Balile: Magufuli katutenda, deni la nje lafikia shilingi Trillion 78

Balile: Magufuli katutenda, deni la nje lafikia shilingi Trillion 78

Nafikiri alikopa kulingana pia na uwezo wa nchi! Unajua ukuaji wa uchumi ndo uwezo wa kukopesheka pia! Na utambue miaka yote tumekopa lakini kilichokuwa kinafanyika cha maana hakikuwepo! Ila kwa vile wote mmegeuka wakosoaji wa Magufuli ili kumlinda mama! Mwambie apambane asisingizie Madeni hata Marekani wana madeni ya kutisha!
Kwa hiyo miradi yooote ya maji nchi nzima kaweka Magufuli peke yake?? Ee maana unasema hakuna cha maana kilichofanyika kabla ya Magufuli . Usambazaji wa maji kazi kubwa nchini imefanywa na Nyerere na Kikwete. Magufuli alikuwa anazindua tu miradi ya maji ya Kikwete. Mloganzila ni kazi ya Magufuli ? Emergency Dept ya Muhimbili kaiweka Magu? Mwendokasi kaweka Magu? Na mengine meeeengi. Mnazidisha mno misifa kwa Magu. Ndiyo, yapo mengi kafanya, lakini kamwachia Samia matatizo mengi.

Magu alikuwa anadhulumu fedha kwa kutumia kina Sabaya na mbinu zingine chafu. Alikuwa anasababisha biashara nyingi zifungwe. Hiyo pekee imetuletea matatizo ya muda mrefu.

Kwa kutoajiri walimu muda wote huu, huku idadi ya wanafunzi mashuleni ikiongezeka, kutokana na "Elimu bure", Magu kamuachia Samia bomu.
 
Magufuli katutenda deni la taifa, trilioni 78 Samia msalabani

Jamhuri October 26, 2021

Na Deodatus Balile

Kazi hii ya uandishi wa habari moja ya majukumu yake ni kuanika ukweli minong’ono inapotawala katika jamii.

Kwa sasa kuna minong’ono mingi. Minong’ono imeanza baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kutangaza hadharani mkopo wa Sh trilioni 1.3, alioukopa kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na akatangaza miradi lukuki itakayotekelezwa kwa kutumia mkopo huo.

Miongoni mwa miradi ya kihistoria ni ujenzi wa madarasa ya sekondari 15,000 nchi nzima na madarasa ya shule za msingi 3,000.

Kwa sasa inakadiriwa kuwa nchi ina upungufu wa madarasa 11,000, lakini Rais Samia ameamua kuona mbali.

Ameamua kufuta mfumo wa zima moto, ambapo kila mwaka wazazi wanakabwa koo vijijini kuchangia ujenzi wa madarasa.

Baadhi ya wazazi pia wameanza minong’ono kuwa watoto wao wamepewa mikopo kidogo, yaani Sh 600,000 kama ada vyuoni.

Hawajui kuwa miaka yote imekuwa hivyo na wakati mwingine wengi wanakuwa hawapati kabisa hata senti tano ya mkopo.

Sitanii, naomba nizungumzie kwa ufupi miezi sita ya Rais Samia akiwa Rais wa Tanzania baada ya kuapishwa Machi 19, 2021.

Nakumbuka vema kilichotokea, maana baada ya kifo cha Rais John Magufuli kulitokea kama sintofahamu hivi.
Wapo watu walioamini Rais Samia angeendelea kuwa Kaimu Rais, baadhi walidhani tunakwenda kwenye uchaguzi mpya na wengine hawakufahamu nini kitatokea.

Asubuhi ya Machi 18, 2021 niliamkia studio za Televisheni ya Taifa (TBC1) na TBC Taifa (radio) kufanya mahojiano na Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Dk. Ayub Rioba.

Hii ilikuwa ni baada ya kifo cha Rais John Magufuli, kilichotokea Machi 17, 2021. Ikumbukwe wiki moja kabla nilikuwa nimefanya mahojiano na kituo cha Star TV nikasema tuambiwe bayana Rais Magufuli yuko wapi na anafanya nini.

Machi 18 pamoja na kwamba nilikuwa bado Kaimu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), ambapo baadaye nilichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa TEF Mei 22, 2021, ilinilazimu kutoa ufafanuzi huo uliokuwa tamko zito.

