Balile: Magufuli katutenda, deni la nje lafikia shilingi Trillion 78

Balile: Magufuli katutenda, deni la nje lafikia shilingi Trillion 78

Tupe na thamani ya miradi iliyotokana na deni, kama uwiano wa deni na uchumi kukua ni 30% huko kutendwa kunatokeaje?

Anzia upanuzi wa bandari, SGR, Upanuzi wa highways, mabarabara ya mitaa, stand za mabasi nchi nzima, New mwendokasi roads, vituo vya afya nchi nzima, Hospitali za wilaya nchi nzima, Mashule, Ndege, upanuzi wa viwanja, ujenzi wa Dodoma plus Ikulu ya Chamino, usambazaji umeme kila kijiji, vivutio vya utalii, Hydropower ya Nyerere na vingine vingi. Ulitegemea hela haitumiki?

Then go back angalia uwiano wa uchumi na ukuaji wa madeni! Njoo kwenye probability means of return. Angalia makusanyo per annual sio kuandika kinafiki.
Jibu hoja zake kwanza.
1. Kwa nini alitudanganya kuwa hatukopi bali tunajenga kwa kodi zetu wenyewe?
2. Kwa nini alikopa mikopo yenye riba kubwa ya kibiashara?
 
Kuiva kwa deni maana yake muda wa kuanza kulipa deni lako na riba yake umefika. Haimaanishi kuwa hilo sasa ni deni jipya on top of that.

Na tunapocalculate deni la Taifa maana yake vitu vyote hivyo unavyovisema tumeshaviinclude ndani yake.

Kwa hiyo ukiambiwa mwaka 2005 Kikwete alikuta deni la Trillion 20, basi hilo ndo deni alilolikuta, akizembea kulipa linajiaccumulate, na hiyo accumulation inaongezwa kwenye deni, na kile atajachokopa yeye nacho kinaongezwa kwenye deni.

Kwa hiyo kama Magufuli alikuta deni la Trillion 42 mwaka 2015, basi ndo deni hilo alilokuta limeshainclude vyote (riba na mkopo wa JK), Sasa na yeye Magufuli kaavha deni la Trillion 70, maana yake kaongeza Trilion zake za kutosha tu kwenye deni alilokuta. Yeye kama rais ilibidi Alipe, hakuna excuse kuwa ni madeni ya watangulizi wangu. Kwani Mkapa, JK hawakuwa na watangulizi?, Mbona wao rate ya ukuaji wa deni haikuwa kama ya Magufuli?
Nimewaza nikujibu nini,nikaona nikuache na upumbavu uliorithi kwa bibi yako!
 
Ni aheri deni lipae ila vitu viwe vinaonekana wazi, hebu tunakanyaga lami za kueleweka na barabara za kiwango cha zege mpaka mitaani! Wakati unalalamika kutendwa na Magufuli mkoonduh wako unapepea kuelekea ulipojenga Mbezi Kibanda Cha mkaa kupitia barabara 8 za lami huku ukipaa toka kwenye kijazi interchange.

Je, unakumbuka ni kero kiasi gani ulizipata kwa kukaa masaa zaidi ya 2 kuvuka tu eneo la Ubungo maziwa mpaka ubungo maji tokana na msuko suko wa magari?
🤣
 
In case you don’t know ni serikali ya Mozambique ndio waliomba London waingilie kati sakata lote, taasisi yao kuchukua government guarantee loan bila ya serikali kujua.

London tena? We si umesema IMF na World Bank?!!

Au baada ya kukuambia wahusika ni UK, US na Swiss Financial Regulators ndo ukaamua kwenda ku-Google kuja kunipa "darasa"?

And guess what... in case you don't know, hicho ulichoongea hakina ukweli wowote!!
 
