Balaa tupu! Diamond, Ally Kiba wakutana ukumbini, wachuniana!

Balaa tupu! Diamond, Ally Kiba wakutana ukumbini, wachuniana!

Ila hata ningekuwa mimi Diamond nisingemsalimia Ali Kiba.
 
Diamond na Ali Kiba wana albamu ngapi na wameuza ngapi?

Bongo ukitegemea kuuza albamu kupata mkwanja utakufa njaa

Unatoa single iki hit tu unapata zako show za kutosha unavuta mapene
 
Kwa muda mrefu sana imekuwa ikinisumbua kuelewa hasa dhumuni la nchi hasa za kiafrika kudai uhuru wetu ikiwa matokeo ya uhuru huo umekuwa na matunda mabaya sana kwa raia wake kisiasa na kiuchumi.

Je, dhumuni hasa lilikuwa kumwondoa mtawala mlowezi na badala yake kumweka mzawa?

Je, ilikuwa mategemeo ya wengi kubadilisha mkono wa mtawala wa uchumi toka mlowezi na badala yake kushikwa na mzawa?

Je, uhuru ulitakiwa kwa sababu ya haki za kibinadamu baada ya matokeo mabaya ya vita kuu ya pili duniani?

Hadi leo ndugu zangu sifahamu kabisa maana ya UHURU ikiwa wananchi wengi wa nchi zilizotawaliwa wamekuwa na maisha mabaya zaidi chini ya utawala wa mzawa. Adui mkubwa wa maendeleo ya mwafrika imekuwa mwafrika mwenzake. Umaskini wa mwafrika unazidi kukua baada ya Uhuru huohuo kuzua matabaka baina yetu. Kuna hao wanaosema afadhali hata mkoloni kwani alitutawala na bado alihakikisha uchumi wetu upo jtk hali nzuri kuondokana na balaa la njaa. Kifupi tulitawaliwa lakini bado jukumu la kuhakikisha tunakula vizuri lilikuwa bado la mtawala! Mwananchi mwenye njaa ni sawa na gari lisilokuwa na mafuta... haliwezi kwenda popote!

Msinielewe vibaya kwamba napendekeza kutawaliwa zaidi ya kujitawala! lakini nachoshindwa kuelewa ni maana ya kujitawala -uhuru! ikiwa kiongozi mzawa mwenyewe hana tofauti kwa mabaya na huyo mtawala mlowezi.

Umaskini afrika ni maradhi ya kujitakia na yawezekana kabisa kuwa UHURU wetu umetafsirika vibaya hivyo kupoteza malengo yake. Haya maswala ya utandawazi yatawezekana tu pale tutakapo weza kutambua sisi tumetoka wapi na malengo yetu ni kwenda wapi.!.. Nje ya hapo Uhuru kwa mwafrika ni mabadiliko ya sura ya mtawala. Mateso na dhulma zipo palepale isipokuwa tu anayekunyonya ni chawa sio kunguni!

Kwa mtazamo wangu naomba sana mchango wenu wanabodi kwa upeo wenye matumaini... upeo ambao unatutakia mabadiliko ndani ya vyombo vyetu vya siasa na uchumi ili kuboresha maisha ya wananchi.

Haki na amani isimame kama ilivyokusudiwa tulipokuwa tukigombea uhuru wetu...

Haki na amani iwe juu yetu sote!

Basi wote waganga njaa tu.
 
By danford
Baadhi ya wasanii wa Bongo fleva wakiwa kwenye mkutano.

Duh! Kama ulikuwa unaamini kuwa lile bifu la wakali wawili wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ?Diamond Platnumz? na Ali Saleh Kiba, limekwisha, basi umenoa baada ya jamaa hao kukutana ukumbini na kuchuniana.

Ishu hiyo ilijiri kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Double Tree Hilton jijini Dar, juzikati ambapo wasanii mbalimbali walikutanishwa na kampuni moja ya huduma ya simu za mkononi ili kuzungumza na wanahabari juu ya maandalizi ya tamasha.

Waandishi wetu, wakiwa wameingiwa na roho ya kutaka ?ubuyu?, hatimaye muda wa kuingia Kiba ukawadia ambapo alitinga na timu yake ya watu wanne.
Alipofika, Kiba alikaa sehemu ya viti vya kushoto akiwa bize na mrembo mmoja wakichati kabla ya Diamond kutimba na timu yake kubwa.

Kama ilivyo ada, macho ya waandishi wetu yakaelekezwa kwa Diamond huku mapichapicha yakiendelea kwa ajili ya kutupia kwenye mitandao ya kijamii.

Kila msanii aliyefika kwenye ukumbi huo alianza kutoa salamu kwa mtu anayeona anafaa kwake, lakini cha kushangaza mastaa wawili Kiba na Diamond walishindwa kupeana hata mikono huku kila mmoja akiwa ameuchuna na kampani yake.

Hata hivyo, wakati ulipofika wa wasanii kujitambulisha mbele ya wadau, mastaa hao walitahadharishwa kwamba atakayeanza au atakayekuwa wa mwisho kujitambulisha haina maana kwamba yeye ndiye mkubwa zaidi kistaa.

Katika kujitambusha, Kiba ndiye aliyeanza huku kila mtu akitamba kufanya vizuri kwenye kila shoo zitakazofanyika mwaka huu.
Hakuna aliyekuwa tayari kumzungumzia mwenzake.
Ok by danford
 
Back
Top Bottom