Balaa tupu! Diamond, Ally Kiba wakutana ukumbini, wachuniana!

GadoTz

JF-Expert Member
Joined
Nov 20, 2014
Posts
370
Reaction score
636


Baadhi ya wasanii wa Bongo fleva wakiwa kwenye mkutano.

Duh! Kama ulikuwa unaamini kuwa lile bifu la wakali wawili wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz' na Ali Saleh Kiba, limekwisha, basi umenoa baada ya jamaa hao kukutana ukumbini na kuchuniana.

Ishu hiyo ilijiri kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Double Tree Hilton jijini Dar, juzikati ambapo wasanii mbalimbali walikutanishwa na kampuni moja ya huduma ya simu za mkononi ili kuzungumza na wanahabari juu ya maandalizi ya tamasha.

Waandishi wetu, wakiwa wameingiwa na roho ya kutaka ‘ubuyu', hatimaye muda wa kuingia Kiba ukawadia ambapo alitinga na timu yake ya watu wanne.
Alipofika, Kiba alikaa sehemu ya viti vya kushoto akiwa bize na mrembo mmoja wakichati kabla ya Diamond kutimba na timu yake kubwa.

Kama ilivyo ada, macho ya waandishi wetu yakaelekezwa kwa Diamond huku mapichapicha yakiendelea kwa ajili ya kutupia kwenye mitandao ya kijamii.

Kila msanii aliyefika kwenye ukumbi huo alianza kutoa salamu kwa mtu anayeona anafaa kwake, lakini cha kushangaza mastaa wawili Kiba na Diamond walishindwa kupeana hata mikono huku kila mmoja akiwa ameuchuna na kampani yake.

Hata hivyo, wakati ulipofika wa wasanii kujitambulisha mbele ya wadau, mastaa hao walitahadharishwa kwamba atakayeanza au atakayekuwa wa mwisho kujitambulisha haina maana kwamba yeye ndiye mkubwa zaidi kistaa.

Katika kujitambusha, Kiba ndiye aliyeanza huku kila mtu akitamba kufanya vizuri kwenye kila shoo zitakazofanyika mwaka huu.
Hakuna aliyekuwa tayari kumzungumzia mwenzake.

 
Diamond na Ali Kiba wana albamu ngapi na wameuza ngapi?
 
wapuuzi wote wawili ndo nini sasa labda??
ujinga hafi mtu wote wapuuuzi...!!!!

Hawa ni wapuuzi wanatakiwa kukemewa hivi leo hii kama mmoja ikitokea hayupo aliyebaki atamlilia mwenzie? Mimi bado namlaumu Kiba maana yeye ni mtu mzima kuzidi Diamond ..kutosalimiana ni upuuzi ulio pitiliza.
 
Haya mabifu ya kipuuzi sana! mabeef tuwaachie wakina Suge knight, wakina 50 cent wakina TI siyo hawa wajiga wanagombeana wananaume
 
Hawa ni wapuuzi wanatakiwa kukemewa hivi leo hii kama mmoja ikitokea hayupo aliyebaki atamlilia mwenzie? Mimi bado namlaumu Kiba maana yeye ni mtu mzima kuzidi Diamond ..kutosalimiana ni upuuzi ulio pitiliza.

nashangaa sana mi nawalaumu hivi ukijishusha unapungukiwa nini ?!!au ndo wanamuogopa shigongo ataandikiwa"A kamshobokea B"
wapumbavu sana hawa
 
Hawa ni wapuuzi wanatakiwa kukemewa hivi leo hii kama mmoja ikitokea hayupo aliyebaki atamlilia mwenzie? Mimi bado namlaumu Kiba maana yeye ni mtu mzima kuzidi Diamond ..kutosalimiana ni upuuzi ulio pitiliza.

Akisha msalimia mumuandike kajipndekeza ?
 
Tired of this...lol kila siku kiba ,diamond khaaa! Are they "God fathers" in Tanzania?enough is enough ,kama ni issue ya celebrities wapo wengi tu hata BAMBO,kibakuli nao ni "celebrities" and they need airtime too.
 
pengine hili tamasha limeandaliwa kwa ajili ya kuingiza, pesa kupitia hii bifu ya kichina kitendo cha wao kusalimiana na kuonyesha hawana tofauti pengine waliona kutapunguza mvuto wa tamasha lenyewe nahisi hivyooo.
 
Huu ndio ujinga wa wasanii wetu.

Hawa kweli wana utoto ulio pitiliza.

Hawa ni wapuuzi wanatakiwa kukemewa hivi leo hii kama mmoja ikitokea hayupo aliyebaki atamlilia mwenzie? Mimi bado namlaumu Kiba maana yeye ni mtu mzima kuzidi Diamond ..kutosalimiana ni upuuzi ulio pitiliza.

Hahahaaaa yaani wewe jamaa bana.

Sasa ujinga na upuuzi uko wapi hapo?

Nini jipya na/ au la ajabu wanalolifanya wao ambalo halijawahi kufanywa na wasanii wengine na/ au ambalo halifanywi na hata watu wengine wasio wasanii?

Mambo ya mabifu kwa wasanii si mageni na yapo tokea enzi na enzi na si ya kipekee kwa wasanii wa Kitanzania tu. Hata huko kwingine mabifu ya kiushindani yapo tena mengi tu.

Ili mradi kila mmoja wao anabaki kwenye njia yake na amani inadumishwa sioni kwa nini uwaite wajinga au wapuuzi.

Bifu za kiusanii huongeza ushindani na ushindani unapoongezeka washabiki hupata bidhaa bora.

Hivyo hamna ujinga wala upuuzi hapo.

What's happening between the two of them comes and goes with the territory.
 

Bora useme we we, halafu watu wasisahau kuwa hawa jamaa wanatoka kigomaaa....huwa hawatupani wale watu...

So tuongee huku tunabakisha maneno, wakija patana tusije kuona aibuu...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…