Mikopo yooote ya JPM tunajua ilifanya nini nakila mtanzania anaiona na iliyokamilika anaifaidi. Tunasubiri isiyokamilika kama JKN Hydro dam ikamilike mwezi ujao. (ingawa kwa huyu mama na akina January wake-nina mashaka!)
Unaweza kunitajia hapa hiyo iliyokamilika ambayo ni matunda ya JPM?!
 
Mzee wakati wa Mwendazake hiyo tovuti ya BoT si ilikuwepo, mbona hukuitumia na kuleta taarifa kama hizi? Nakumbuka kuna wakati gazeti lako lilisifiwa hadharani na JPM kwa kuibua uozo sijui bandarini ama wapi lakini hili ambalo unasema linatutoa utumbo hukulisema. Leo ndio umeliona, kweli ya Mungu mengi.
Afadhali kuchelewa kuliko kutokufika kabisa, kwa maana nyingine afadhali ametueleza sasa kuliko kukaa kimya kabisa
 
London tena? We si umesema IMF na World Bank?!!

Au baada ya kukuambia wahusika ni UK, US na Swiss Financial Regulators ndo ukaamua kwenda ku-Google kuja kunipa "darasa"?

And guess what... in case you don't know, hicho ulichoongea hakina ukweli wowote!!
Will be back in two hours, soma tena extended post.

Ungekuwa unafahamu masharti ya IMF na WB, pertaining DSA (Debt Sustainability Analysis) na frameworks zingine kabla ya kukopesha nchi maskini; ndio ungeelewa misingi ya hiyo ruling na makosa ya Credit Suisse.

Kuna commitment hapa za kutimiza first, laters.
 
Mzee wakati wa Mwendazake hiyo tovuti ya BoT si ilikuwepo, mbona hukuitumia na kuleta taarifa kama hizi? Nakumbuka kuna wakati gazeti lako lilisifiwa hadharani na JPM kwa kuibua uozo sijui bandarini ama wapi lakini hili ambalo unasema linatutoa utumbo hukulisema. Leo ndio umeliona, kweli ya Mungu mengi.
Kwa hiyo ulitaka anyamaze ili wewe useme au? Kwa kuamua kuwajulisha watanzania wenzake hali halisi ya uchumi na changamoto za viongozi wetu wewe inakuuma nini hasa?? Watanzania wengi, ikiwemo wewe pengine ni wavivu sana wa kusoma vitu, mwenzetu ameingia tovuti ya BOT since 2000 to date na kutuwekea ugali ulioiva na nyama choma mezani sisi kazi yetu ni kula tuu, bado wewe unakereka daaah kweli bongo bahati mbaya aisee [emoji119][emoji119]
 
Tupe na thamani ya miradi iliyotokana na deni, kama uwiano wa deni na uchumi kukua ni 30% huko kutendwa kunatokeaje?

Anzia upanuzi wa bandari, SGR, Upanuzi wa highways, mabarabara ya mitaa, stand za mabasi nchi nzima, New mwendokasi roads, vituo vya afya nchi nzima, Hospitali za wilaya nchi nzima, Mashule, Ndege, upanuzi wa viwanja, ujenzi wa Dodoma plus Ikulu ya Chamino, usambazaji umeme kila kijiji, vivutio vya utalii, Hydropower ya Nyerere na vingine vingi. Ulitegemea hela haitumiki?

Then go back angalia uwiano wa uchumi na ukuaji wa madeni! Njoo kwenye probability means of return. Angalia makusanyo per annual sio kuandika kinafiki.
Yeye kafanya wajibu wake, hilo na wewe si ulifanya tatizo liko wapi hapo? Au ndo yale yale ya mimi mjuaji huku waungua na jua?
 
1.Mama yako alikudanganya mara ngapi ukavae viatu anakusubiri nje na hukumkuta ulipotoka? Japo ulilia sana je, uliwahi kumsema wapi?