Sitanii, tamko nililolitoa lilizaa kuapishwa kwa Rais Samia kuwa Rais wa Awamu ya Sita Machi 19, 2021. Nilirejea Katiba ya Tanzania (1977) Ibara ya 37(5) inayosema: “Endapo kiti cha Rais kitakuwa wazi kutokana na Rais kufariki dunia, kujiuzulu, kupoteza sifa za uchaguzi au kutomudu kazi zake kutokana na maradhi ya mwili au kushindwa kutekeleza kazi na shughuli za Rais, basi Makamu wa Rais ataapishwa na atakuwa Rais kwa muda uliobaki katika kipindi cha miaka mitano na kwa masharti yaliyoelezwa katika ibara ya 40, kisha baada ya kushauriana na chama cha siasa anachotoka Rais atapendekeza jina la mtu atakayekuwa Makamu wa Rais na uteuzi huo utathibitishwa na Bunge kwa kura zisizopungua asilimia hamsini ya wabunge wote.”

Kwa mara ya kwanza kupitia makala hii ninakisema kilichotokea baada ya tamko hilo. Walinipigia simu watu wengi wakiwa na hofu.

Baadhi hawakufahamu Katiba inasemaje. Walinishutumu wakidai nimetangaza utaratibu wa kwangu, kwani baada ya kifo cha Rais kinachofuata ni uchaguzi.

Hii ilinipa shida kuona hata baadhi ya wabunge hawakufahamu nini kinafuata baada ya kifo hicho. Machi 18, 2021 itabaki kuwa siku ya kihistoria kwangu, kwani ujumbe nilioutoa ulitangazwa katika radio zote za ndani na za kimataifa na siku moja baadaye Rais Samia akaapishwa.

Sitanii, leo ninazungumzia mzigo wa madeni ambao Rais Magufuli amelitwisha taifa letu. Nimetangulia kusema na ninarudia, mimi ni msema kweli. Wala sipepesi macho katika kusema ukweli.

Wakati Rais Magufuli kwa miaka mitano yote alikuwa anawaaminisha Watanzania kuwa nchi inajenga miundombinu na inanunua ndege kwa kutumia fedha zetu wenyewe, uhalisia ni kinyume chake.

Kwa kipindi cha miaka mitano tu, Rais Mafuguli amekopa fedha nyingi kuliko fedha zote alizokopa Rais Benjamin Mkapa kwa miaka 10 aliyokaa madarakani.

Kwa miaka mitano, amekopa pia fedha nyingi kuliko alizokopa Rais Jakaya Kikwete kwa miaka 10 naye aliyokaa madarakani.

Rais Mkapa alirithi madeni mengi mno. Alipambana nayo, akaiingiza nchi katika Mpango wa Kusamehe Madeni Nchi Maskini (HIPC) na hadi anatoka madarakani, Tanzania ilikuwa inadaiwa Sh trilioni 20 tu.

Rais Kikwete wakati wake deni la taifa liliongezeka kwa Sh trilioni 23, hivyo akatoka madarakani deni la taifa likiwa Sh trilioni 43 kwa miaka 10. Rais Magufuli kwa miaka mitano tu, deni la taifa limeongezeka kwa Sh trilioni 29 na kufikia Sh trilioni 72 hadi anafariki dunia Machi, 2021.

Sitanii, kwa kasi hii ya ukopaji ina maana kama angekaa madarakani kwa miaka 10 kamili na akaendelea na kasi ya ukopaji wa wastani wa Sh trilioni 29 kwa miaka mitano, basi angetoka madarakani deni la taifa likiwa Sh trilioni 101 kufikia mwaka 2025.

Kuna jambo baya halisemwi. Rais Magufuli amekopa mikopo ya kibiashara inayoanza kulipwa baada ya miaka mitatu na inapaswa kulipwa ndani ya miaka minane, ikiwa na riba za kati ya asilimia 6 na 8.

Baadhi ya mikopo hii imeiva tayari. Imeanza kukuza deni la taifa kwa kasi kutokana na riba. Deni la taifa sasa limefikia Sh trilioni 78.

Kwa vyovyote vile iwavyo, Rais Samia anapaswa kuchukua hatua za haraka, ikiwamo kuunda timu ya majadiliano na wakopeshaji kwa ajili ya kubadili masharti ya mikopo ya kibiashara aliyochukua Rais Magufuli.

