POTOSHI Balile: Dunia nzima Mwendokasi ipo Tanzania na Brazil tu

POTOSHI Balile: Dunia nzima Mwendokasi ipo Tanzania na Brazil tu

Uhalisia wa taarifa hii umepindishwa ili kupotosha
Source #1
View Source #1
Wakuu nimekutana na hii video ya Mwenyekiti wa jukwaa la wahariri Tanzania (TEF) akisema kuwa dunia nzima mwendokasi ipo Brazil na Tanzania tu. Hii imekaaje?

1759155733300.png
 
Tunachokijua
Barabara za magari yaendayo haraka (Mwendokasi) ni aina ya miundombinu inayotengenezwa kwa lengo la kurahisisha usafirirshaji wa abiria katika maeneo ya miji.

Madai

Septemba 29, 2025 wakati akizungumza na Clouds TV Mwenyekiti wa Jukwaa la wahahriri Tanzania (TEF), Deodatus Balile alieleza kuwa Tanzania na Brazil ndiyo nchi pekee zenye barabara za mwendokasi.

Uhalisia wa madai hayo

Ufuatiliaji wa JamiiCheck umebaini kuwa Taarifa hiyo inapotosha uhalisia.

Utafutaji kwa njia ya mtandao unabainisha uwepo wa barabara za mabasi yaendayo haraka katika maeneo mbalimbali duniani.

Mathalani taarifa ya Benki ya dunia (World Bank) ya mwaka 2022 ilibainisha majiji mbalimbali ambayo yanafadhiliwa na benki hiyk barani Afrika kwa lengo la kuendeleza miradi ya mabasi yaendayo haraka ikiwemo Abidjan, Dakar, Dar es Salaam (phases 3 & 4), Douala, Kampala, Kumasi, Maputo, and Ouagadougou.

Taarifa hiyo iliendelea kueleza kuwa hadi kufikia mwaka huo (2022) majiji ambayo yalikuwa yamekamilisha miradi ya barabara za mabasi yaendayo haraka kwa Afrika ni Dar es Salaam, Lagos, na Majiji ya Afrika kusini ni Cape Town, George, Johannesburg, na Pretoria.

Takwimu zilizotolewa na Seasia stats kwa mwaka 2024 ilitaja majiji 10 yaliyokuwa na mtandao mrefu zaidi wa mabasi yaendayo haraka ambapo majiji hayo namba moja likuwa ni
  1. TransJakarta (Indonesia)
  2. Bhopal BRT (India)
  3. Mexico City Metrobus (Mexico)
  4. Transmilenio Bogota (Colombia)
  5. Surat BRTS (India)
  6. Rainbow BRTS (India)
  7. Suzhou BRT (China)
  8. Ahmedabad BRTS (India)
  9. Islamabad metrobus (Pakistan)
  10. RIT (Brazil)

Aidha, mtandao wa barabara za mabasi yaendayo haraka nchini Indonesia TransJakarta ndiyo unaoshikilia rekodi ya dunia kwa kuwa mrefu zaidi kulingana na Guinness.
Back
Top Bottom