Balile: Magufuli katutenda, deni la nje lafikia shilingi Trillion 78

Nchi bora iuzwe kila mtu achukue chake ujinga na ushabiki mandazi umezodi
 
Dhana ya kuminya Uhuru wahabari utoaji takwimu ilikua kwajili ya Hilo na sivinginevyo uchaguzi 2015 uliimaliza ccm
 
Unaumilia maumivu kutokea pande zipi za dunia?!

Hakuna nilipopambanisha mtu, unalilia kwamba napambanisha marais... je, nikipambanisha?!

Na hivi nilivyokuwa na database ya facts si ndo utazidi kuumia!!
 
Hata kama watu wanajifanya hawaoni lakini ukweli ndo huo... tulikuwa tunaelekea pabaya!!

Mara zote niliamini JK ndo rais msaanii zaidi kuwahi kutokea Tanzania, na asingetokea mwingine zaidi yake! Baada ya kuja JPM, ndo nikaja kugundua kwa usanii, JK cha mtoto!!

Na zile gia zake za kujifanya ana uchungu na wanyonge, basi akawageuza wengi kuwa ndondocha wake wa kuamini kila anachowaambia!!!

Eti kuna wengine wanatoa povu hata kwa hii habari ya Balile wakati Balile katumia takwimu za hiyo hiyo serikali lakini HAWATAKI... wanachukulia mambo yote too personal!!! Hapo wanaona ni chuki tu bila kuangalia facts zilizotolewa
 
wenye akili tunajua mchawi hapa ni ccm hii mideni itatua kabla ya muda wetu
 
wenye akili tunajua mchawi hapa ni ccm hii mideni itatua kabla ya muda wetu
Na mbaya zaidi... hili ni trela tu!!

Mradi wa SGR bado sana!! Kwahiyo tutaendelea kukopa maradufu kwa ajili ya SGR!!!

Hata Bwawa la Nyerere, bado!!! Kwahiyo tutaendelea kukopa kwa ajili ya kuendelea na ujenzi!!

Na kwavile kote huko tunatumia mikopo ya kibiashara... it's a matter of time kabla hatujaanza kutafutana!!!
 
Kwani yeye ni mpumbavu. Ulitaka ajipige Risasi mwenyewe. Wakati wa Magufuli nani alikuwa jasiri mbele ya kifo
 
Anatafuta teuzi kwa nguvu, anasema kazi ya uandishi wa habari ni kuibua ukweli, mbona kipindi chote alikuwa kimya Sasa hivi ndio anajifanya anajua wajibu wake.
 
Kwani yeye ni mpumbavu. Ulitaka ajipige Risasi mwenyewe. Wakati wa Magufuli nani alikuwa jasiri mbele ya kifo
Shujaa huwa halilii bunduki! Kama aliogopa basi aendelee kuogopa badala ya kuleta unafiki
 
Wapo waliojitokeza kumkabili Magufuli na kumwambia live, kupitia press conferences na hata bungeni (Tundu Lissu), kupitia mitandaoni tena kwa kutumia majina yao halisi (Ben Saanane), kupitia taratibu za kikazi ( Prof. Assad na Prof. Benno Ndulu). Kwa kweli waliothubutu kumkabili NDULI Magufuli hawakuwa wengi, na sababu ni majanga yaliyowakuta hao waliothubutu.
Tundu Lissu alinusurika kuwa executed kwa muujiza wa Mungu tu. Ben Saanane hakuwa na bahati hiyo. Assad alikumbana na misukosuko kibao, na Prof. Ndulu pia.

Wapo ambao naweza kuwaita wanafiki, mfano Spika Ndugai. Lakini wale wa aina ya Balile wala siwalaumu. Kama walishindwa kutimiza wajibu wao wakati ule, wakiutimiza sasa hivi kuna shida gani?
Hata hivyo mimi na wewe hatuwezi kulinganishwa na watu aina ya Balile. Wao wanaongea kwa majina yao halisi. Mimi na wewe tunaojificha kwenye keyboard tunapata wapi ujasiri wa kuwakosoa??
 
CC: joto la jiwe
 
Ni vyema kusimamia unachokiamini muda wote badala ya kuwa mnafiki. Mbona hakuogopa alipoandika madudu ya Bandari na JPM akawasifu. Kama walikuwa wanaogopa basi wangenyamaza kimya pia kwa hilo.
 
Duuh ndio maana wamerudisha stika za usalama bara barani wanatafuta kila sehemu ya kuchanga hela...
 
Mama Samia anaubunifu? Yeye alishasema kazi yake ni kuangali graph! Sasa hapo ujiongeze nini kitatokea? Mama samia tumwache apambane kivyake msije hapa kumtetea wakati mwenzake JPM alikopa na akafanya vitu vya kuonekana!
Tembelea serikali za mitaa uone anavyomwaga pesa. Hana mbwembwe wala majivuno hivyo unaweza ukawa haufahamu.
 
Mkuu, hata kama Magu kafanya yote hayo, kama kulikuwa na uwezekano wa kufanya mengi zaidi, kwa gharama nafuu zaidi, kuna ubaya gani kusema?

Kwa mfano, katika ujenzi wa SGR, Wabunge wa upinzani walipendekeza kitumike chuma cha kwetu, badala ya kuagiza toka nje. Nadhani kwa kuwa Magufuli alikuwa na haraka ili aonekane kafanya yeye, alikataa. Kitaifa tungefaudika zaidi kuvuna chuma chetu, na kwa maslahi ya muda mrefu. Ila alifanya hivyo kwa maslahi binafsi. Ingechukua muda zaidi kuanza. Matokeo yake gharama kubwa inatumika. Pia financing ya SGR kulikuwa na better options. Sasa hivi miaka 6, bado hatujaanza kutumia Dar - Moro.

Kamati ya Bunge inayohusika na bajeti, chini ya Hawa Ghasia, waliwahi kuhoji iweje serikali inatumia zaidi commercial loans, ambazo zina riba kubwa zaidi na zinaiva mapema, badala ya concessional loans ambazo riba ni ndogo zaidi na maturity ndefu zaidi.

Bila shaka ubabe na nia ovu zilimvuta zaidi kwenye commercial loans.

Pia hii habari ya kununua ndege cash, kuna catch-22 ambayo ina harufu mbaya. Ukinunua bila cash, kuna njia nyingi, inabidi uwe na Business Plan, ambayo itaonesha utakavyofanya ili mradi uwe na mafanikio. Lakini ukinunua cash, hata ukiipaki ndege miaka 3, hakuna shida.

Pia Magufuli alikuwa Fisadi wa kupindukia. Alipata wapi fedha za uwekezaji mkubwa vile kule Chato, bilakupitia bajeti? Kiwanja cha ndege, navingine vingi ?
 
Makusanyo ya wapi propagamda tupu
 
Mafisadi lazima mjipe moyo...poleni nchi hii hairudi tena kwenye mikono yenu hata mkatambikie makaburi ya babu zenu...Kama alivyoingia 2015 bado Mungu anampango na nchi hii
 
Fisadi anawekeza kwenye public goods mie binafsi namuunga mkono....
 
Tuliambiwa tozo zitajenga vituo vya afya shule umeme maji lakn tunakopa kwa ajil ya shule afya maj umeme

Hapo ndyo mnatuchanganya sisi darasa la Saba B

..serikali iwe inatoa ufafanuz wa lugha nyepesi kwa sisi la 7B tuweze kuelewa ..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…