Balile: Magufuli katutenda, deni la nje lafikia shilingi Trillion 78

Balile: Magufuli katutenda, deni la nje lafikia shilingi Trillion 78

Meko alikopa mikopo ya hovyo, fullstop!! Mikopo nafuu waliyokopa wenzie kabla yake, na anayokopa Mama sasa alinyimwa kutokana na udikteta wake uchwara!! Trl 29 kwa miaka 5, tena mikopo ya biashara, thats insane!! Huyo Meko wako ndiyo alikuwa hakopesheki mikopo nafuu

Wewe unaekopesheka c ukachukue huo mkopo
 
We ndo utueleezee vizuri unadhan imeenda wap!! Maana transaction zote za serikali n documented!! Kama unadhan kuna upotevu wa hela n sh ngap
Assad alijaribu kusema kuna 1.5 tril hazijulikani zipo wapi kwenye hesabu, unajua kilichompata, kutokana na hilo tunaweza sema hela nyingi kipindi cha awamu pendwa ilikuwa inatolewa kutegemea na Bwana Yule anachosema/kuamua! Hakuna aliyethubutu kumuuliza chochote kuhusu matumizi na documentation! Inachofanya awamu hii ni kujaribu kumsitiri, kufunika kombe! Wakiamua miaka 5 ya jamaa ichunguzwe kwenye matumizi ya fedha itakuwa ni aibu haijapata kutokea nchi hii
 
Magufuli katutenda deni la taifa, trilioni 78 Samia msalabani

Jamhuri October 26, 2021

Na Deodatus Balile

Kazi hii ya uandishi wa habari moja ya majukumu yake ni kuanika ukweli minong’ono inapotawala katika jamii.

Kwa sasa kuna minong’ono mingi. Minong’ono imeanza baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kutangaza hadharani mkopo wa Sh trilioni 1.3, alioukopa kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na akatangaza miradi lukuki itakayotekelezwa kwa kutumia mkopo huo.

Miongoni mwa miradi ya kihistoria ni ujenzi wa madarasa ya sekondari 15,000 nchi nzima na madarasa ya shule za msingi 3,000.

Kwa sasa inakadiriwa kuwa nchi ina upungufu wa madarasa 11,000, lakini Rais Samia ameamua kuona mbali.

Ameamua kufuta mfumo wa zima moto, ambapo kila mwaka wazazi wanakabwa koo vijijini kuchangia ujenzi wa madarasa.

Baadhi ya wazazi pia wameanza minong’ono kuwa watoto wao wamepewa mikopo kidogo, yaani Sh 600,000 kama ada vyuoni.

Hawajui kuwa miaka yote imekuwa hivyo na wakati mwingine wengi wanakuwa hawapati kabisa hata senti tano ya mkopo.

Sitanii, naomba nizungumzie kwa ufupi miezi sita ya Rais Samia akiwa Rais wa Tanzania baada ya kuapishwa Machi 19, 2021.

Nakumbuka vema kilichotokea, maana baada ya kifo cha Rais John Magufuli kulitokea kama sintofahamu hivi.
Wapo watu walioamini Rais Samia angeendelea kuwa Kaimu Rais, baadhi walidhani tunakwenda kwenye uchaguzi mpya na wengine hawakufahamu nini kitatokea.

Asubuhi ya Machi 18, 2021 niliamkia studio za Televisheni ya Taifa (TBC1) na TBC Taifa (radio) kufanya mahojiano na Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Dk. Ayub Rioba.

Hii ilikuwa ni baada ya kifo cha Rais John Magufuli, kilichotokea Machi 17, 2021. Ikumbukwe wiki moja kabla nilikuwa nimefanya mahojiano na kituo cha Star TV nikasema tuambiwe bayana Rais Magufuli yuko wapi na anafanya nini.

Machi 18 pamoja na kwamba nilikuwa bado Kaimu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), ambapo baadaye nilichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa TEF Mei 22, 2021, ilinilazimu kutoa ufafanuzi huo uliokuwa tamko zito.