Anapaswa kuomba msamaha wa riba na pengine kuomba kuongezewa muda wa kulipa deni kama ulivyo utaratibu wa mikopo kwa serikali nyingi duniani.

Mikopo mingi kwa serikali huwa inalipwa kati ya miaka 20 hadi 50 kulingana na ukubwa wa mkopo na hutozwa riba kati ya asilimia 0.3 hadi asilimia 1. Mikopo ya aina hii inapatikana katika Benki ya Dunia, Shirika la Maendeleo Duniani, Benki ya Maendeleo Afika na nyingine za aina hii.

Kwa bahati mbaya na kwa masikitiko makubwa, kwa miaka mitano Wazungu tuliowaita mabeberu, ila tukawa tunakopa fedha zao kupitia benki za biashara. Kwa hali halisi, madeni haya yakiiva yote, ikiwa hakuna majadiliano ya dharura kuomba marekebisho ya masharti ya mikopo tuliyochukua chini ya Rais Magufuli, itafika mahala asilimia 60 ya bajeti ya taifa letu itakuwa inakwenda kulipa madeni. Waliomo serikalini watajua la kufanya katika hili.

Sitanii, ninafahamu baadhi ya wasomaji watakuwa wanaanza kufuka moshi kwa kusema ukweli huu. Wanajiuliza taarifa hizi nimezipata wapi? Taarifa hizi si za siri. Ziko wazi kwenye tovuti ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Nimepitia taarifa za mapitio ya mwenendo wa uchumi tangu mwaka 2000 hadi 2021. Zipo mtandaoni na zinaonyesha deni lilivyokua hatua kwa hatua. Kwa nia ya kuweka uelewa unaofanana, ifuatayo ni hali ya deni la taifa tangu mwaka 2005 hadi 2021.

Oktoba 2005, deni la nje lilikuwa USD milioni 8,361.9 sawa na Sh 19,286,471,493,000 na deni la ndani lilikuwa Sh 1,712,800,000,000. Jumla kuu ya deni wakati Rais Mkapa anaondoka madarakani lilikuwa Sh 20,999,271,493,000 (Sh trilioni 20.9). Nimekokotoa hesabu hizi kwa kutumia viwango vya BoT vya kuuza dola ya Marekani ambavyo ni USD 1 kwa Sh 2,306.47.

Oktoba 2015, wakati Rais Kikwete anatoka madarakani deni la nje lilikuwa USD milioni 15,321.3, sawa na Sh 35,338,118,811,000 na deni la ndani lilikuwa Sh 7,826,200,000,000. Jumla kuu deni la nje na deni la ndani lilikuwa ni Sh 43,164,318,811,000 (Sh trilioni 43.1).

Deni la taifa lilianza kupanda kwa kasi Oktoba 2016. Deni la nje lilipanda na kuwa USD milioni 16,407.6 sawa na Sh 37,843,637,172,000, huku deni la ndani nalo likipanda na kuwa Sh 10,089,000,000,000. Jumla kuu ya deni ikafikia Sh 47,932,637,172,000 (Sh trilioni 47.9).

Oktoba 2017 deni la nje lilipanda kwa kasi kubwa na kufikia USD milioni 19,074.4 sawa na Sh 43,994,531,368,000. Kutokana na makandarasi kutolipwa deni la ndani nalo lilikua na kufikia Sh 12,563,300,000,000. Jumla kuu ya deni kwa mwaka huo likawa Sh 56,557,831,368,000 (Sh trilioni 56.5).

Oktoba 2018, deni la nje lilizidi kupanda na kuwa USD milioni 20,759.1 sawa na Sh 47,880,241,377,000, huku deni la ndani nalo likipanda na kuwa Sh 14,116,100,000,000. Jumla kuu ikawa Sh 61,996,341,377,000 (Sh trilioni 61.9).

Oktoba 2019, mwanamume aliongeza tena deni la taifa, deni la nje likafikia USD milioni 22,569.4, sawa na Sh 52,055,644,018,000, huku deni la ndani likipanda na kufikia Sh 14,187,400,000,000. Jumla kuu ya deni ikafikia Sh 66,243,044,018,000 (Sh trilioni 66.2).

Oktoba 2020, deni la nje lilipanda na kufikia USD milioni 23,599.3, sawa na Sh 54,431,077,471,000, huku deni la ndani likifikia Sh 15,608,500,000,000. Jumla kuu ikafikia Sh 70,039,577,471,000 (Sh trilioni 70).