2.Mkopo ni mkopo na riba ndo utaratibu wake, inategemea na urgency ya hela! Ukitaka upewe hela za haraka lazma ulipe riba kubwa unless ukakope falme za kiarabu ambako hawana riba!
Jibu hoja zake kwanza.
1. Kwa nini alitudanganya kuwa hatukopi bali tunajenga kwa kodi zetu wenyewe?
2. Kwa nini alikopa mikopo yenye riba kubwa ya kibiashara?
 
Nafikiri alikopa kulingana pia na uwezo wa nchi! Unajua ukuaji wa uchumi ndo uwezo wa kukopesheka pia! Na utambue miaka yote tumekopa lakini kilichokuwa kinafanyika cha maana hakikuwepo! Ila kwa vile wote mmegeuka wakosoaji wa Magufuli ili kumlinda mama! Mwambie apambane asisingizie Madeni hata Marekani wana madeni ya kutisha!
Jibu hoja, kwa nini akope kwenye mabenki ya biashara yenye riba za 6 % na zaidi? Kwa nini kukopa ilikuwa ni siri yake mwenyewe? Rais SSH ameweka wazi matumizi yoooteee ya mkopo wa juzi wa Trilioni 1.3 yaani kila mtanzania anajua, sasa ni kipi kilimfanya mwendazake kila kitu kiwe ni siri yake??
 
Kwani deni linalipwa na pesa za nje?

Ni msaada tu ndio huwa za nje, borrowed zote ni za ndani. Unachanga unalipa... ukikamilisha mradi ni wako.

We ukikopa ukajenga nyumba then ukikamilisha mkopo ni bank imekujengea au we mwenyewe?
You missed the point... Alisema fedha za ndani kwa maana kwamba hatujakopa na mara kwa mara alisikika akisema sisi ni matajiri.
 
Wewe Balile acha unafiki! Mama kakopa hela ya UVICO na ile miradi ni kudanyanya wananchi ili waone anafanya kazi! Nambie sasa miezi sita angalia mwenendo wa miradi inavyosuasua mfano, Ujenzi wa barabara nyingi unasuasua hata mwendo kasi Dar bila shaka unaona, ujenzi wa madaraja makubwa kama Mto wami na Busisi!

Kwa ujumla hakuna jipya! Huo mkopo unaodai ukweli na uwazi ni mkopo wa Corona na kwa taarifa yako pamoja na tozozote ila mapato yamepungua ila kwenye media mnaambia anakusanya trilion karibia mbili kwa mwezì!
Kwa nini miradi inasuasua wakati mwendazake alikopa Trilioni 29 in five years period? Mama SSH hiyo miradi kaikuta, sasa tuambie wewe hizo 29 Trilioni zilizokopwa kwenye commercial banks zimefanya kazi zipi na zipi?
 
Magufuli katutenda deni la taifa, trilioni 78 Samia msalabani

Jamhuri October 26, 2021

Na Deodatus Balile

Kazi hii ya uandishi wa habari moja ya majukumu yake ni kuanika ukweli minong’ono inapotawala katika jamii.

Kwa sasa kuna minong’ono mingi. Minong’ono imeanza baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kutangaza hadharani mkopo wa Sh trilioni 1.3, alioukopa kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na akatangaza miradi lukuki itakayotekelezwa kwa kutumia mkopo huo.

Miongoni mwa miradi ya kihistoria ni ujenzi wa madarasa ya sekondari 15,000 nchi nzima na madarasa ya shule za msingi 3,000.

Kwa sasa inakadiriwa kuwa nchi ina upungufu wa madarasa 11,000, lakini Rais Samia ameamua kuona mbali.

Ameamua kufuta mfumo wa zima moto, ambapo kila mwaka wazazi wanakabwa koo vijijini kuchangia ujenzi wa madarasa.

Baadhi ya wazazi pia wameanza minong’ono kuwa watoto wao wamepewa mikopo kidogo, yaani Sh 600,000 kama ada vyuoni.

Hawajui kuwa miaka yote imekuwa hivyo na wakati mwingine wengi wanakuwa hawapati kabisa hata senti tano ya mkopo.