Sitanii, tamko nililolitoa lilizaa kuapishwa kwa Rais Samia kuwa Rais wa Awamu ya Sita Machi 19, 2021. Nilirejea Katiba ya Tanzania (1977) Ibara ya 37(5) inayosema: “Endapo kiti cha Rais kitakuwa wazi kutokana na Rais kufariki dunia, kujiuzulu, kupoteza sifa za uchaguzi au kutomudu kazi zake kutokana na maradhi ya mwili au kushindwa kutekeleza kazi na shughuli za Rais, basi Makamu wa Rais ataapishwa na atakuwa Rais kwa muda uliobaki katika kipindi cha miaka mitano na kwa masharti yaliyoelezwa katika ibara ya 40, kisha baada ya kushauriana na chama cha siasa anachotoka Rais atapendekeza jina la mtu atakayekuwa Makamu wa Rais na uteuzi huo utathibitishwa na Bunge kwa kura zisizopungua asilimia hamsini ya wabunge wote.”

Kwa mara ya kwanza kupitia makala hii ninakisema kilichotokea baada ya tamko hilo. Walinipigia simu watu wengi wakiwa na hofu.

Baadhi hawakufahamu Katiba inasemaje. Walinishutumu wakidai nimetangaza utaratibu wa kwangu, kwani baada ya kifo cha Rais kinachofuata ni uchaguzi.

Hii ilinipa shida kuona hata baadhi ya wabunge hawakufahamu nini kinafuata baada ya kifo hicho. Machi 18, 2021 itabaki kuwa siku ya kihistoria kwangu, kwani ujumbe nilioutoa ulitangazwa katika radio zote za ndani na za kimataifa na siku moja baadaye Rais Samia akaapishwa.

Sitanii, leo ninazungumzia mzigo wa madeni ambao Rais Magufuli amelitwisha taifa letu. Nimetangulia kusema na ninarudia, mimi ni msema kweli. Wala sipepesi macho katika kusema ukweli.

Wakati Rais Magufuli kwa miaka mitano yote alikuwa anawaaminisha Watanzania kuwa nchi inajenga miundombinu na inanunua ndege kwa kutumia fedha zetu wenyewe, uhalisia ni kinyume chake.

Kwa kipindi cha miaka mitano tu, Rais Mafuguli amekopa fedha nyingi kuliko fedha zote alizokopa Rais Benjamin Mkapa kwa miaka 10 aliyokaa madarakani.

Kwa miaka mitano, amekopa pia fedha nyingi kuliko alizokopa Rais Jakaya Kikwete kwa miaka 10 naye aliyokaa madarakani.

Rais Mkapa alirithi madeni mengi mno. Alipambana nayo, akaiingiza nchi katika Mpango wa Kusamehe Madeni Nchi Maskini (HIPC) na hadi anatoka madarakani, Tanzania ilikuwa inadaiwa Sh trilioni 20 tu.

Rais Kikwete wakati wake deni la taifa liliongezeka kwa Sh trilioni 23, hivyo akatoka madarakani deni la taifa likiwa Sh trilioni 43 kwa miaka 10. Rais Magufuli kwa miaka mitano tu, deni la taifa limeongezeka kwa Sh trilioni 29 na kufikia Sh trilioni 72 hadi anafariki dunia Machi, 2021.

Sitanii, kwa kasi hii ya ukopaji ina maana kama angekaa madarakani kwa miaka 10 kamili na akaendelea na kasi ya ukopaji wa wastani wa Sh trilioni 29 kwa miaka mitano, basi angetoka madarakani deni la taifa likiwa Sh trilioni 101 kufikia mwaka 2025.

Kuna jambo baya halisemwi. Rais Magufuli amekopa mikopo ya kibiashara inayoanza kulipwa baada ya miaka mitatu na inapaswa kulipwa ndani ya miaka minane, ikiwa na riba za kati ya asilimia 6 na 8.