Machi, 2021 wakati Rais Magufuli anafariki dunia, deni la nje la Tanzania lilikuwa limefikia USD milioni 24,429.2, sawa na Sh 56,345,216,924,000. Deni la ndani nalo lilipanda na kufikia Sh 16,116,500,000,000. Jumla kuu, deni la taifa lilifikia 72,461,716,924,000 (Sh trilioni 72.4).

Kilichofuata baada ya hapo, madeni yameanza kuiva kwa ajili ya kulipwa, huku mengine yakizalisha riba ya kufa mtu.

Makandarasi wengi Tanzania wanadai mabilioni kati ya hizo Sh trilioni 16 ambazo ni deni la ndani hawajalipwa siku nyingi. Kutokana na hali hiyo, madeni haya yaliyokopwa bila mpangilio katika benki za biashara yameanza kuwa msalaba kwa Rais Samia.

Taarifa ya hali ya Uchumi ya BoT ya Septemba, 2021 inayorejea mwezi Agosti, 2021 kutokana na mazingira hayo, deni la nje limekua na kufikia USD milioni 25,956.1 sawa na Sh 59,866,965,967,000, huku deni la ndani nalo likikua na kufikia Sh 18,225,000,000,000. Ukuaji huu unafanya kiwango cha deni la taifa kufikia jumla kuu ya Sh 78,091,965,967,000 (trilioni 78).

Sitanii, deni hili likigawanywa kwa Watanzania milioni 60, bila kujali mkubwa na mdogo, kila Mtanzania anadaiwa Sh 1,301,533 (Sh milioni 1.3). Hata hivyo, wataalamu wa uchumi wanasema deni hili si tishio kwa uchumi wa taifa letu kwa sasa kwani liko katika uwiano wa asilimia 30 kwa uchumi wa taifa letu, wakati kuna mataifa Afrika ambayo tayari yana uwiano wa asilimia 54 ya deni kwa uchumi wa nchi zao, ila wanaionya serikali iepuke mikopo ya kibiashara ina riba kubwa, masharti mabaya na inalipwa kwa muda mfupi.

Pale Dodoma, tumeona Rais Samia ameanzisha utaratibu mpya wa ukweli na uwazi katika mikopo. Ameeleza fedha alizokopa zitafanya nini kwa kuorodhesha miradi itakayotekelezwa na akatueleza amezikopa kutoka wapi.

Ninajiuliza, hivi ilikuwa ni kwa faida ya nani Rais Magufuli na wapambe wake kuficha ukweli kuwa miradi ya reli, barabara, umeme, ujenzi wa hospitali na mingine mingi aliyoijenga alikuwa anakopa?

Hivi sisi kama tungejua anakopa, tungemzuia? Lakini si tungepata fursa ya kumshauri asichukue mikopo ya kibiashara inayoanza kututoa utumbo sasa? Mungu ibariki Tanzania.

Copyright [emoji2398]2021. Gazeti la Jamhuri
Huyu mwandishi nashauri arejee maongezi ya Hayati Magufuli maana alikuwa anasema tumekopa sana
 
Fisadi anawekeza kwenye public goods mie binafsi namuunga mkono....
Lowasa aliwezesha ujenzi wa shule za kata, lakini ni fisadi mkubwa. Kama Magufuli angekuwa na nia njema kweli, angeanzisha kodi kwa wenye nyumba za kupangisha.

Serikali ingepata siyo mabilioni, bali trilioni. Kwa nini hakufanya? Nimemtaja Magu sababu ndio rais aliyeonesha uthubutu mkubwa zaidi.
 
1. Magu alikomba hela za mfuko wa korosho.

2. Akaingia kwenye account za watu na kukomba hela.

3. Akavamia wafanyabiashara wa bureau de change akatwaa pesa zao.

4. Akatumia pesa kununua wanasiasa wa upinzani.

5. Akatumia pesa kwenye chaguzi
alizokwenda kuzivuruga anyway.
 
Njaa inamsumbua, hawa ndo wanato sifa zisizo na tija,
Wasubili hata miaka ifike mitatu ndo wasifie,
Hizo ni teuzi wanata tu hakuna kingine.

Wangejua kwa sas huku mtaani palivyo pagumu, unashinda kwenye biashara huoni mnunuzi na watu ndo wameachwa na pesa zao lakini shida tupu.

