Hivi unadhani mabeberu ata kwa kupitia private banks yanakopesha nchi maskini bila ya IMF na WB kufanya stress test kama unaweza kulipa madeni yako huko mbele based on your tax collections.
Hivi hoja ni kuweza kulipa deni au kukopa kwenye private commercial banks ambazo riba zake zinakuwa juu?!
Embu fuatilia sakata la ‘Credit Suisse’ linaloendelea wamelimwa fine ya $475 million na kulazimishwa kufuta deni $200 million walilokopesha taasisi ya serikali msumbiji; yote kwa sababu huo mkopo ulitolewa kwa swirl bila ya kuwaambia IMF na WD.
Ni kweli wamelimwa hicho kiwango,lakini SIO KWELI kwamba eti wamepigwa faini kwa sababu walitoa mkopo bila kuwaambia IMF na WB... SIO KWELI!!!
Na wala hawakuwa punished na IMF/WB kama unavyodai hapa bali wamekuwa punished na regulators wa US, UK, na Uswisi!! Yaani ni kama uchunguzi ambao hatima yake BAE walitakiwa kurejesha change ya radar...
Kwa maelezo yako hayo inaonesha wazi kwambahata wewe HUJAFUATILIA hilo unalowaambia wengine hawajafuatilia!
Na lau kama ungefuatilia, usingeleta ushabiki kwa sababu tu unaona kuna wmtu ameguswa! Badala yake, ulitakiwa kuwa na hofu kwa taifa lako kukopa kwenye private banks!! Makosa ya Credit Suisse ni yale yale yalizoeleka unapoamua kukopa kwenye benki za biashara!
Pamoja na mambo mengine, CS na benki nyingine ya Russia wanatuhumiwa ku-violate missing ya money laundering control na rushwa! Millions of dollars zilishia kwenye mifuko ya watumishi wa benki waliofanikisha kupatikana kwa mkopo!!
Na hayo ndo matatizo ya hizi benki binafsi!!! Hata wakati wa JK, serikali yake iliwahi kukopa Stanbic, na baadae ikagundulika kampuni ya Growth Market Advisors waliingiziwa zaidi ya Sh 10 Billion na Stanbic!
Ni hawa Growth Market Advisors ndio waliwezesha serikali kupata mkopo kutoka Stanbic!
So, pamoja na possible higher interest rates, matatizo mengine ya benki binafsi ndo hayo!!
Mozambique wameshindwa kulipa madeni yao mengine jamaa donors wamewaka watalipa wao ‘Credit Suisse’ waliotengeneza madeni ya nyongeza nchi maskini bila ya ridhaa yao.
Donors gani?! Ina maana financial regulators ni donors?
Unadhani mzungu mjinga, JK na Mkapa sio kwamba walikua awataki kukopa, sema walikuwa awakopesheki na hela ilikuwa aifanyi kazi iliyokopewa.
Ushabiki mwingine mbaya sana!!!
Wenye akili timamu walijua IMF na WD watatia nanga soon, ‘mama’ kujifanya anaenda na utaratibu wake; ameshaonywa na watu wengi sana kaa mbali na JK, rudi njia ya Magufuli hataki na bado.
Yaani we jamaa bhana!!
Yaani ili mradi uweze kutetea ujinga, unafikia kushangilia mikopo from private banks na kuponda kukopa IMF?! Hivi unafahamu kwanini Mkapa aliacha deni dogo?!
Ingawaje Mwandishi kasema Mkapa"
Alipambana nayo, akaiingiza nchi katika Mpango wa Kusamehe Madeni Nchi Maskini (HIPC) " lakini uhalisia HIPC Initiative ulikuwa ni mpango wa IMF, WB na Paris Club. Mpango huu uliasisiwa kabla Mkapa hajawa Rais, na ni huo Mpango ndio uliingiza Tanzania.
Mkapa alipambana kutekeleza matakwa ya HIPC ili hatimae nchi ifutiwe madeni, na kweli, kwa ujasiri mkubwa, Mkapa alifanikiwa katika hilo na hatimae kupunguziwa mzigo wa madeni!!
Hizo ndo faida za kukopa kwa IMF, WB na Paris Club!!