Baadhi ya mikopo hii imeiva tayari. Imeanza kukuza deni la taifa kwa kasi kutokana na riba. Deni la taifa sasa limefikia Sh trilioni 78.

Kwa vyovyote vile iwavyo, Rais Samia anapaswa kuchukua hatua za haraka, ikiwamo kuunda timu ya majadiliano na wakopeshaji kwa ajili ya kubadili masharti ya mikopo ya kibiashara aliyochukua Rais Magufuli.

Anapaswa kuomba msamaha wa riba na pengine kuomba kuongezewa muda wa kulipa deni kama ulivyo utaratibu wa mikopo kwa serikali nyingi duniani.

Mikopo mingi kwa serikali huwa inalipwa kati ya miaka 20 hadi 50 kulingana na ukubwa wa mkopo na hutozwa riba kati ya asilimia 0.3 hadi asilimia 1. Mikopo ya aina hii inapatikana katika Benki ya Dunia, Shirika la Maendeleo Duniani, Benki ya Maendeleo Afika na nyingine za aina hii.

Kwa bahati mbaya na kwa masikitiko makubwa, kwa miaka mitano Wazungu tuliowaita mabeberu, ila tukawa tunakopa fedha zao kupitia benki za biashara. Kwa hali halisi, madeni haya yakiiva yote, ikiwa hakuna majadiliano ya dharura kuomba marekebisho ya masharti ya mikopo tuliyochukua chini ya Rais Magufuli, itafika mahala asilimia 60 ya bajeti ya taifa letu itakuwa inakwenda kulipa madeni. Waliomo serikalini watajua la kufanya katika hili.

Sitanii, ninafahamu baadhi ya wasomaji watakuwa wanaanza kufuka moshi kwa kusema ukweli huu. Wanajiuliza taarifa hizi nimezipata wapi? Taarifa hizi si za siri. Ziko wazi kwenye tovuti ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Nimepitia taarifa za mapitio ya mwenendo wa uchumi tangu mwaka 2000 hadi 2021. Zipo mtandaoni na zinaonyesha deni lilivyokua hatua kwa hatua. Kwa nia ya kuweka uelewa unaofanana, ifuatayo ni hali ya deni la taifa tangu mwaka 2005 hadi 2021.

Oktoba 2005, deni la nje lilikuwa USD milioni 8,361.9 sawa na Sh 19,286,471,493,000 na deni la ndani lilikuwa Sh 1,712,800,000,000. Jumla kuu ya deni wakati Rais Mkapa anaondoka madarakani lilikuwa Sh 20,999,271,493,000 (Sh trilioni 20.9). Nimekokotoa hesabu hizi kwa kutumia viwango vya BoT vya kuuza dola ya Marekani ambavyo ni USD 1 kwa Sh 2,306.47.

Oktoba 2015, wakati Rais Kikwete anatoka madarakani deni la nje lilikuwa USD milioni 15,321.3, sawa na Sh 35,338,118,811,000 na deni la ndani lilikuwa Sh 7,826,200,000,000. Jumla kuu deni la nje na deni la ndani lilikuwa ni Sh 43,164,318,811,000 (Sh trilioni 43.1).

Deni la taifa lilianza kupanda kwa kasi Oktoba 2016. Deni la nje lilipanda na kuwa USD milioni 16,407.6 sawa na Sh 37,843,637,172,000, huku deni la ndani nalo likipanda na kuwa Sh 10,089,000,000,000. Jumla kuu ya deni ikafikia Sh 47,932,637,172,000 (Sh trilioni 47.9).

Oktoba 2017 deni la nje lilipanda kwa kasi kubwa na kufikia USD milioni 19,074.4 sawa na Sh 43,994,531,368,000. Kutokana na makandarasi kutolipwa deni la ndani nalo lilikua na kufikia Sh 12,563,300,000,000. Jumla kuu ya deni kwa mwaka huo likawa Sh 56,557,831,368,000 (Sh trilioni 56.5).