Kinachofata ni watu kufilisika bila kunyanganywa mali yako.
Lini palikuwa rahisi? Washenzi nyie si mliharibu mambo miaka yote 6 hadi mkaanza kupora pesa za matajiri?

Watu wakati wanalalamika kwamba vyuma vimekaza si mlikuwa mnawaita wapiga dili na hawafanyi Kazi? Kenge wakubwa nyie..

Saizi Samia anajitahidi kulaonisha lakini anakumbana na ma riba ya mikopo mliyopiga na kihonga,kujenga Chato na upumbavu wa kununua wapinzani na mamairadi uchwara..Washenzi wakubwa nyie.
 
Wandishi wetu wengi ni wanafiki sana. Atakuwa anawinda cheo cha Msigwa huyo. Anachokisema sasa kilishazungumziwa hapa JF.

Ukubwa wa deni la serikali na mikopo kutoka benk za kibiashara vyote vilizungumziwa hapa.

JPM alikuwa ana agenda yake ambayo kwa bahati mbaya imeshindwa kufanikiwa. Hizo propaganda zilizokuwa zikiendelea kipindi kile zilikuwa calculated. Akina Kabudi, Polepole na Bashiru hawakuwekwa pale kwa bahati. Ukiangalia their past ndiyo utajua kwa nini waliwekwa pale......!!
Majambazi tuu ni vile ma ccm huwa wanalindana ila walitakiwa kuwa nyuma ya nondo saizi.
 
Hapa inabidi ahojiwe waziri wake wa fedha, kwa kuwa walitueleza wanatumia fedha za ndani, ni vipi deni kupaa!
 
Mzee wakati wa Mwendazake hiyo tovuti ya BoT si ilikuwepo, mbona hukuitumia na kuleta taarifa kama hizi? Nakumbuka kuna wakati gazeti lako lilisifiwa hadharani na JPM kwa kuibua uozo sijui bandarini ama wapi lakini hili ambalo unasema linatutoa utumbo hukulisema. Leo ndio umeliona, kweli ya Mungu mengi.
Tatizo ni wanafiki sana
 
1. Magu alikomba hela za mfuko wa korosho.

2. Akaingia kwenye account za watu na kukomba hela.

3. Akavamia wafanyabiashara wa bureau de change akatwaa pesa zao.

4. Akatumia pesa kununua wanasiasa wa upinzani.

5. Akatumia pesa kwenye chaguzi
alizokwenda kuzivuruga anyway.
Saizi mifuko ya pension ina madeni balaa yaani ni hatari karibu ina collapse.Yule bwana hajui kuzalisha pesa ila kuharibu na kitumia vya wengine,hovyo kabisa.
 
Kwa taarifa yako hizo unazoambiwa ni fedha za kujenga madarasa kutokana na tozo ndio rejesho la vaccine ya Uviko19 na usitegemee eti ipo siku serikali itakuwa na transparency kwa kila jambo. Bora hata JPM alisema fedha zetu za ndani na kimantiki alikuwa sahihi kama unakopa kujenga then unalipa from inner source hizo fedha ni zako baada ya kukamilisha mkopo (na ndio maana deni huwa lako) hizo ni tofauti na msaada wa mashimo ya vyoo. Kinadharia anaweza kuwa hakuwa sahihi na hilo ni swala binafsi na pia ki protocol... Kitu ambacho unakishangilia sasa ni mama kukopa fedha za Uviko then hakwambii nani atazilipa na kutoka chanzo gani?.

Angalia kupanda kwa bidhaa za petrol angalia Chuma angalia ushuru wa imported products kuanzia mafuta ya kula mpaka utaelewa tu.
Wewe na huyo kenge wako mwendazake ni wapumbavu tuu,,pesa zote mlizokopa mlifanyia nini cha maana?

Leo unatunga upumbavu wako mara ooh tozo za kulipia uviko 19 mara sijui nini yaani unatapa tapa wakati umeambiwa matumizi ya pesa husika.

Unadhani Samia ni mtu muongo na mshenzi kama mtu wako? Samia yuko clear na malengo ya pesa zake na matokeo yanaonekana.
 