Sitanii, naomba nizungumzie kwa ufupi miezi sita ya Rais Samia akiwa Rais wa Tanzania baada ya kuapishwa Machi 19, 2021.

Nakumbuka vema kilichotokea, maana baada ya kifo cha Rais John Magufuli kulitokea kama sintofahamu hivi.
Wapo watu walioamini Rais Samia angeendelea kuwa Kaimu Rais, baadhi walidhani tunakwenda kwenye uchaguzi mpya na wengine hawakufahamu nini kitatokea.

Asubuhi ya Machi 18, 2021 niliamkia studio za Televisheni ya Taifa (TBC1) na TBC Taifa (radio) kufanya mahojiano na Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Dk. Ayub Rioba.

Hii ilikuwa ni baada ya kifo cha Rais John Magufuli, kilichotokea Machi 17, 2021. Ikumbukwe wiki moja kabla nilikuwa nimefanya mahojiano na kituo cha Star TV nikasema tuambiwe bayana Rais Magufuli yuko wapi na anafanya nini.

Machi 18 pamoja na kwamba nilikuwa bado Kaimu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), ambapo baadaye nilichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa TEF Mei 22, 2021, ilinilazimu kutoa ufafanuzi huo uliokuwa tamko zito.

Sitanii, tamko nililolitoa lilizaa kuapishwa kwa Rais Samia kuwa Rais wa Awamu ya Sita Machi 19, 2021. Nilirejea Katiba ya Tanzania (1977) Ibara ya 37(5) inayosema: “Endapo kiti cha Rais kitakuwa wazi kutokana na Rais kufariki dunia, kujiuzulu, kupoteza sifa za uchaguzi au kutomudu kazi zake kutokana na maradhi ya mwili au kushindwa kutekeleza kazi na shughuli za Rais, basi Makamu wa Rais ataapishwa na atakuwa Rais kwa muda uliobaki katika kipindi cha miaka mitano na kwa masharti yaliyoelezwa katika ibara ya 40, kisha baada ya kushauriana na chama cha siasa anachotoka Rais atapendekeza jina la mtu atakayekuwa Makamu wa Rais na uteuzi huo utathibitishwa na Bunge kwa kura zisizopungua asilimia hamsini ya wabunge wote.”

Kwa mara ya kwanza kupitia makala hii ninakisema kilichotokea baada ya tamko hilo. Walinipigia simu watu wengi wakiwa na hofu.

Baadhi hawakufahamu Katiba inasemaje. Walinishutumu wakidai nimetangaza utaratibu wa kwangu, kwani baada ya kifo cha Rais kinachofuata ni uchaguzi.

Hii ilinipa shida kuona hata baadhi ya wabunge hawakufahamu nini kinafuata baada ya kifo hicho. Machi 18, 2021 itabaki kuwa siku ya kihistoria kwangu, kwani ujumbe nilioutoa ulitangazwa katika radio zote za ndani na za kimataifa na siku moja baadaye Rais Samia akaapishwa.

Sitanii, leo ninazungumzia mzigo wa madeni ambao Rais Magufuli amelitwisha taifa letu. Nimetangulia kusema na ninarudia, mimi ni msema kweli. Wala sipepesi macho katika kusema ukweli.

Wakati Rais Magufuli kwa miaka mitano yote alikuwa anawaaminisha Watanzania kuwa nchi inajenga miundombinu na inanunua ndege kwa kutumia fedha zetu wenyewe, uhalisia ni kinyume chake.

Kwa kipindi cha miaka mitano tu, Rais Mafuguli amekopa fedha nyingi kuliko fedha zote alizokopa Rais Benjamin Mkapa kwa miaka 10 aliyokaa madarakani.

Kwa miaka mitano, amekopa pia fedha nyingi kuliko alizokopa Rais Jakaya Kikwete kwa miaka 10 naye aliyokaa madarakani.