Oktoba 2018, deni la nje lilizidi kupanda na kuwa USD milioni 20,759.1 sawa na Sh 47,880,241,377,000, huku deni la ndani nalo likipanda na kuwa Sh 14,116,100,000,000. Jumla kuu ikawa Sh 61,996,341,377,000 (Sh trilioni 61.9).

Oktoba 2019, mwanamume aliongeza tena deni la taifa, deni la nje likafikia USD milioni 22,569.4, sawa na Sh 52,055,644,018,000, huku deni la ndani likipanda na kufikia Sh 14,187,400,000,000. Jumla kuu ya deni ikafikia Sh 66,243,044,018,000 (Sh trilioni 66.2).

Oktoba 2020, deni la nje lilipanda na kufikia USD milioni 23,599.3, sawa na Sh 54,431,077,471,000, huku deni la ndani likifikia Sh 15,608,500,000,000. Jumla kuu ikafikia Sh 70,039,577,471,000 (Sh trilioni 70).

Machi, 2021 wakati Rais Magufuli anafariki dunia, deni la nje la Tanzania lilikuwa limefikia USD milioni 24,429.2, sawa na Sh 56,345,216,924,000. Deni la ndani nalo lilipanda na kufikia Sh 16,116,500,000,000. Jumla kuu, deni la taifa lilifikia 72,461,716,924,000 (Sh trilioni 72.4).

Kilichofuata baada ya hapo, madeni yameanza kuiva kwa ajili ya kulipwa, huku mengine yakizalisha riba ya kufa mtu.

Makandarasi wengi Tanzania wanadai mabilioni kati ya hizo Sh trilioni 16 ambazo ni deni la ndani hawajalipwa siku nyingi. Kutokana na hali hiyo, madeni haya yaliyokopwa bila mpangilio katika benki za biashara yameanza kuwa msalaba kwa Rais Samia.

Taarifa ya hali ya Uchumi ya BoT ya Septemba, 2021 inayorejea mwezi Agosti, 2021 kutokana na mazingira hayo, deni la nje limekua na kufikia USD milioni 25,956.1 sawa na Sh 59,866,965,967,000, huku deni la ndani nalo likikua na kufikia Sh 18,225,000,000,000. Ukuaji huu unafanya kiwango cha deni la taifa kufikia jumla kuu ya Sh 78,091,965,967,000 (trilioni 78).

Sitanii, deni hili likigawanywa kwa Watanzania milioni 60, bila kujali mkubwa na mdogo, kila Mtanzania anadaiwa Sh 1,301,533 (Sh milioni 1.3). Hata hivyo, wataalamu wa uchumi wanasema deni hili si tishio kwa uchumi wa taifa letu kwa sasa kwani liko katika uwiano wa asilimia 30 kwa uchumi wa taifa letu, wakati kuna mataifa Afrika ambayo tayari yana uwiano wa asilimia 54 ya deni kwa uchumi wa nchi zao, ila wanaionya serikali iepuke mikopo ya kibiashara ina riba kubwa, masharti mabaya na inalipwa kwa muda mfupi.

Pale Dodoma, tumeona Rais Samia ameanzisha utaratibu mpya wa ukweli na uwazi katika mikopo. Ameeleza fedha alizokopa zitafanya nini kwa kuorodhesha miradi itakayotekelezwa na akatueleza amezikopa kutoka wapi.

Ninajiuliza, hivi ilikuwa ni kwa faida ya nani Rais Magufuli na wapambe wake kuficha ukweli kuwa miradi ya reli, barabara, umeme, ujenzi wa hospitali na mingine mingi aliyoijenga alikuwa anakopa?

Hivi sisi kama tungejua anakopa, tungemzuia? Lakini si tungepata fursa ya kumshauri asichukue mikopo ya kibiashara inayoanza kututoa utumbo sasa? Mungu ibariki Tanzania.

