Balile: Magufuli katutenda, deni la nje lafikia shilingi Trillion 78

Balile: Magufuli katutenda, deni la nje lafikia shilingi Trillion 78

Unaona kama anataka kwenda China si lazima apande ndege kwenda dar ndo achukue fulaiti ya China! Mkuu sisi tumezunguka nchi hii! Watu wa mikoa hiyo ya Geita na mikoa jirani watautumia uwanja maana wako vizuri! Ukitaka kujua nenda huko geita ukaone watu walivyo na pesa! Usifikiri kupanda mwendo kasi ndo ujanja!
Kwa mtazamo wako, kati ya Dodoma na Chato wapi palistahili kuanza kujengwa sehemu ya kutua ndege kubwa? Maana challenge kubwa leo hii ya Dodoma ni kwamba kuna baadhi ya ndege haziwezi kutua pale, leo hii ikitokea Putin anakuja TZ itamlazimu Rais akampokee DSM or (Chato!!!!)!! Uwanja wa chato haukuwa na sababu ya kuharakishwa kwa namna jamaa aliuharakisha...
 
Wewe hujui hivi wewe unafikiri Chato ni kijiji? Endelea kusikiliza wapuuzi hapa! Chato ina miji kama Katoro kuna watu wanahela ya kupanda ndege na wanafata bidhaa China!

mkuu sio kila mwenye pesa lazima afwate mzigo china acha ushamba[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Unafiki mtupu! Kwani wakati JPM yupo hiyo tovuti ya BoT haikuwepo?
Ukweli kwamba yeye peke yake ndiye alikuwa anaijua Katiba na andiko lake ndilo lilifanya katiba ifuatwe? Take my words, anataka kuvizia uteuzi

Ukweli mchungu haijarishi umesemwa wakati gani
 
Mswahili ukiwa naye anakusifia kwelikweli. Ukiondoka tu na akajua kutokuwepo kwako kejeli zake na matusi yake ni ya kiwango cha SGR
 
Naona huu uzi umejaa mtifuano kati ya watoto wa MAMA na watoto wa MWENDAZAKE 🤣🤣 ila mwisho wa siku dhambi haisafishwi kwa dhambi
 
Tupe na thamani ya miradi iliyotokana na deni, kama uwiano wa deni na uchumi kukua ni 30% huko kutendwa kunatokeaje?

Anzia upanuzi wa bandari, SGR, Upanuzi wa highways, mabarabara ya mitaa, stand za mabasi nchi nzima, New mwendokasi roads, vituo vya afya nchi nzima....
We ni mpumbavu,miaka yote 6 mradi gani umeisha? Badala ya kugharamia hiyo miradi kwa mikopo nafuu na makusanyo unaenda Kukopa mikopo ya miaka 3 na riba kubwa huku miradi inakamilika kwa muda mrefu?

Harafu ni uwendawazimu kujenga miradi ambayo haina tija na hitumiki mfano Bandari karibu zote za Ziwa Tanganyika na baadhi ya Ziwa Victoria zimejengwa na zipo tuu hakuna kinachoendelea maana hakuna mzigo.

Like lijamaa liliharibu Sana nchi na bora lilivyowahi.Unaacha kuboresha uchumi Ili upate mapato unaharibu na kugombana na kila mtu si mfanyabiashara si jirani yaani ni shida.
 
Nimesikitika sana kusikia mikopo ilikopwa kwa masharti ya kibiashara na ya mda mfupi kiasi hicho huku huku Aliyekuwa Rais anadanganya.

Kiukweli Rais wa sasa alifaa awafute Kazi wapuuzi wote wa serikali iliyopita...
Hahaha, mkuu hapo kwenye kufuta wasaidizi wa Mwendazake itabidi ajifute na yeye pia (Maana alikuwa ni msaidizi wa mwendazake namba moja), Kifupi hakuna msaidizi aliyefurukuta mbele ya yule jamaa, aliwakamata na kuwanyongesha! Nadhani kwa sasa unaona waziri mkuu anafanya kazi ya waziri mkuu, na anaonesha furaha ya wazi kabisa na kujiamini!

Mawaziri wanatenda kazi zao bila kuingiliwa, wanaonesha vipaji vyao pia, kwa sasa wanaruhusiwa hata kusafiri nje ya nchi! Juzi Gwajima alikuwa Russia, January kwa wiki moja sasa yupo Saudi na UAE, Jafo yupo Saudi arabia sasa, February Rais ataambatana na akina Dotto james kwenda kwenye Expo Dubai!