Jamaa anahisi wenye pesa ya kupanda ndege wanapatikana Dar tu. Uwanja wa ndege ni mradi utakaonufaisha umma! Watu wakiweza kula flight moja kwa moja toka chato mpaka duniani huko ni achievement kubwa sana!
We nae ni kenge tuu,kwa hiyo inakopa pesa kwa masharti ya kibiashara unajenga uwanja useless Chato afu unasubiria siku watu wakija kupata pesa miaka ijayo ndio uwe na tija? Una akili timamu?
 
Hivi nyie watu mmerogwa, au?!

Yaani unaonea fahari kukopa sekta binafsi... are you serious?!

FYI, ukiona taifa linakopa kwenye private bank basi hiyo ni last resort!! Private Banks wanafurahia hii mikopo ya kuwakopesha serikali, na ndo maana mingini inahusishwa na rushwa!!

Na watoaji wa rushwa hizi sio wengine, bali mabenki wenyewe!! Kuna mwenzako mmoja hapo juu katolea mfano wa Credit Suisse na mkopo wa Msumbiji, lakini inaelekea ama issue yenyewe haifahamu vizuri au ameamua tu kudanganya!!!

Credit Suisse wametoa mkopo Msumbiji huku mabilioni ya pesa yakiwa yameishia mifukoni mwa waliofanikisha deal la Msumbiji kukopa Credit Suisse!! Ni kama ambavyo ilitokea back in 2013 pale tulipochukua mkopo Stanbic!!

Kwenye mkopo ule ikaja kugundulika Enterprise Growth Market Advisors, kampuni ambayo iliiunganisha Stanbic na serikali, wao wakaingiziwa zaidi ya Sh 10 Billion na Stanbic!!

Ukishakuwa na collateral, Benki Binafsi watakupa tu pesa... kwahiyo wala sio issue ya kukopesheka!!

Hata Msumbiji walikopeshwa USD 1 Billion na Credit Suisse wakati ambao taifa hilo lilipogundua gas ya kutosha!!!

With huge gas discovery in Tanzania, hakuna private bank inayoweza kuacha kuikopesha! And FYI, hizo benki binafsi zinaweza kuwa comfrtable zaidi kumkopesha Samia kuliko JPM ambae alikuwa branded kwamba hatabiriki!!

Kitu kinachoogopwa zaidi na private banks ni unpredictability of the government policy!! That having been said, kama hizo benki ziliweza kumkopesha JPM, basi kwa Samia wanaweza kufanya mara 10...

hapa naongelea financial risk assessments... sio ushabiki wa kisiasa!

Kwahiyo acheni huu ushabiki wenu!!! Kukopeshwa na benki binafsi wala sio jambo la kujivunia kwamba eti "tunakopesheka"!!

Sasa kama hao IMF & WB walifahamu kwamba JPM ni matendo na sio maneno, na Samia ni maneno na sio vitendo; kwanini basi wakaamua kumkopesha mtu wa maneno bila vitendo na kuacha kumkopesha mtu wa vitendo badala ya maneno?!

Ukiangalia mikopo mingi ya IMF na WB iliyotolewa enzi za JPM ni ile ambayo ni mwendelezo wa awamu zilizopita!!

Au ndo kwavile unadhani kukopa benki binafsi ni suala la kujivunia?
We ni kenge kama kenge wengine,,pesa za masharti ya kibiashara ni pesa at your own risk na hizo mikopo hazina masharti yoyote na wanapenda Sana ukope kwa staili hiyo Ili upigwe vizuri..

By the way mikopo mingi ya kibiashara haitolewi na WB na IMF bali kutoka financial markets kama mabenki binafsi.

Samia hakopeshwi mikopo ya kibiashara bali concessional loans ambayo hadi ukopeshwe basi wamekuamini na wanataka uwazi na uwajibikaji .
 
Mikopo yooote ya JPM tunajua ilifanya nini nakila mtanzania anaiona na iliyokamilika anaifaidi. Tunasubiri isiyokamilika kama JKN Hydro dam ikamilike mwezi ujao. (ingawa kwa huyu mama na akina January wake-nina mashaka!)
Ilifanya nini? Tunaona nini?
 
We nae ni kenge tuu,kwa hiyo inakopa pesa kwa masharti ya kibiashara unajenga uwanja useless Chato afu unasubiria siku watu wakija kupata pesa miaka ijayo ndio uwe na tija? Una akili timamu?
Kwa akili hizi bora hata Magu angekugongea dadaako ampe ukuu wa wilaya pengine ungekuwa hata dereva wake😂
 
Maneno umeongea mwenyewe halafu unasema nimekuwekea maneno?