Rais Mkapa alirithi madeni mengi mno. Alipambana nayo, akaiingiza nchi katika Mpango wa Kusamehe Madeni Nchi Maskini (HIPC) na hadi anatoka madarakani, Tanzania ilikuwa inadaiwa Sh trilioni 20 tu.

Rais Kikwete wakati wake deni la taifa liliongezeka kwa Sh trilioni 23, hivyo akatoka madarakani deni la taifa likiwa Sh trilioni 43 kwa miaka 10. Rais Magufuli kwa miaka mitano tu, deni la taifa limeongezeka kwa Sh trilioni 29 na kufikia Sh trilioni 72 hadi anafariki dunia Machi, 2021.

Sitanii, kwa kasi hii ya ukopaji ina maana kama angekaa madarakani kwa miaka 10 kamili na akaendelea na kasi ya ukopaji wa wastani wa Sh trilioni 29 kwa miaka mitano, basi angetoka madarakani deni la taifa likiwa Sh trilioni 101 kufikia mwaka 2025.

Kuna jambo baya halisemwi. Rais Magufuli amekopa mikopo ya kibiashara inayoanza kulipwa baada ya miaka mitatu na inapaswa kulipwa ndani ya miaka minane, ikiwa na riba za kati ya asilimia 6 na 8.

Baadhi ya mikopo hii imeiva tayari. Imeanza kukuza deni la taifa kwa kasi kutokana na riba. Deni la taifa sasa limefikia Sh trilioni 78.

Kwa vyovyote vile iwavyo, Rais Samia anapaswa kuchukua hatua za haraka, ikiwamo kuunda timu ya majadiliano na wakopeshaji kwa ajili ya kubadili masharti ya mikopo ya kibiashara aliyochukua Rais Magufuli.

Anapaswa kuomba msamaha wa riba na pengine kuomba kuongezewa muda wa kulipa deni kama ulivyo utaratibu wa mikopo kwa serikali nyingi duniani.

Mikopo mingi kwa serikali huwa inalipwa kati ya miaka 20 hadi 50 kulingana na ukubwa wa mkopo na hutozwa riba kati ya asilimia 0.3 hadi asilimia 1. Mikopo ya aina hii inapatikana katika Benki ya Dunia, Shirika la Maendeleo Duniani, Benki ya Maendeleo Afika na nyingine za aina hii.

Kwa bahati mbaya na kwa masikitiko makubwa, kwa miaka mitano Wazungu tuliowaita mabeberu, ila tukawa tunakopa fedha zao kupitia benki za biashara. Kwa hali halisi, madeni haya yakiiva yote, ikiwa hakuna majadiliano ya dharura kuomba marekebisho ya masharti ya mikopo tuliyochukua chini ya Rais Magufuli, itafika mahala asilimia 60 ya bajeti ya taifa letu itakuwa inakwenda kulipa madeni. Waliomo serikalini watajua la kufanya katika hili.

Sitanii, ninafahamu baadhi ya wasomaji watakuwa wanaanza kufuka moshi kwa kusema ukweli huu. Wanajiuliza taarifa hizi nimezipata wapi? Taarifa hizi si za siri. Ziko wazi kwenye tovuti ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Nimepitia taarifa za mapitio ya mwenendo wa uchumi tangu mwaka 2000 hadi 2021. Zipo mtandaoni na zinaonyesha deni lilivyokua hatua kwa hatua. Kwa nia ya kuweka uelewa unaofanana, ifuatayo ni hali ya deni la taifa tangu mwaka 2005 hadi 2021.

Oktoba 2005, deni la nje lilikuwa USD milioni 8,361.9 sawa na Sh 19,286,471,493,000 na deni la ndani lilikuwa Sh 1,712,800,000,000. Jumla kuu ya deni wakati Rais Mkapa anaondoka madarakani lilikuwa Sh 20,999,271,493,000 (Sh trilioni 20.9). Nimekokotoa hesabu hizi kwa kutumia viwango vya BoT vya kuuza dola ya Marekani ambavyo ni USD 1 kwa Sh 2,306.47.

