Balile: DPP, IGP, DCI lifutieni taifa aibu kesi ya Mbowe

Nafasi za ajira jeshi la polisi;
Sifa za kujiunga:
Awe na division 4 ya point 29, mpaka 34.

Asante
Hoja za div 4 au PhD nihoja za kipumbafu kabisa kuongoza nimoyo Wa huruma na kutambua wajibu wako kila muda wakati wote chamuhim kabisa kuzingatia haq wenye ma PhD ndio waliotuingiza katika mikataba mibovu na wizi wakutisha unafanywa nawao katika Mali zauma tuache kuamini madaftari na vyeti tuangalie kusoma nakuandika kikubwa kabisa katika hili uadilifu ndio msaada kwa nchi sio phd
 
Miongoni mwa wachache wenye uwezo wa kutumia kalamu vxr je wanaufahamu?

Sent from my Nokia 3.2 using JamiiForums mobile app
 
Kama Mbowe ni gaidi, Gaidi ni gaidi tu, tutumie jina gani lingine? Nyoko nn, Balile aache uchadema wake kuandika kuhusu Mbowe. Balile ni Chadema inajulikana. Acha Mbowe afunzwe adabu.
 
Kuna watu wanajua kufikiri sawa sawa.Nadhani wakati umefikia katiba mpya wakatazama namna ya kuunda chombo kitakacho tazama utendaji wa Police.
... kabisa; kuna watu wako vizuri upstairs. Chombo huru cha ku-oversee utendaji wa polisi ni muhimu mno kwa sasa kuliko wakati mwingine wowote na mamlaka ya ukamataji mapolisi watakoonekana kukiuka sheria na taratibu wanaweza kukabidhiwa JWTZ, kitengo maalumu cha kudili na mapolisi. Kuwaacha polisi hao hao wajikamate wenyewe ni kulindana kama ilivyo sasa.
 
Umeongea ukweli, lakini kwa kuwa Rais Samia bado anashinikizwa na kundi moja ndani ya serikali yake au chama, hatafanya ila anaishi kwa kisasi. Ninyi Jamiiforums, tafadhali mkubali ukweli acheni kujipendekeza kufungia fungia watu wanaosema ukweli.
 
Sasa tuambie kwanini wanakimbilia madaraja ya mwisho ya ufaulu wakati ya kwanza yapo?tena wanaweka na sharti kabisa kwamba aanzie division 4 ilhali kuna vijana waliofaulu vizuri wapo mtaani lakini vigezo vya polisi haviwaruhusu?
 
Mzee mmoja amedai SSH haijui hii nchi! Nadhani madai hayo yanaweza kuwa na ukweli kiasi. SSH angekuwa anaifahamu vizuri hii nchi angejua kuwa jeshi la polisi siyo chombo cha kukiamini sana. Angekuwa anaifahamu nchi ikiwa ni pamoja na undani wa jeshi la polisi asingemeza jumla jumla taarifa kuwa ushahidi wa kutosha upo kuwa Mbowe ni gaidi! Matokeo ya SSH kutolifamu jeshi lake la polisi pamoja na vyombo vingine kesi ya ugaidi dhidi ya Mbowe sasa imeanza kugeukwa mwiba kwa nchi yetu. Kesi imeanza kuibua mambo mazito kuhusu jeshi la polisi ambayo lazima yaje kufanyiwa kazi bila kujali Mbowe amepatikana na hatia au la. Lakini pia inaelekea huu ni mpango wa Mungu kuwa pamoja na madhara yanayotokana na kesi hii yatokee mambo ya kunufaisha jamii yetu. Sote sasa tunajua kuwa udhaifu uliopo katika jeshi la polisi hauvumiliki!
 
... najaribu kuwaza tu; hivi ikija kugundulika hii kesi ni just fabrication na ushahidi ni wa kutunga then what next? Kuna hatua zozote zinazoweza kuchukuliwa, sio kwa washtakiwa kufungua kesi ya madai, bali mamlaka dhidi ya genge lote la polisi waliohusika kuanzia IGP? Kimsingi hii ni kashfa kubwa sana chombo ambacho kazi yake ya msingi ni kutenda HAKI kinafanya kinyume kabisa!

