza kubamiza mlango huku akipiga mayowe ya kuomba msaada.
WENGINE WADHANI WAMEFUMANIWA
Huku akizidisha kupiga kelele akitaka kuvunja mlango, ndipo akakatiza stimu za watu wengine waliokuwa wakilimega tunda tamtam kwenye vyumba vingine ambao walitoka kwa kihoro wakidhani wamefumaniwa wao.
MUME ATIMKA NA NGUO YA NDANI
Aliendelea kusimulia mkasa kuwa watu walianza kujaa nje ya chumba hicho ndipo Abdulatif akafungua mlango kwa kasi na kutimka kama mkizi akiwa na nguo ya ndani pekee kisha akaruka fensi.
WATU WEWEEE!
Alisema kuwa wakati anachomoka nduki alimgonga kikumbo Lulu na kumwangusha chini huku akimwacha akigaragara ambapo watu walikuwa wakimkimbiza wakisema: “Weweee.”
VITA
Baada ya kunyanyuka na Abdulatif kumchomoka hivihivi ndipo vita kuu ikaanza dhidi ya mgoni wake.

KWA HABARI KAMILI BOFYA HAPA GUMZO LA JIJI: BALAA: NISHA AMFANYIA BETHIDEI MUME WA MTU
 
SALMA Jabu ‘Nisha’, aliye msanii wa filamu Bongo, ameendelea kujinadi kutoka na jamaa anayedaiwa ni mume wa mtu aitwaye Geofrey Kusila ambapo safari hii amemuandalia bonge la ‘bethidei’, Risasi Mchanganyiko limechungulia.
Tukio hilo ambalo Nisha ameonekana kulifanya bila hofu wala kificho lilidakwa na paparazi wetu Jumapili iliyopita katika Baa ya Uhuru Peak, Mwananyamala jijini Dar ambapo wasanii kibao walihudhuria.
Awali, chanzo kilichokuwepo eneo la tukio kilimuendea hewani paparazi wetu na kumtonya kuwa Nisha amemfanyia ‘surprise’ jamaa huyo kwa kumuandalia pati ya kimyakimya ndipo akatinga eneo hilo na kujionea kila kitu.
ENEO LA TUKIO
Paparazi wetu alifika eneo la tukio na kushuhudia shamrashamra za kulishana keki zikiendelea kabla hajawapiga picha za kumwaga lakini baadaye mtiti ukaibuka na kuamriwa azifute.
“Jamani hebu acha kupiga picha na unatakiwa kufuta zote ulizopiga. Yaani nyie hampitwi! Kwanza nani amekualika hapa?” alihoji Nisha kwa hasira.
Hata hivyo, mwandishi wetu alifanikiwa kuwachomoka bila kufuta picha hizo.
Aidha, juzi Jumatatu gazeti hili liliwasiliana na Nisha kwa njia ya simu na kumwuliza juu ya sakala hilo, akasema: “Ni mchumba’ngu na amenivisha pete, kama angekuwa mume wa mtu angeweza kukaa nyumbani kwangu kwa muda wote huo? Ninachojua ni mpenzi wangu basi, sitaki maswali zaidi lakini nakusisitiza ufute zile picha.”

KWA HABARI KAMILI BOFYA HAPA GUMZO LA JIJI: KIZAAZAA: CHUZ ASAKWA KWA KUTAPELI SH MILIONI 5
 
Back
Top Bottom