Oktoba 2015, wakati Rais Kikwete anatoka madarakani deni la nje lilikuwa USD milioni 15,321.3, sawa na Sh 35,338,118,811,000 na deni la ndani lilikuwa Sh 7,826,200,000,000. Jumla kuu deni la nje na deni la ndani lilikuwa ni Sh 43,164,318,811,000 (Sh trilioni 43.1).

Deni la taifa lilianza kupanda kwa kasi Oktoba 2016. Deni la nje lilipanda na kuwa USD milioni 16,407.6 sawa na Sh 37,843,637,172,000, huku deni la ndani nalo likipanda na kuwa Sh 10,089,000,000,000. Jumla kuu ya deni ikafikia Sh 47,932,637,172,000 (Sh trilioni 47.9).

Oktoba 2017 deni la nje lilipanda kwa kasi kubwa na kufikia USD milioni 19,074.4 sawa na Sh 43,994,531,368,000. Kutokana na makandarasi kutolipwa deni la ndani nalo lilikua na kufikia Sh 12,563,300,000,000. Jumla kuu ya deni kwa mwaka huo likawa Sh 56,557,831,368,000 (Sh trilioni 56.5).

Oktoba 2018, deni la nje lilizidi kupanda na kuwa USD milioni 20,759.1 sawa na Sh 47,880,241,377,000, huku deni la ndani nalo likipanda na kuwa Sh 14,116,100,000,000. Jumla kuu ikawa Sh 61,996,341,377,000 (Sh trilioni 61.9).

Oktoba 2019, mwanamume aliongeza tena deni la taifa, deni la nje likafikia USD milioni 22,569.4, sawa na Sh 52,055,644,018,000, huku deni la ndani likipanda na kufikia Sh 14,187,400,000,000. Jumla kuu ya deni ikafikia Sh 66,243,044,018,000 (Sh trilioni 66.2).

Oktoba 2020, deni la nje lilipanda na kufikia USD milioni 23,599.3, sawa na Sh 54,431,077,471,000, huku deni la ndani likifikia Sh 15,608,500,000,000. Jumla kuu ikafikia Sh 70,039,577,471,000 (Sh trilioni 70).

Machi, 2021 wakati Rais Magufuli anafariki dunia, deni la nje la Tanzania lilikuwa limefikia USD milioni 24,429.2, sawa na Sh 56,345,216,924,000. Deni la ndani nalo lilipanda na kufikia Sh 16,116,500,000,000. Jumla kuu, deni la taifa lilifikia 72,461,716,924,000 (Sh trilioni 72.4).

Kilichofuata baada ya hapo, madeni yameanza kuiva kwa ajili ya kulipwa, huku mengine yakizalisha riba ya kufa mtu.

Makandarasi wengi Tanzania wanadai mabilioni kati ya hizo Sh trilioni 16 ambazo ni deni la ndani hawajalipwa siku nyingi. Kutokana na hali hiyo, madeni haya yaliyokopwa bila mpangilio katika benki za biashara yameanza kuwa msalaba kwa Rais Samia.

Taarifa ya hali ya Uchumi ya BoT ya Septemba, 2021 inayorejea mwezi Agosti, 2021 kutokana na mazingira hayo, deni la nje limekua na kufikia USD milioni 25,956.1 sawa na Sh 59,866,965,967,000, huku deni la ndani nalo likikua na kufikia Sh 18,225,000,000,000. Ukuaji huu unafanya kiwango cha deni la taifa kufikia jumla kuu ya Sh 78,091,965,967,000 (trilioni 78).

