Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Mchezaji bora wa Mwaka wa Ballon D'or imenyakuliwa na Lionel Messi (33) wa PSG na timu ya taifa ya Argentina. Aliisaidia taifa lake kushinda kombe la Copa America na kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa mashindano hayo.
Hii ni mara yake ya saba kushinda tuzo hii maarufu zaidi duniani kwa wachezaji wa Soka.
Licha ya Messi kushinda tuzo hii wachezaji wengine walioshinda tuzo mbalimbali ni hawa wafuatao:
Hii ni mara yake ya saba kushinda tuzo hii maarufu zaidi duniani kwa wachezaji wa Soka.
Licha ya Messi kushinda tuzo hii wachezaji wengine walioshinda tuzo mbalimbali ni hawa wafuatao:
- Tuzo ya kinda anayeinukia imeenda kwa mchezaji Pedri wa FC Barcelona. Hapo majuzi alishinda tuzo ya Golden Boy.
- Tuzo ya mshambuliaji hatari imenyakuliwa na Roberto Lewandowski.
- Tuzo ya mchezaji bora wa kike imeenda kwa Alexia Putellas (27) wa FC Barcelona. Alifunga jumla ya mabao 35 na assits 19.
- Tuzo ya Golikipa bora (Yachne Trophy) imenyakuliwa na Donnarumma (22), mshindi wa EURO 2020 na mchezaji bora wa michuano hiyo.
- Tuzo ya klabu bora ya mwaka imeenda kwa Chelsea FC ya nchini Uingereza. Ilijinyakulia kombe la Mabingwa Ulaya (UEFA CL).