Toa mfano MMOJA TU wa hayo maneno niliyokuwekea...

NI wewe mwenyewe ndie umesmema kwamba:-

Yaani hapo unataka kudanganya LIVE kwamba hata private banks za kibeberu haziwezi kukopesha nchi maskini bila approval ya IMF....

Ukaendelea kwamba:-

Kwanza hiyo 200M sio kwamba walilazimishwa...

Narudia... chanzo cha sakata hili sio IMF kama unavyojaribu kuaminisha watu bali financial regulators wa US, UK na Uswisi. Baada ya wao kufanya uchunguzi, ndipo wakagundua violation of money laundering control na massive corruption!

Hiyo 200M uliyoitaja bila kufahamu undani wake, inahusishwa na settlement ya corruption kwa sababu, uchunguzi ulithibitisha maofisa wa benki kuweka kibindoni zaidi ya USD 50 Million na Wafanyakazi wa Serikali ya Msumbiji na wenyewe waliweka kibindoni zaidi ya USD 130M!

Ingawaje hizo pesa zililipwa na benki husika, lakini burden yake ilienda kwa serikali kwa sababu inakuwa cost of loan!! Ni kutokana na hilo, ndo maana Credit Suisse wakaji-commit kufuta mkopo kwa USD 200M kama compensation ya pesa iliyoingia mifukoni mwa watu lakini burden inahamia kwa serikali ya Msumbiji!

Narudia... SIO KWELI

Issue sio Credit Suisse kukopesha bila idhini!!

Private banks hawahitaji idhini ya IMF ili kukopesha nchi!

Uhusika wa IMF kwa muktadha unaoeleza, ni kama ulivyo kwa any Creditor to her Debtor!!

Kwamba, taifa kama Msumbiji linapotaka mkopo toka popote pale, Lender atataka kufahamu financial status ya mkopaji, hii ikiwa ni pamoja na madeni aliyonayo na creditors wengine. Ni kutokana na hilo, ndo maana wengine wanakuwa na Credit Bureau!!

Sasa issue ya Msumbiji na IMF ilikuja wakati financial regulators niliowataja wakiendelea na uchunguzi wao dhidi ya Credit Suisse vs Mozambique! Hapo ndipo serikali ya Msumbiji ikazungumzia suala la guarantee waliyoweka kwenye mkopo MWINGINE toka kwa Credit Suisse!!

Hapo ndipo IMF wakafahamu kwamba kumbe kuna mkopo mwingine ambao wao walikuwa hawajui wakati walikuwa katika process za kutoa mkopo "mwingine" kwa Mozambique... hapo ndipo waka-cancel huo mkopo!!!

Kwahiyo ni issue ya IMF vs Serikali ya Msumbiji na sio IMF vs Credit Suisse!!!

Hayo uliyasema baadae baada kuweka wazi maelezo yasiyo sahihi uliyokuwa umetoa mwanzoni!!

Kama hayana msingi mbona umeshindwa kujibu?! Nimekuuliza swali jepesi sana hapo juu, kwahiyo ningependa kurudia hapa...

TAJA MFANO MMOJA TU wa maneno niliyokuwekea!!

Hapo ulikuwa unajaribu kusema nini?!

We bhana acha kujifanya unajua sana wakati hakuna unachojua...

Hivi unajua IMF wanaingiza dola billion ngapi kupitia contribution quota?!

Hivi umeshawahi kuona Quota Formular inayotumika kuchangia?!

Hivi mataifa kama US yanavyoiletea jeuri UN unadhani ni kwa sababu HQ ya UN ipo Marekani?

Acha kuongea vitu usivyovijua wewe

Halafu unashindwa hata kutumia common sense!!

Yaani IMF waweze ku-control mikopo na ku-minimize default risks kushinda private banks zenyewe?!!

Hivi akina Nyerere waliokuwa wanavimba waziwazi kwamba "...madeni yenu hayalipiki, na kwahiyo hatutalipa".... hivi unadhani mkopeshaji angekuwa ni Private Bank akina Nyerere wangeongea kwa tambo namna hiyo?!

Hilo nishaeleza hapo juu... ACHA KUCHANGANYA MADESA...

Btw, mbona hujaweka hiyo link?! Au huyo screenshot ndo unaita link?