Copyright [emoji2398]2021. Gazeti la Jamhuri
Huyu ni mwanamtandao hana lolote zaidi ya fitina. Timu JK hawa

Sent from my TECNO P704a using JamiiForums mobile app
 
Ni bora ya Magufuli kuna miradi tunaiona kwa macho ,Mbowe alichangisha bilkion7 za wabunge na akatafuna zote.
Ofisi ya chama pale ufipa ni pagala vilevile hadi leo
 
And alikuwa anakopa kwa siri as if hiyo hela angelipa kutoka mifukoni mwake, akiwa majukwaani anawatukana mabeberu, Usiku anawapigia simu kuwakopa hela!! Trl 29 kwa miaka 5 ni nyingi sana, and sijui kafanyia nini hiyo hela, maana mamiradi yake yote yapo under 50% ya utekelezaji
[emoji106][emoji106]
 
Toa mfano acha projo Huyo mama yenu hakopesheki ndo maana hela za UVICO zimekuwa za kudanganyia wananchi miradi uchwara!

Kwa kuona kwamba hakopesheki ameanzisha tozo ovyo ovyo! Unafikiri hao IMF&WB huwa hawajui kuwa Rais fulani ni mtendaji sio wa maneno! Hapa wanajua Mama ni Maneno sio vitendo! Ila JPM walijua ni vitendo sio maneno!
Onyesheni basi hizo 29 Trilioni mlizokopa kimyakimya usiku wa manane mmezitumiaje kwenye hiyo miradi? Maana mlituambia kila kitu ni fedha zetu za ndani...
 
Ukiangalia mikopo mingi ya IMF na WB iliyotolewa enzi za JPM ni ile ambayo ni mwendelezo wa awamu zilizopita!!

Au ndo kwavile unadhani kukopa benki binafsi ni suala la kujivunia?
Zipo faida na hasara za kukopa WB na IMF na pia kukopa benk binafsi.

Hasara ya kukopa WB na IMF nikiwa wakopeshaji hawa wanakupangia fedha walizokukopesha uzitumieje na kuchunguza sana masharti wanayokupa ukiyafuata kama yalivyo huo mradi uliopanga kuutekeleza kwa fedha hizo hautakaa uje kukuletea tija. Kibaya zaidi uambatanisha na masharti ambayo hayahusu financial issues kwa nchi mkopaji. Mifano ipo. Riba inasemwa ni ndogo hatuelezwi udogo wake.

Hasara ya kukopa benki binafsi nikuwa riba yao nikubwa ingawa hatuelezwi ukubwa wa riba hiyo. Mikopo ya hawa jamaa haina masharti zaidi ya kuelekezwa ulipe deni kwa wakati. Mifano ipo
====
Sina hakika mkuu wangu, Chige hauyajui haya.

Pitia peer reviewed article hii inayofafanua vizuri hasara ya kutumia wb na imf hasa kwa nchi za Afrika.

 
Kwa akili zake unapewa tu hela kama njugu, aende wizara ya fedha DMO office wamfahamishe kanuni za kukopa nje na frameworks za kukopesheka wanazotumia.

Kushindwa kulipa madeni na kuendeleza miradi ni mawili either mapato yametereka au wakopaji awana imani na mama.

Sio kuja kutunga uongo na kutupia lawama watu wengine.
Ametuwekea BOT summary report since 2000 to date halafu unasema uwongo? Acha undezi jombaa na kama wewe una ubavu tuwekee na wewe BOT report unayohisi ni ya kweli. Msilete mahaba yenu ya matandu/ukoko wa wali kwenye masuala nyeti ya uchumi wa nchi.
 
Kwa nini mnalazimisha mtu atawale kama Magu? Nyie jamaa vipi? Unadhani walioweka ukomo wa uongozi ni wajinga? Miaka yako 10 tawala vile unaamini, ikiisha unapisha mwingine atawale anavyoamini, mazuri yako atayaendeleza and mabaya yatapigwa chini, na itaendelea hivyo!!

