Balile: Magufuli katutenda, deni la nje lafikia shilingi Trillion 78

SukumaGang katika ubora!!!
 
Huu uzi ni mzuri kwa maslahi mapana ya taifa ila naona umegeuzwa kuwa battle kati ya watetea legacy vs waponda legacy
Kutetea legacy na kuponda legacy kwa hoja ni afya kwa taifa.
Kila mmoja anaponda au kutetea kwa maslahi ya nchi.
Kama unadhani mwendazake amekosea mahali, weka vitu hapa watanzania waone na wengine wajifunze.
Kama unaamini amefanya mazuri kwa faida ya nchi dondosha ushahidi tuone.
Naona mjadala unaenda vema kwa maslahi ya taifa
 
Reactions: Ame
Majibu yake ni marahisi.
Mabenki ya biashara hayana masharti magumu kama ilivyo IMF na WB.
IMF na WB wanaweza kukukopesha lkn wanakupa masharti magumu kama vile kufutilia mbali baadhi ya taasisi za umma.
Kukuelekeza miradi ya kufanyia fedha wanayokukopesha, watakuambia usiajiri kwa miaka kadhaa, watakuambia ongeza kodi katika eneo na samehe kodi katika eneo hili.
Yaani ni vurugu tupu. Unakuwa unaendeshwa kama mashine.
 
Mikopo haijawahi kuwa siri. Ndio maana hata mwandishi amesema inapatikana tovuti ya Benki Kuu ya Tanzania. Nadhani mahali pengine unapoweza kupata ni Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS) na Wizara ya Fedha kwenye Hotuba za Waziri wa Fedha za bajeti na za hali ya uchumi.
Lakini hata kauli za JPM zilikuwa kwamba hata fedha za mikopo ni za kwetu kwa sababu zitalipwa kwa kodi za Watanzania.
 
Uongo kwa kuniwekea maneno yako. Unakuja na story ambazo unataka nizijibu vitu ambavyo sijaongea.
Maneno umeongea mwenyewe halafu unasema nimekuwekea maneno?

Toa mfano MMOJA TU wa hayo maneno niliyokuwekea...

NI wewe mwenyewe ndie umesmema kwamba:-
Hivi unadhani mabeberu ata kwa kupitia private banks yanakopesha nchi maskini bila ya IMF na WB kufanya stress test kama unaweza kulipa madeni yako huko mbele based on your tax collections.
Yaani hapo unataka kudanganya LIVE kwamba hata private banks za kibeberu haziwezi kukopesha nchi maskini bila approval ya IMF....

Ukaendelea kwamba:-
Kwanza hiyo 200M sio kwamba walilazimishwa...

Narudia... chanzo cha sakata hili sio IMF kama unavyojaribu kuaminisha watu bali financial regulators wa US, UK na Uswisi. Baada ya wao kufanya uchunguzi, ndipo wakagundua violation of money laundering control na massive corruption!

Hiyo 200M uliyoitaja bila kufahamu undani wake, inahusishwa na settlement ya corruption kwa sababu, uchunguzi ulithibitisha maofisa wa benki kuweka kibindoni zaidi ya USD 50 Million na Wafanyakazi wa Serikali ya Msumbiji na wenyewe waliweka kibindoni zaidi ya USD 130M!

Ingawaje hizo pesa zililipwa na benki husika, lakini burden yake ilienda kwa serikali kwa sababu inakuwa cost of loan!! Ni kutokana na hilo, ndo maana Credit Suisse wakaji-commit kufuta mkopo kwa USD 200M kama compensation ya pesa iliyoingia mifukoni mwa watu lakini burden inahamia kwa serikali ya Msumbiji!
Narudia... SIO KWELI

Issue sio Credit Suisse kukopesha bila idhini!!

Private banks hawahitaji idhini ya IMF ili kukopesha nchi!

Uhusika wa IMF kwa muktadha unaoeleza, ni kama ulivyo kwa any Creditor to her Debtor!!

Kwamba, taifa kama Msumbiji linapotaka mkopo toka popote pale, Lender atataka kufahamu financial status ya mkopaji, hii ikiwa ni pamoja na madeni aliyonayo na creditors wengine. Ni kutokana na hilo, ndo maana wengine wanakuwa na Credit Bureau!!

Sasa issue ya Msumbiji na IMF ilikuja wakati financial regulators niliowataja wakiendelea na uchunguzi wao dhidi ya Credit Suisse vs Mozambique! Hapo ndipo serikali ya Msumbiji ikazungumzia suala la guarantee waliyoweka kwenye mkopo MWINGINE toka kwa Credit Suisse!!

Hapo ndipo IMF wakafahamu kwamba kumbe kuna mkopo mwingine ambao wao walikuwa hawajui wakati walikuwa katika process za kutoa mkopo "mwingine" kwa Mozambique... hapo ndipo waka-cancel huo mkopo!!!

Kwahiyo ni issue ya IMF vs Serikali ya Msumbiji na sio IMF vs Credit Suisse!!!
Sasa kuelezea hizo stress taste zinahusu ni mlolongo mrefu ndio maana kila nchi ina DMO ya kufanya hiyo kazi. Hiki ndio nilichosema mimi.
Hayo uliyasema baadae baada kuweka wazi maelezo yasiyo sahihi uliyokuwa umetoa mwanzoni!!
Sasa wewe unataka ni entertain mawazo yako na maswali yasiyo na msingi
Kama hayana msingi mbona umeshindwa kujibu?! Nimekuuliza swali jepesi sana hapo juu, kwahiyo ningependa kurudia hapa...

