Balile atamba niko tayari Kufa

Balile atamba niko tayari Kufa

Basi sasa Balile kaamua kutumia hiyo approach ya kuyakabidhi majina kwa serikali ili yachunguzwe kwanza ikijiridhisha yatawekwa hadharani. Vuta subira mwana wane.

Hayo majina hayatakaa yawekwe hadharani kaka. Iko wapi ripoti ya mtu aliyekamatwa akiwa kajiunganishia bomba la mafuta hapa mjini? Ingekuwa serikali ya watu waadilifu hapo sawa, sio hii.
 
MWENYEKITI wa Jukwaa la Wahariri, Deodatus Balile amesema yuko tayari kufa lakini hatoacha kuendesha mapambano ya kulinda Mto Ruaha dhidi ya wakulima na wafugaji walioko kwenye eneo hilo.

Balile anasema yuko tayari kufa baada ya kupokea vitisho vingi baada ya kutaja familia 12 zinazoharibu Mto Ruaha akizungumza na wanahabari leo Disemba 24, 2022

Balile anasema anatishiwa kuawa na hizo familia ikiwa anatambua kuwa hakutaja majina ya viongozi hao hadi sasa na hakuna mtanzania hata mmoja anayezijua familia hizo. Sasa aliyemtishia kumuua ni nani?

Ni nini kilichowafanya mpaka kushindwa kuyataja majina ya Mawaziri, Majaji na Wabunge wanaohusika na uharibifu huo.
Mpaka sasa hivi kwenye sakata hili ni mimi tu Mtoto wa Shule ambaye nimediriki kumtaja mmoja ambaye ni JOHN HECHE! Nikiwajua wengine nitawataja bila kuogopa. Na mlio na majina na mnaogopa kuwataja nipeni hayo majina INBOX niyataje hapa!

#Ukiniua umenipunguzia matatizo!!!
 
12 January 2021

WALIOKAIDI MKATABA WA NARCO KIKAANGONI NDANI YA SIKU KUMI


Na. Edward Kondela

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki ametoa siku kumi kwa Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) kubaini na kuwanyang’anya maeneo, wawekezaji waliopatiwa vitalu katika ranchi za taifa ambao wamebadili matumizi ya ardhi kinyume na makubaliano ya mikataba yao.

Waziri Ndaki amebainisha hayo jana (12.01.2021) wakati alipotembelea Ranchi ya Usangu iliyopo Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya alipokuwa kwenye ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani humo na kufanya mkutano wa hadhara na baadhi ya wawekezaji, wakulima na wafugaji, ambao wanafanya shughuli zao katika ranchi hiyo na kubaini kuwa baadhi ya wawekezaji waliopatiwa vitalu na NARCO kwa ajili ya kufuga na kulima malisho ya mifugo wamekuwa wakikodisha maeneo hayo kwa wakulima na wafugaji kinyume na mkataba.


“NARCO siku kumi nadhani zinawatosha kubaini watu wanaojiita wawekezaji, waliobadilisha matumizi ya ardhi ambayo siyo kufuga wala malisho wanyang’anywe maeneo kwa kuwa wameenda kinyume na utaratibu wa mkataba kati yao na NARCO, na mimi nitafuatilia nitapenda kupata taarifa mmepata wangapi na wangapi wamenyang’anywa kwa kuwa wameenda kinyume na utaratibu waliokubaliana.” Amesema Mhe. Ndaki



Waziri Ndaki amelazimika kutoa kauli hiyo baada ya kupata taarifa kutoka kwa baadhi ya wakulima na wafugaji wa Wilaya ya Mbarali kuwa wamekuwa wakikodishwa maeneo ya ranchi hiyo na wawekezaji kwa shilingi elfu ishirini kwa hekari moja kwa ajili ya kilimo na madebe kumi ya nafaka baada ya mavuno kwa kila hekari moja, huku wafugaji wakilipa takriban shilingi milioni mbili kwa hekari moja katika kipindi cha miezi minne kwa ajili ya kulisha mifugo yao kwenye maeneo ya wawekezaji ambao wamepatiwa vitalu na NARCO kwa mkataba wa kufuga au kulima malisho ya mifugo.

Amefafanua kuwa mkataba wa NARCO na wawekezaji kwa ajili ya kufugia mifugo na kulima malisho hauruhusu wawekezaji kukodisha eneo kwa mtu mwingine kwa ajili ya shughuli zozote kwa kuwa maeneo ya ranchi za taifa ni mali ya Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO).



Kuhusu deni la zaidi ya Shilingi Bilioni Sita ambalo NARCO inawadai wawekezaji waliopatiwa vitalu katika ranchi za taifa zilizopo kwenye maeneo mbalimbali nchini, Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki ameutaka uongozi wa NARCO kufikia Tarehe 15 Mwezi Februari Mwaka 2021 saa saba mchana awe amepata taarifa ya wawekezaji waliolipa madeni yao pamoja na ambao bado hawajalipa, kabla ya kuchukuliwa kwa hatua zaidi.



“Wawekezaji wote ambao tunawadai hapa Usangu na kwenye ranchi zingine wote walipe pesa ya NARCO tulipokubaliana kwenye mkataba tulikubaliana mtalipa pesa, mlipe madeni yenu ifikapo tarehe 15 mwezi februari saa saba mchana muwe mmelipa madeni yenu tunataka NARCO ijiendeshe kibiashara, lakini sioni tukielekea kwenye kujiendesha kibiashara na moja ya matatizo yanayotufanya tusifike huko ni kulea watu wa namna hii.” Amefafanua Mhe. Ndaki.

SOMA ZAIDI : HABARI MIFUGO NA UVUVI
 
MWENYEKITI wa Jukwaa la Wahariri, Deodatus Balile amesema yuko tayari kufa lakini hatoacha kuendesha mapambano ya kulinda Mto Ruaha dhidi ya wakulima na wafugaji walioko kwenye eneo hilo.

Balile anasema yuko tayari kufa baada ya kupokea vitisho vingi baada ya kutaja familia 12 zinazoharibu Mto Ruaha akizungumza na wanahabari leo Disemba 24, 2022

Balile anasema anatishiwa kuawa na hizo familia ikiwa anatambua kuwa hakutaja majina ya viongozi hao hadi sasa na hakuna mtanzania hata mmoja anayezijua familia hizo. Sasa aliyemtishia kumuua ni nani?

Ni nini kilichowafanya mpaka kushindwa kuyataja majina ya Mawaziri, Majaji na Wabunge wanaohusika na uharibifu huo.

Naye mnafiki tu.
 
Back
Top Bottom