Balali alishakufa hatukuambiwa?

Balali alishakufa hatukuambiwa?

Swali jingine kwani lazima kumuona mtu katika jeneza. Wewe unahusika vipi na ndugu zake? tuwe na tamaduni za watu kutafuta ukweli sio gossips, hazitusaidii kitu. gazeti la Majira lilienda ndani zaidi likaandika mahojiano na mdogo wake huko iringa kijijini kabisa na akaconfirm kuwa ndugu yake ni no more na yeye anasimamia maslahi yake hapa nchini.Ikumbukwe kwamba balali alikuwa na uraia wa Marekani na mkewe ni Mganda hapa nyumbani pamoja na kutoka iringa alikuwa TX. Mnataka kuchukua raia wa nchi nyingine kumzika ahh sawa yaani mtu tx alisema anataka kuzikwa hapa. Jambo jingine hivi mnajua kwamba huyu kabla ya kifo chake safari za afrika Kusini kwa matibabu zilikuwa nyingi. Mnasema tu. nani ashiriki kuficha kifo cha mtu kwa sababu gani hasa. Mliona maiti ya wako jacko?Kama mnakuwa na haja naye kwanini msitafakari maisha wakati mwingine unacheka madaktari wazima wanatengeneza conspiracy story ili wawini uanasiasa. kweli siasa si hasa!

Umejielezea vizuri but unasahau kitu kimoja hata picha basi za mazishi hakuna. Umetoa mfano kuwa wacko jacko kuwa amefariki hatukuona mtu but umesahau maiti yake kabla haijazikwa ilipigwa picha. Serikali ya Marekani kupitia California walifanya hivyo kuondoa conspiracy theory za washabiki wake. Anapofariki mtu hatuna haja ya kuona maiti bali tunataka kuwa na uhakika huyo bwana amefariki tu basi. Na pengine tuweke kumbukumbu za kifo chake.

Wewe mbona ukienda katika mazishi unachukua picha, video na kumbukumbu zenginezo? Iweje mtu mkubwa kama huyo azikwe kama mtu aliyezikwa na jiji tu pasina kuwa na ndugu wala watu wa kumzika? Unaweza kusema ni conspiracy au vyovyote ila tunataka evidence. Kuenda kumuuliza ndugu yake Iringa haina maana kwani kama umeangalia movie ya minority report wao wanaweza kuwa katika kiza kama sie. Witness protection program mara nyingi inainvolve watu wawili au watatu wanaojua what is going on. Wengine wote mnapumbazwa
 
Leo napitia nyuzi za zamani tu na kufukua makaburi.
JF ya zamani ilikuwa na GT kweli kweli labda kwakuwa enzi hizo vitisho vilikuwa sio vingi.
 
Kwa vile Balali alipelekwa kwenye matibabu huko Marekani, matibabu ambayo yalisababisha alazwe kwa muda mrefu;

Kwa vile hali yake haikuwa nzuri na iliendelea kuwa mbaya hadi kumlazimisha amuombe Rais amruhusu aachie ngazi

kwa vile Rais hakukubali Balali ajiuzulu na baadaye kumtimua kazi akiwa mahututi kitandani;

Kwa vile Rais aliamua kuunda kamati maalumu ya kuchunguza wizi wa EPA na mhusika mkuu wa sakata hilo alidaiwa kuwa ni mahututi;

Kwa vile kwa muda mrefu sasa viongozi wetu wamekuwa wakituambia kuwa hawajui aliko Balali jambo ambalo limerudiwa tena hapo jana na Waziri Mkuu

Kwa vile Balali alikuwa mgonjwa mahututi, hana kazi, na serikali haijui alipo

Hivyo basi, madai ya serikali kuwa wakimtaka watampata hayana ukweli; Kuwa serikali ikimhitaji mtu wasiyejua alipo wataweza kumpata kwa haraka, kimsingi madai hayo ya serikali na kauli hizo hazina msingi wowote.

Kwa sababu,

Balali alishafariki na kuzikwa huko huko majuu baada ya hali yake kuwa mbaya. Na kwa vile serikali haijui alipo hawana njia yoyote ya kujua liliko kaburi lake na hawana ujuzi wowote kuwa ni mzima au ni marehemu.

Hivyo, basi anayesubiri kumuona Balali akirudi Tanzania mzima anasubiri mvua jangwani!!

RIP Balali!!

NB: Kama ni mzima bado, serikali imejuaje wakati hawajui aliko?
Mzee enzi hizo ulikuwa mtu
 
Wakati huu uzi unaandikwa nilikua form 1[emoji23] [emoji23]
Shkamoo wahenga
 
sasa we ndo unajua kama kafa au umemuua ww ?? acha kuombea wenzako kifo
 
sasa we ndo unajua kama kafa au umemuua ww ?? acha kuombea wenzako kifo
 
Back
Top Bottom