TAJA MFANO MMOJA TU wa maneno niliyokuwekea!!
sijui ina maana private lending ni rahisi kukopa kushinda IMF na WB ndio nilichoandika hiko.
Hapo ulikuwa unajaribu kusema nini?!
Besides if you do not know ata hela wanazotoa IMF na WD asilimia kubwa ni za private banks; sema zinakuwa channeled through them ili ku control mikopo ya nchi na kuminimise risk za default.
We bhana acha kujifanya unajua sana wakati hakuna unachojua...

Hivi unajua IMF wanaingiza dola billion ngapi kupitia contribution quota?!

Hivi umeshawahi kuona Quota Formular inayotumika kuchangia?!

Hivi mataifa kama US yanavyoiletea jeuri UN unadhani ni kwa sababu HQ ya UN ipo Marekani?

Acha kuongea vitu usivyovijua wewe

Halafu unashindwa hata kutumia common sense!!

Yaani IMF waweze ku-control mikopo na ku-minimize default risks kushinda private banks zenyewe?!!

Hivi akina Nyerere waliokuwa wanavimba waziwazi kwamba "...madeni yenu hayalipiki, na kwahiyo hatutalipa".... hivi unadhani mkopeshaji angekuwa ni Private Bank akina Nyerere wangeongea kwa tambo namna hiyo?!
Hilo nishaeleza hapo juu... ACHA KUCHANGANYA MADESA...

Btw, mbona hujaweka hiyo link?! Au huyo screenshot ndo unaita link?
 
Kauli za kitapeli hizi, kwahiyo Marais waliopita walikuwa wanadanganya watu kama yeye mwendakuzimu?
 
Wale wajinga wenye akili kama punje ya sukari..watakuja hapa kupinga na kutetea ujinga uliofanywa na malaika muovu
 
Watu hawataki kusikia haya...Wapo tu kuwaza yao ya kisiasa....
 
Nadhani upo Ubelgiji. Utakaporudi tafuta mtu wa kukupitisha pale mataa usije ukapotea.
Kumbuka nimesema mradi ambao ni "matunda ya JPM"!!

Hapo mataa ni wapi?! Kama ni Ubungo, na kwavile wengi reference yenu ni interchange... ule ni mradi wa BRT!!

Mnaona imejengwa wakati wa JPM kwa sababu, mwanzoni BRT Design ilihusisha kuweka traffic lights tu pale makutano! Hata hivyo, mabasi ya BRT ndiyo yalikuwa yamependelewa kwenye plan ile, kwa maana, gari zingine ZOOOTE hazikutakiwa kupinda kulia wakishafika pale mataa!

Kwa mfano, kama gari inatoka Buguruni na inaenda town, ilitakiwa ikifika mataa, wale kushoto kama wanaenda Kimara kisha huko mbele wakapige U-turn na kushika lane ya kwenda town!

In 2013, TANROAD wakaona wamechemka kwa hiyo design kwa sababu ingeleta balaa(congestion) kubwa sana pale Ubungo Mataa.

Kutokana na hilo, TANROADS wakaamua kuandaa design na proposal nyingine ambayo waliwasilisha kwa JK. Sasa kwavile World Bank ndio financier wa BRT, kama kawaida yake ya kutochoka kujikomba, JK akaagiza warudi tena World Bank; na World Bank wakakubali ku-finance ujenzi wa interchange baada ya kukubaliana na hoja zilizotolewa!

Sasa kazi kubwa afanye mwingine, credit aje kupewa mwingine?! Mbona Samia anavyotoa pesa kwa ajili ya SGR na Nyerere Dams, mbona hamumpi credit zake lakini zote zinaenda kwa JPM?

Kwa sababu ukweli ni kwamba, ni JPM ndie ana-deserve hizo credits kwa sababu ndie kafanya kazi kubwa kuhakikisha miradi hiyo inasimama!!! Hata mkataba wa juzi wa kununua ndege zingine (kwangu naona ni jambo la ovyo, except kwa ndege ya mizigo), bado credit zinaenda kwa JPM kwa sababu ndie alihakikisha suala hilo linafanyika!
 
I knew it, lile zee lilikuwa baba la uongo, ona sasa linaumbuka.
Yaani Magu sikuwahi kabisa kumuamini, na mara zote niliamini sijawahi kuingia king na uongo wake wowote ule ... kumbe nilikuwa najidanganya aisee!!!

Pamoja na kufuatilia kwangu kote kwa haya mambo, Magu aliniamnisha kabisa kwamba ndege zimenunuliwa cash kwa pesa zetu!!

Juzi nasoma ripoti ya PAC ndo nakuja kushangaa ndege nazo ni mkopo wa zaidi ya Sh 800 Billion... NIKACHOKA!!
 
Mungu ameliokowa hili Taifa bila umwagaji damu, tunapaswa kumpa Mungu shukrani.

Kama Watanzania tunashindwa kumwambia Mungu asante kwa kutuondolea kiumbe katili alijejipachika mamlaka ya umungu mtu basi nchi yetu haitobalikiwa.

Mimi ndio maana sina tatizo na huyu mama naona wanasiasa wanamwingia kwa wrong timing tu, lakini mwendakuzimu alikuwa ni shetani, mpenda sifa na wengine waonekane si lolote si chochote.
 
Huyu Balile anatumika kumsafisha Samia,unaweza kuona uandishi wake,hawa waandishi ndo maana Mkapa alikuwa anawatukana
 
Tatizo la kila moja wenu ni kuhangaika na personalities za watu na upambe ambo wengi ni nuksi na sababu kubwa ya viongozi kuchukiwa na raia...Kwanini mnapambanisha marais?

JK awamu yake iliisha ambapo wote JPM na Mama Samia walikuwa sehemu ya awamu hiyo...Tatizo ni ninyi wapambe, acheni kujitoa akili...Tanzania ni ya sisi sote...Na mtu akisifiwa haiondoi sifa ya mwingine...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…