Sitanii, deni hili likigawanywa kwa Watanzania milioni 60, bila kujali mkubwa na mdogo, kila Mtanzania anadaiwa Sh 1,301,533 (Sh milioni 1.3). Hata hivyo, wataalamu wa uchumi wanasema deni hili si tishio kwa uchumi wa taifa letu kwa sasa kwani liko katika uwiano wa asilimia 30 kwa uchumi wa taifa letu, wakati kuna mataifa Afrika ambayo tayari yana uwiano wa asilimia 54 ya deni kwa uchumi wa nchi zao, ila wanaionya serikali iepuke mikopo ya kibiashara ina riba kubwa, masharti mabaya na inalipwa kwa muda mfupi.

Pale Dodoma, tumeona Rais Samia ameanzisha utaratibu mpya wa ukweli na uwazi katika mikopo. Ameeleza fedha alizokopa zitafanya nini kwa kuorodhesha miradi itakayotekelezwa na akatueleza amezikopa kutoka wapi.

Ninajiuliza, hivi ilikuwa ni kwa faida ya nani Rais Magufuli na wapambe wake kuficha ukweli kuwa miradi ya reli, barabara, umeme, ujenzi wa hospitali na mingine mingi aliyoijenga alikuwa anakopa?

Hivi sisi kama tungejua anakopa, tungemzuia? Lakini si tungepata fursa ya kumshauri asichukue mikopo ya kibiashara inayoanza kututoa utumbo sasa? Mungu ibariki Tanzania.

Copyright ©2021. Gazeti la Jamhuri
Balile ameniacha hoi: Hivi ni kweli hata Mwanasheria Mkuu wa Serikali alikuwa hajui kama baada ya kifo cha JPM katiba inaelekeza Samia, yaani Makamu wa Rais ndiye alipaswa kuapishwa kuwa Rais mpaka yeye alipohojiwa TBC sijui na wapi?
 
Walinda legacy wamechachamaa! [emoji16][emoji16][emoji16]

Magufuli alikuwa anakopa utadhani hakuna kesho!

Aina ya mikopo aliyokuwa akichukua Magufuli siyo ya masharti nafuu ni kitanzi kitupu!

Kwan hilo deni lililokuepo kabla hajaingia lilisababishwa na nn !! S atleast maguful tunaona na vitu vilivofanyka!mtutolee utopolo
 
Will be back in two hours, soma tena extended post.

Ungekuwa unafahamu masharti ya IMF na WB, pertaining DSA (Debt Sustainability Analysis) na frameworks zingine kabla ya kukopesha nchi maskini; ndio ungeelewa misingi ya hiyo ruling na makosa ya Credit Suisse.

Kuna commitment hapa za kutimiza first, laters.
Acha mbwembwe...

Ungekuwa unafahamu basi ungeonesha ufahamu wako from the very first post!!

Nimekukosoa kwa jambo la wazi kabisa ndo unataka kuleta habari za masharti ya IMF...

Ni yupi unayetarajia kumdanganya kwamba masharti ya IMF ni mabaya zaidi kulinganisha na yale ya benki zilizo sekta binafsi?!
 
And alikuwa anakopa kwa siri as if hiyo hela angelipa kutoka mifukoni mwake, akiwa majukwaani anawatukana mabeberu, Usiku anawapigia simu kuwakopa hela!! Trl 29 kwa miaka 5 ni nyingi sana, and sijui kafanyia nini hiyo hela, maana mamiradi yake yote yapo under 50% ya utekelezaji

We ndo utueleezee vizuri unadhan imeenda wap!! Maana transaction zote za serikali n documented!! Kama unadhan kuna upotevu wa hela n sh ngap
 
Shida ya Magufuli alipenda pesa ya wazungu lakini masharti alikuwa hayapendi, ndio maana akaangukia kwenye mikopo umiza. Serikali inakopaje mikopo ya muda mfupi hivyo tena kwa riba ya 8%??

Huko alikoenda kama kuna kufa tena, afe tu again.

Ndiyo maana watu wanalilia KATIBA iliyojitosheleza!!! Haya mambo yasingetokea kama Bunge letu lilikuwa sio la mazuzu.
If we had strong institutions these poor decisions that Magufuli made would have been nipped in the bud!
 
Back
Top Bottom