Tatizo lako unasoma articles zilizoandikwa kwa lugha ya layman na wewe unatafsiri word for word without understanding where the author is coming from in terms of regulation, industry norms and the reason for such penalties.

B22833C4-D713-471A-99B6-F29A5E43B736.jpeg


Umeona hiyo FCA fines zao zimezingatia Credit Suisse waliamua kusamehe $200m so ni sehemu ya settlement vinginevyo fine ingekuwa kubwa zaidi tofauti na porojo zako.

Pili, deni la taifa sio lote ni la wizara ya fedha (serikali kuu), humo kuna majumuisho na madeni ya taasisi zingine za serikali. But

Mfano TANESCO anapokopa anatakiwa alipe mwenyewe pamoja na hivyo deni lao litakuwa kwenye vitabu vyao na vitabu vya serikali; ukishindwa kulipa kama ni government guarantee loan serikali inatakiwa kugharamia hilo deni.

Hizo kampuni za Mozambique zilienda kukopa bila ya idhini ya serikali yet mkopo unadhamana ya serikali na hawakujua mpaka hizo taasisi ziliposhindwa kulipa.

Can you see why IMF would be pissed wakati wameweka frameworks za stress test, wewe unakwepa njia zao kwenda kukopesha nchi maskini na uishirikishi serikali kuu.

Vualla mambo yanaenda ndivyo sivyo, ndio maana wanakwambia hawakufuata rules na rushwa ilitumika, in other word hawakufuata taratibu za kimataifa za kukopesha nchi maskini.

Serikali kuu inaweza kopa bila ya idhini ya IMF/WB but there is a catch ukishindwa kulipa madeni yako, structural adjustment policies zinafuata. Ukikataa kupangiwa nao ukopeshwi tena mnakufa njaa. Na ukienda tena private bank upati mkopo kwa sababu ulishindwa kulipa deni lao you are not credit worthy na huyo CEO si ajabu akatimuliwa kazi kwa kutoa mikopo yenye high risk bila ya kufuata taratibu za IMF.

Ndio maana pia kuna ranking the nations credit kutoka kwa watu ‘Moody’s’ na ‘Standard and Poor‘ kuwaambia private lenders credit worthiness za nchi.

Hizo ni baadhi ya sababu nchi maskini kwenda kukopa bila ya kuongea na IMF mambo yakienda kombo inajitengenezea matatizo makubwa siku wakirudi kutaka mikopo yao.

Matter of fact crisis za 70 na 80’s zilitengenezwa na private banks kukopesha nchi maskini ovyo; na ndio sababu zilizopelekea kufutwa kwa madeni ya nchi maskini na donor lenders, private banks wao wakaja ‘Brady bonds’ na reforms za kukopesha nchi maskini zikafanywa na IMF/WB ili makosa yasijirudie tena.

Ni hivi kuna topics personal nikisoma comment najua huyu ni mbobezi, huyu ni average na huyu unga unga; na wewe private finance bado sana. Una unga unga tu kwa kusoma article at face value but can’t reason behind the course of action.
 
Kwa nini miradi inasuasua wakati mwendazake alikopa Trilioni 29 in five years period? Mama SSH hiyo miradi kaikuta, sasa tuambie wewe hizo 29 Trilioni zilizokopwa kwenye commercial banks zimefanya kazi zipi na zipi?
Swali zuri Til.29 zimefanya nini ilhali hakuna hata mradi mmja uliokamiloka miaka yote 6? Majizi yalishika hatamu kwa mgongo wa uzalendo
 
Kwa akili hizi bora hata Magu angekugongea dadaako ampe ukuu wa wilaya pengine ungekuwa hata dereva wake😂
Bora agonge kuliko upuuzi wake na wako unaotetea hapa.Eti nyie machadema na upopoma wenu Ndio mnataka kushika nchi? 😀😀.

Hiyo nchi labda ya Mbowe..Narudia til.29 zimefanya nini ilhali hakuna hata mradi uliokamiloka miaka yote 6?
 
Bora agonge kuliko upuuzi wake na wako unaotetea hapa.Eti nyie machadema na upopoma wenu Ndio mnataka kushika nchi? 😀😀.

Hiyo nchi labda ya Mbowe..Narudia til.29 zimefanya nini ilhali hakuna hata mradi uliokamiloka miaka yote 6?
Sasa miradi sini multiple ilikuwa inafanyika at once!
 
Back
Top Bottom