Balile: Magufuli katutenda, deni la nje lafikia shilingi Trillion 78

Kamuulize mama yenu amekuta shilingi ngapi hazina ndio ulete hapa upupu wako
 
kweli nchi sasa inapumua yaani kipindi cha mwendazake Jamaa wange Mlissu fasta , weeeee umseme mungu wa Chattle heheheeeeeee kina utapata tabu sana wanaweza wakakuua hadharani kabisa na cheo wangeongezewa
"NITAKUWA MSEMA UKWELI DAIMA,FITINA KWANGU MWIKO" kiapo cha Utii na Uzalendo...

Bora kufariki ukisimamia haki za wengine kuliko kufariki ukisengenya na kubagaza wengine ambao wakati wa uhai wao hukuwahi kuwaeleza ukweli.

Bora Askofu Kakobe aliyesema "KUTUBU" hata kama alibadilika kuliko huyu Mhariri.
 
Kakuta kweupee ni vile tu mstaarabu anamsitiri marehemu
Zile billion za Dola alizosema amekuta ni za bibi yako?

Mwambie mama yenu hawezi kufanikiwa kwa style hii ya kumchafua marehemu zaidi anamzidi kujianika na kutuonesha jinsi alivyo mweupe.

Any nilikuwa nimesahau kuwa ni mmakunduchi
 
Ulitaka apotezwe?
 
Nashauri akaunti binafsi za Magufuli na za familia yake yote kuanzia na mkewe na wanawe zipigwe ban na kuchunguzwa. Fedha zote zilizomo huko ziamishiwe serikalini. Haiwezekani nchi hii kufanyiwa uhuni wa kisukuma namna ile.
 
Huwezi kulinganisha mkopo wa Mkapa aliyekuwa Rais wakati GDP ya Tanzania ni USD 12B na Tax capacity ya TZs 300B kwa mwezi na mkopo wakati wa Magufuli aliyekuwa Rais wakati GDP ni USD 62B na tax capacity ya 1.3 T kwa mwezi. Balile unajivunjia heshima kwa kuchambua vitu juu. Naamini wachambuzi wengi mnafanya hivyo kwa kujua kwamba watanzania wengi wanapokea tu, hawana uwezo wa re-analysis.
 
Naona unatutoa nje ya Reli. Kukopa si dhambi hata kidogo, lakini kuwaaminisha wananchi wako kuwa miradi hiyo yote inafanywa kwa pesa zetu wenyewe bila kukopa ni kuudanganya UMMA na ni kosa kubwa sana la Jinai. Infact katika nchi zinazofuata sheria, kiongozi wa aina hiyo hushtakiwa mahakamani kwa vile katenda kosa la Jinai.

Rais Samia S H anakopa na analieleza Taifa kuwa nimekopa kiasi fulani, kwani watanzania wanatabu na hilo! Ni muhimu kusema kwa sababu kesho na kesho kutwa ni sisi wananchi ndio tutaolipa na kufaidika na huo mradi tuliokopea.

Kwa hiyo suala la msingi hapa ni moja tu: Kwanini Magu hakusema ukweli kuhusu upatikanaji wa Fedha za miradi aliyoijenga? Kwa hiyo maelezo kuwa watanzania twende kifua mbele kwa vile tunafanya mambo yetu bila kutegemea mabeberu yalikuwa ni mchezo wa kuigiza.

Fahamu ukikopa ni lazima ulipe na usipofanya hivyo umeiweka nchi katika Rehani. Na huwezi kwenda kifua mbele wakati nchi ipo kwenye Rehani kwa mabeberu.
 
Kikwete aliacha madaraka tukiwa na tax capacity ya 800B TZS kwa mwezi, GDP ya 43 B USD na alikopo 23T.
Hesabu linganishi zifanywe.
 
Zile billion za Dola alizosema amekuta ni za bibi yako?

Mwambie mama yenu hawezi kufanikiwa kwa style hii ya kumchafua marehemu zaidi anamzidi kujianika na kutuonesha jinsi alivyo mweupe.

Any nilikuwa nimesahau kuwa ni mmakunduchi
Hajawahi kumchafua, hayo wasema wewe!! Zile dola bilioni ilikuwa kauli ya kumsitiri marehemu
 
Swali kwako ni dogo sana, pamoja na analysis zako hizo za kina kuna maswali mawili tu unatakiwa uyajibu:
  1. Kwanini Serikali awamu ya 5 ilikopa mikopo ktk mabenki ya biashara yenye riba kubwa ya mpaka 6% badala ya mabenki kama benki ya Dunia, Afrika na IMF ambazo riba zake hazizidi 2%. (Mind you, hiyo tofauti ni kubwa sana.)
  2. Kwanini Magu Asiwaambie ukweli watanzania kuwa anakopa pesa kutekeleza miradi badala yake alituaminisha kuwa anatekeleza miradi hiyo kwa fedha zetu wenyewe hapa ndani ikiwa pamoja na gharama za uchaguzi?
 
Magufuli hayupo tena,lakini kama alikopa zaidi kwenye hizo private banks matrioni ya shilling ni wazi riba ni kubwa mno.Tukishindwa kulipa yasije yakageuka yalioikumba bandari ya Sri Lanka kama mdau alivyoiweka humu.
Hili jambo la serikali ya Magufuli kukopa sana lilikalipiwa sana na Mheshimiwa Zitto Kabwe hadi bungeni.
Na yawezekana kuna maofisa wa serikali walinufaika kibnafsi waliowezesha serikali kukopa kwenye hizo benki binafsi.

Kwa sasa serikali ijikite kupunguza matumizi yasio ya lazima kama kuongeza mikoa na wilaya,au kununua ma VX,na pengine kuendelea kuzika pesa za walipa kodi kwenye miradi kama mji mkuu Dodoma.
 
Nchi imetendwa vibaya sana!
 
Shule zetu hizi zina mambo. Kiukweli unakopesheka kama una madini yamelala ardhini, mafura , gesi n.k. Tena hata mikopo yako yote ya nyuma unaweza kusamehewa na wakaanza kukukopesha tena kesho yake. Halafu Mwaafrika hashangai kwa nini?

Eti nimekukopesha umeshindwa kunilipa, kesho nafuta madeni yote na kesho kutwa nakukopesha tena. Huyu mtu anakopesheka!
 
Ndiyo maana watu wanalilia KATIBA iliyojitosheleza!!! Haya mambo yasingetokea kama Bunge letu lilikuwa sio la mazuzu.
If we had strong institutions these poor decisions that Magufuli made would have been nipped in the bud!
Kabisa mkuu.... CCM hawataki kabisa Bunge huru. Ndio maana wametengeneza mfumo wa kuhakikisha bunge liko chini ya chama na by implication liko chini ya Mwenyekiti wa CCM ambaye ni Rais. Ni bunge la kizuzu kabisa, kutwa kupitisha maazimio ya kumpongeza Rais. Hivi ingekuwa TCRA kila siku inafanya kazi ya kuisifu mitandao ya simu watu wote tungekuwa tunatoka povu humu
 
Balile mnafiki wa hali ya juu sana apuuzwe. Eti deni la taifa limepaa kufikia Tr 78 kwanini hajachanganua thamani ya miradi iliyowekezwa kulinganisha?

Tangu achukue aliyepo sasa madarakani deni la taifa limefikia kiasi gani?

Mkopaji mkuu huwa ni waziri wa fedha na mipango sio rais
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…