Kungekuwa na oversight body ya jeshi la polisi hii ndio ilikuwa miongoni mwa majukumu yake ya msingi baada ya kesi kumalizika; kuchunguza kama kulikuwa na ukiukwaji wa haki za washtakiwa wote waliohusika na ukiukwaji huo wawajibishwe. Nchi haiwezi kuendeshwa kihuni na genge fulani lililokabidhiwa madaraka kwa mujibu wa katiba na sheri za nchi wakaamua kizinajisi!
 
IGP anaju
IGP anajua mipaka yake kisheria. Anapoingilia vyama vya siasa siyo kwamba hajui balj anatekeleza maelekezo ya watawala. Awali ilidhaniwa vyama husika vitaogopa na kurudi nyuma. Hilo halijatokea; badala yake CHADEMA wamekomaa licha ya kukamatwa na kulala mahabusu. Jeshi la polisi wamejikuta wakimbizana nao kila kukicha. Wakati huo huo polisi hao wanatuhumiwa kuvunja katiba. Hali hii siyo endelevu; lazima ifikie mwisho. Hivyo kinachotafutwa sasa ni huo mwisho; uonekane kana kwamba mazungumzo yamefanyika na maelewano yamepatikana! Ndipo msajili anaingia!
 
Bwana Balile, asante kwa Mchango wako ambao umeutoa kwa kutoa mwanga wa muono wako kwa kesi hii ya ugaidi. Kwa muono wangu nakuona Umekua fundi wa uchambuzi populist ambao siku zote huficha ukweli na hautoi matokeo ya uchambuzi chanuo ambao ungetupatia utajiri wa muono na uhalisia wa tukio.

Umeshindwa kuanza uchambuzi wako kwa kutueleza Mbowe ni nani, ni nani kisiasa leo, ana nguvu gani au ushawishi wake katika siasa za leo. Tengeneza ushawishi katika uchambuzi wa kisiasa.

Jee umeona kuna fikra mpya zozote katika siasa za Mbowe na za upinzani? au bado ni muendelezo wa siasa za kupayuka tuu bila strategy for?.

Jee unaona kuna ufahari wowote kwa Mbowe kuwa mgeni wa bwana Jela? kuna matokeo ya kustua huko chini kwa wananchi kwa tukio hilo?

Ungeweza kutufahamisha kiwango cha arthari ambazo zilitegemewa.

Charity begins at home.
Injili ambayo anayo ailete huku Kilimanjaro kwani nasi tunaitaka sana. Na sisi kwa umoja wetu tuipeleke maeneo mbali mbali ya nchi yetu.
Kwa msio jua, mvuto wa Mbowe na Upinzani umepoteza sana ushawishi wake huku kwao Mbowe.

Balile kuna uwezekano mkubwa mna wakweza juu viongozi wetu sehemu ambayo hawapaswi kuwapo tena kwa siasa za leo.
 
hapa umelikoroga, does it mean that Mbowe is not patriotic? Not at all!
Unaweza ukawa mzalendo namba Moja.....ila malipo ya uzalendo wako yakawa ni mapigo (maumivu)

Binadamu tumeumbiwa Revenge (kisasi)
Binadamu wachache Sana mfano wa Nelson Mandela ndio pekee walituonesha kwa mifano na vitendo kua hatupaswi kuwafanyia Revenge watesi wetu......

Binadamu tunapishana level of understanding.... ndio maana naungana na jamaa alie sema wakae mezani na mbowe wamalize Hili jambo......

Viva Tanzania.....Viva wazalendo
 
Kwani gaidi anakuwa amevaa shanga usoni ilikujuwa kuwa ni gaidi? nyie vipi!!
uliwahi kusikia ugaidi unadhaminiwa kwa sh 600,000 dola 260? Ikiwa sabaya ni mwema alitaka agaidiwe na mbowe kwa nini mnataka kumfunga.

learn to think in three dimensions
 
👍👍
 
uliwahi kusikia ugaidi unadhaminiwa kwa sh 600,000 dola 260? Ikiwa sabaya ni mwema alitaka agaidiwe na mbowe kwa nini mnataka kumfunga.

learn to think in three dimensions
Kwani kesi zote si zipo mahakamani!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…