Samia siyo Magu na hawezi kutawala kama Magu, huo ndiyo ukweli!! Na baada ya Samia atakuja mwingine naye hatatawala kama Samia!! Huu upuuzi wenu wa kumgeuza Magu SI Unit ya kutawala TZ hakuna ataufuata!! Kwanza bora hata ya Samia anajitahidi kuendeleza mamiradi hewa ya Magu, Magu yeye kutwa alikuwa anapita kuwatukana watangulizi wake...
Igweeeeee [emoji120][emoji120][emoji106][emoji106]
 
Tupe na thamani ya miradi iliyotokana na deni, kama uwiano wa deni na uchumi kukua ni 30% huko kutendwa kunatokeaje?

Anzia upanuzi wa bandari, SGR, Upanuzi wa highways, mabarabara ya mitaa, stand za mabasi nchi nzima, New mwendokasi roads, vituo vya afya nchi nzima, Hospitali za wilaya nchi nzima, Mashule, Ndege, upanuzi wa viwanja, ujenzi wa Dodoma plus Ikulu ya Chamino, usambazaji umeme kila kijiji, vivutio vya utalii, Hydropower ya Nyerere na vingine vingi. Ulitegemea hela haitumiki?

Then go back angalia uwiano wa uchumi na ukuaji wa madeni! Njoo kwenye probability means of return. Angalia makusanyo per annual sio kuandika kinafiki.
Huyu mwandishi kasomea uchumi au ni mchumua tumbo tu .Mbona aelewi kabisa anachoandika.?Huyu ni mchumia tumbo tu.Amepewa vijisenti na timu Fulani.Tunaijua.Ili amchafue Mzalendo Magu.
 
Balile ile heshima yangu kwako nimeipunguza kaka. Hizo numbers za BOT hazisomwi bila consideration ya mambo mengi. Alafu unaposema alidanganya kuwa miradi tunafanya kwa fedha zetu ni kusema uongo na unfortunately zipo dhambi ni za kuepuka kama kusema uongo makusudi kwa lengo la kuharibu utu wa mtu ambaye hawezi kujitetea!

Saga la SGR, na bwawa la Nyerere inafahamika nini kilitokea hadi JPM akaamua kuanza kibishi kwa funds za ndani! Hakuna aliposema hii miradi itakamilishwa na fedha za ndani tu bali hakutaka kushindwa kupitia masharti ya mikopo ila lengo lake lilikuwa kukopa tangu awali.

Uongo kama huu, kutenga muda kuuandika na jinsi ulivyokuwa unachagua maneno ni dhahiri hili lina dhamira isiyo njema.
 
Balille ameleta hoja muhimu sana sana kwetu waungwana humu tuichambue. Kosa lake lililoshusha credibility yake ni kutaka tuamini kwamba alisababisha Rais Samia aapishwe kama Rais kwa mujibu wa Katiba ya nchi. Kwamba Katiba aliijua yeye tu. Serious? Anyways tusimlaumu timing kwa sababu sote tulijua JPM hakuwa ana entertain mijadala inayokwenda kinyume na malengo yake binafsi. Alisema ni pesa zetu za ndani tu na kutuambia ubaya wa wazungu/mabeberu huku tukijua wazi anakopa kama anatukomoa wanyonge wake na mbaya zaidi kwa hao hao mabeberu. Sote tunajua malengo ya JPM kutaka kumuondoa Govornor mkweli Ndulu na CAG Assad ili aendelee kudanganya umma mambo ya kiuchumi, fedha na ubadhirifu na hapa ndipo tulipo na hoja za Balile. Tusingekuwa Taifa tunu yake kuu ni UNAFIKI, Bwana Rioba CEO wa TBC angeandaa mjadala wa wazi miongoni mwa wasomi, raia na wanasiasa tujadili kwa hoja na facts. Lakini Lissu alinyanyuka kukemea uongo mwingi wa JPM pamoja na viongozi wachache wa dini. Uthubutu wa namna ya pekee! Ukweli ni kwamba JPM alikopa kifichoni mwa walipaji hiyo mikopo na ukweli ni kwamba faida ya hiyo mikopo alipeleka ALIPOKUWA na maslahi binafsi kwa manunguniko kwa wengi na hatuna uhakika kama yote ilitumika kwa maslahi ya Taifa hasa katika mazingira ambayo CAG hakutakiwa kufanya kazi yake. Kwa sasa mwacheni Rais Samia afanye anachoona kitatuokoa na nafurahi anashirikisha viongozi waliopita. Wito wangu Rais aruhusu upinzani, amwachie Mbowe, Lissu, Zitto et all, ili tusifiche mambo ambayo mwisho wa siku yanatufikisha tuliko leo. Hapo ndio umuhimu wa Katiba mpya unaonekana. Kumbukeni Mficha uchi....Mficha Marathi...
 