1 La muhimu ni kuyafuta maujinga yote ya Mwendazake na kuimalizia hii miradi yake aliyoianzisha (Yeye alikuwa anaiita ya kimkakati, sijui mkakati gani huo, anajua yeye na Polepole wake)
 
We ni mpumbavu,miaka yote 6 mradi gani umeisha? Badala ya kugharamia hiyo miradi kwa mikopo nafuu na makusanyo unaenda Kukopa mikopo ya miaka 3 na riba kubwa huku miradi inakamilika kwa muda mrefu?...
Hadi hio miradi ikamilike ishachakaa unaanza tena kukopa Ili ukarabati.
 
"Ninajiuliza, hivi ilikuwa ni kwa faida ya nani Rais Magufuri na wapambe wake..........."Balile wewe ni mnafiki na si vinginevyo.
 
Aliponichekesha Balile ni kuwa alitoa tamko lililopelekea kuapishwa rais Samia..kwa hiyo asingetoa tamko rais asingeapishwa😂😂😂upuuzi kama huu ndio ulinifanya nikaacha kununua magazeti mda mrefu sana zaidi ya miaka 10 sasa
 
Tangu mwaka 1994 tulianza kudanganywa kuhusu makampuni ya kuzalisha umeme kina IPTL, DOWANS na wengineo pambio kemkem sofa za kufa mtu hakuna asiyejua tulifikishwa wapi,midomoni mwa mamba tuliingizwa tulilia Sana bila msaada wa mtu yeyote.

Hadi JPM alipoingia na kutunasua kwenye mtego tulip ingizwa na wanasiasa mmesahau meremeta, escrow na takataka kibao ya miradi ya kitapeli tuliyoingizwa na Wana siasa huko nyuma!

Leo eti mmepiga hatua ya kimaendeleo ya fikra mnasifia huo utopolo na kuponya maendeleo thabiti tunayoyashuhudia Lisa tu tunamchukia aliyeyahamasisha!
 
Watu wote wanaomsifia kichaa yule walaaniwe pia. Magufuli alipenda sifa kuliko nchi yake
 
Nilisha post humu kitambo sana, ni kwa nini sisi kama nchi tunafurahia sana kukopa na kulipa ni majanga? Ifikie wakati sisi kama nchi tuwe na mikakati na njia ya kuhakikisha tunakuwa self sufficeint kila kona...

hivi ndivyo walivyoanza nchi za Asia- kama Thailand , yaani kuwa self sufficeint kwanza kwenye chakula, barabara, huduma za afya, Kulipa madeni yao yote ya nje na ilianzishwa kodi maalumu ya kulipia madeni, yaani kwa mfano kila mtu atalipa Tsh 100 kila mwezi kulipa mikopo.

halafu tuwe na independent tax payers alliance ili kujua hiyo mikopo kama imetumika kama ilivyokusudia na kama malipo yanafanyika kama yavyotakiwa... sio hizi habari za tunakopesheka, halafu kulipa inakuwa kutafutana. Hii habari za Balile ni kama wamemtuma aje kupima upepo.
 
Mzee wakati wa Mwendazake hiyo tovuti ya BoT si ilikuwepo, mbona hukuitumia na kuleta taarifa kama hizi? Nakumbuka kuna wakati gazeti lako lilisifiwa hadharani na JPM kwa kuibua uozo sijui bandarini ama wapi lakini hili ambalo unasema linatutoa utumbo hukulisema. Leo ndio umeliona, kweli ya Mungu mengi.
Balile ni Yuda Iskariote
 
Naona namna nzuri ya kuchukua hatua za kupunguza hilo deni ni kupunguza mikopo tunayochukua hata kama inaitwa "rafiki" tena kwa kuifanyia mambo ambayo tumeshaambiwa yatafanywa kwa fedha za tozo.
...
Kuna Wakati ukimua kutumia akili zako huwa una maoni mazuri
 
Hadi hio miradi ikamilike ishachakaa unaanza tena kukopa Ili ukarabati.
Ni upuuzi wa Hali ya Juu.Mikopo ya kibiashara inakopwa na kuwekezwa kwenye miradi ya mda mfupi na yenye return ya haraka sio kama hao wapuuzi walivyofanya.
 
Back
Top Bottom