Mkuu 50% ya project ni kubwa! Sema unachuki na JPM ndo maana hauoni alichofanya JPM hakujipendekeza kwao walikuja wenyewe baada ya kuona mziki wake! Angalia project kama zifuatazo
•Tanzania haikuwahi kuw ana Radar tokea uhuru amejenga nne kwa mkupuo Dar,mwanza,mbeya na klimanjaro
•Tanzania haikuwahi kuwa na Mahakama zakisasa tokea uhuru mahakama standard zilikuwa ni zile za kanda! Leo tunazungumzia mahaka zenye miundombinu ya kisasa!
•Nchi hii ilikuwa na hospital kubwa za kanda nyinhi za mashirika ya dini leo hii tuna hospital kubwa za hadhi ya kitaifa kule Musoma, mtwara,mbeya n.k Wao waliopita hawakufanya haya si kwa kuwa hawakuweza tu bali hata utendaji wao haukuwa katika viwango vya JPM!
•Vituo vya afya,hospital za wilaya, masoko.
•Uanzishwaji wa masoko ya madini mfano soko la dhahabu Geita limeinbiza takribani trilion tatu kwa miaka miwili na nusu!
•Upanuzi wa bandari hapo Dar, mtwara ma tanga!
•Ufufuami wa treni kutokea Dar mpaka moshi/arusha!
•Ujenzi wa flyover,busisi,mto wami n.k

Hayo ni ambo yanahitami usimamizi na fedha kwa hiyo kama matokeo yanaonekana kukopa kwake hakuna shida! Hata nyumbani kwako ukikopa benki ili ujenge nyumba na ukajenga kwa ubora na ikaonekana hakuna mtu atakaye kulaum! Ila kwa vile mmezoea maneno sio utendaji endeleeni kumsifia huyu mama ambaye hana hata historia ya utendaji kwenye maisha yake, kitu pekee kimemfikisha hapo ni kubebwa na siasa!
Umeeleza meeengiii lakini hujajibu Trilioni 29 zimetumikaje? Kulikuwa na shida gani kuweka wazi in public matumizi ya hizo fedha kama aliyofanya juzi SSH? Hiyo si ni pesa ya umma unaficha matumizi yake kwa nini? Pili kujenga majengo makuubwaa kama hayo mahospitali unayosema lakini hayana vifaa tiba, watumishi wa kutosha, madawa etc kuna faida gani? Unajenga masoko (Mtwara na Dodoma) kwa billions of money but mwisho wa siku hakuna wafanyabiashara wanataka kwenda huko really?? Unajenga mahakama sawa halafu mahakama unazikandamiza hazitoi haki what's that?? Pale penye kutoa haki hata mahakama ikiwa chini ya Mwembe watu wataisifia kwa kutoa haki!!
 
Masharti ya mikopo ya IMF ni nafuu zaidi kuliko ya private commercial banks. This is a fact!
Concessional loans inayoambatana masharti ya kutiliwa mashaka.
=====

"Whilist the World Bank and IMF require budget cuts in the public sectors of the African
countries, the Structural Adjustment Programme permitted public sector spending on arms and the overall military sector. As a direct result, African government spending on arms import increased leading to the proliferation of arms in the continent thereby increasing the occurrence of conflicts and the violation of human rights on a wider scale.

The United States (one of the architects of the IMF) is the world’s biggest arms exporter. In 1999, the United States exported well over $11.8 billion arms and armaments, out of which about $7.6 billion worth were sold in Africa at the peak of SAP.

Sad, isn’t it?" Written by Kingston (2011).
 
Acha mbwembwe...

Ungekuwa unafahamu basi ungeonesha ufahamu wako from the very first post!!

Nimekukosoa kwa jambo la wazi kabisa ndo unataka kuleta habari za masharti ya IMF...

Ni yupi unayetarajia kumdanganya kwamba masharti ya IMF ni mabaya zaidi kulinganisha na yale ya benki zilizo sekta binafsi?!

6AA27C2F-5F8B-4D81-ACD1-38E7DED966F8.jpeg


Ungesoma post hii na mwenye uelewa wa ‘public finance’ na historia yake vizuri.

Ungefahamu DMO stands for ‘Debt Management Office’ na hizo department zinatakiwa kuwa wizara fedha zote duniani, hasa nchi maskini kama sehemu ya kuangalia mikopo ya nchi na kufanya stress ambazo IMF na WD wanazipitia kwa kufuata frameworks zako.

Sasa maana yake nini ili ukope kuna frameworks zao moja wapo ni hiyo DSA, by know you should public finance sio uwanja so tusipotezeane muda.
 
Kuanzia 2016-2020 kumbe ulikuwa unatania eti?

Kupewa tu Uenyekiti wa Jukwaa 2021 na baada ya Mh.Magufuri kufariki Dunia ndio unasema "utanii" si ndio au?

Siku zote hizo 2016-2020 nyinyi kama Jukwaa lenye taarifa kwanini hamkuyasema haya (Takwimu za nyuma).?


Ifike mahala watu wazima tuwe tunaheshimiana walau kidogo,kuna siku tutakuja kuchekwa na wahisani huku kizazi kijacho kikituzomea.

Mikopo iliyokopwa wengi tumeona matunda yake,kumlaumu Hayati Mh.Magufuri huko ni kutengeneza mazingira ya kuhujumu miradi inayotegemea mikopo hiyo.

Ndugu Balile kipi bora kuendelea kukopa tumalizie miradi tuanze tufanye return au tuache kukopa miradi isitekelezeke tupunguze madeni?

Hata hivyo nini sababu ya kusema haya kwa sasa?
Na labda unategemea nini kifanyike?

Hujuma na njama sio kuiba au kufanya jambo lolote la kivitendo,kalamu/ulimi ina/unaweza kuwa
na silaha nzito ya kuhujumu/kula njama za kuhujumu.

Siku zote mtu mzalendo sio muoga wala mnafiki,mzalendo wa kweli husema ukweli pasipo kuangalia anayemsema atamfanya nini ,ungelisema hayo kipindi unayemsema yupo hai ungeliliokoa Taifa/kupata ufafanuzi kwa kina,kwa sasa ni kama vile unajichoresha na kujihaibisha na kuhaibisha taaluma ya Uhandishi wa habari.

Tunaomba utupe takwimu za riba ya mikopo hiyo kwa awamu zilizopita (Mh.Mkapa na Mh.JK) kwa kuwa riba zake usituambia hazijaiva hadi leo (Mikopo yake bado hiko fixed au?).....elewa ya kuwa riba za mikopo mara nyingi ni Geometrically na sio Arthmetrically unless otherwise...?
 
Nafikiri alikopa kulingana pia na uwezo wa nchi! Unajua ukuaji wa uchumi ndo uwezo wa kukopesheka pia! Na utambue miaka yote tumekopa lakini kilichokuwa kinafanyika cha maana hakikuwepo! Ila kwa vile wote mmegeuka wakosoaji wa Magufuli ili kumlinda mama! Mwambie apambane asisingizie Madeni hata Marekani wana madeni ya kutisha!
Mleta mada kaandika ukweli mtupu. Awamu ya tano imeacha mzigo wa madeni. Mama anapambana kwa ubunifu alionao ili yaweze kulipwa.
 
Back
Top Bottom