Ballon d'or vs FIFA best player of the year

Unataka ulete ubishi wa kitoto sasa. Zidane aliibeba Madrid kwa mgongo wake Uefa na akafunga lile wonder goal na Leverkusen mwaka 2002.


Na vipi Schevchenko na Ronaldinho?

Na Sasa Hivi Dunia ya mpira ndio IPO ulaya Ila zamani mpira ulikuwepo America kusini ndio maana Brazil ama Uruguay zenye wachezaji wanaocheza America kusini tupu zilitawala kwa kipindi kirefu mataji ya Kombe la Dunia kuliko timu zote za ulaya combined.

Na siku zote mkuu huwezi ukaforce class, wachezaji wanaokumbukwa Ni wa Tuzo za FIFA, hakuna anaekumbuka Owen ama Nedved Kama top wa Dunia, wanaokumbukwa tu Kama wachezaji wazuri, Ila walioshinda Tuzo za FIFA ndio wanaokumbukwa Leo hii mtafute Mashabiki wowote wa soka mwambie Nedved alikuwa zaidi ya Zidane 2002 au mwambie Schevchenko alikuwa zaidi ya Ronaldinho 2004 Kama atakuelewa.

Na suala jengine mkuu unaamini Ni fair mchezaji wa America kusini anajua Kama Maradona ambaye amesajiliwa na timu ilioshika nafasi ya 18 kwenye ligi ya Italia, akaitoa toka nafasi ya 18 mpaka wakawa mabingwa wa Italia, na akabeba kombe la Dunia, Mafanikio yote hayo Tuzo akapewa Michael platini sababu tu Maradona amezaliwa nje ya Ulaya. Hio ndio Baloon D or.
 

Mkuu hilo goli lilikua ni 2002, na mwaka huo Ronaldo De lima ndie aliekusanya tunzo zote. Nedved alibeba Ballon 2003 ambao ndio mwaka Zidane alibeba Fifa. Hoja yetu ipo kwenye 2003 na sio 2002.

Na 2004 Shevchenko alikua ni zaidi ya Ronaldinho. Umepoteza kumbukumbu mkuu kidogo unaonekanwa. huo mwaka Ronaldinho hata Champion league hakucheza na Barca ilistragle mno kule la liga.
 

Mkuu Wewe ndie utakua humkumbuki Nedved lakini wadau Tunamkumbuka vizuri tu.

Mkuu halafu hua unaropokwa sana mkuu. Maradona hakubeba kombe la ligi mwaka aliosajiliwa. Na mwaka aliobeba kumbe Platini hakua mchezaji bora wa Ulaya.

Halafu hebu pata hii mkuu itakusaidia
Le nouveau palmarès (internationalized reevaluation)YearOriginal winnerAlternative
1958 Raymond Kopa - Pelé
1959 Alfredo Di Stéfano - Pelé
1960 Luis Suárez - Pelé
1961 Omar Sívori - Pelé
1962 Josef Masopust - Garrincha
1963 Lev Yashin - Pelé
1964 Denis Law - Pelé
1970 Gerd Müller - Pelé
1978 Kevin Keegan - Mario Kempes
1986 Igor Belanov - Diego Maradona
1990 Lothar Matthäus - Diego Maradona
1994 Hristo Stoichkov - Romário
 
Kwa ninavyofahamu tuzo hutolewa kwa Mafanikio ya msimu uliopita, hivyo tuzo ya 2003 Ina involve 2002 pia, na hio ilikuwa Ni Era ya Madrid, hata msimu wa 2003 Madrid walibeba super cup, la Liga, international cup na nusu fainali Uefa, hivyo makombe 3 still Zidane ana Ground.

Barca pia huwezi kusema walistrugle, Bali walikuwa ndio wanaibuka na kuanzia 2004 Kupanda wakapindua utawala wa Madrid, mwaka Huu Ronaldinho alikuwa ndio top scorer wao, na walishika nafasi ya Pili la Liga nyuma ya Valencia. Na hio Ni achievement kwa timu ambayo msimu uliopita haikupata Nafasi ya Uefa.
 

Huo mwaka unaozungumza Juventus pia walishinda Serie A, Italian Super Cup napia walicheza Final Champion League.

Nilichokupinga mimi nikua ile haighlight ya goli la Zidane haihusiani kabisa na msimu wa 2003. Ile ilikua 2001 - 2002. Nasi 2002 - 2003 tizama vizuri mkuu.
 

Bali Milan Walibeba Serie A, Italian Super Cup, European Super Cup na Shevchenko akiwa ndio Top Score wa Serie A.
 
Mkuu mbona list yako imechagua miaka?

Na sijasema kwamba Maradona kasajiliwa na kuipa ubingwa Hapo Hapo nimekupa nafasi waliyokuwa Napoli kabla ya kuja kwake (ya 18) na alivyowatoa huko chini na kuwapa ubingwa Mara 2 wa Italia pamoja na Kombe la ulaya.

Na it doesn't matter mwaka Kama Maradona alikuwa anacheza ulaya na alikuwa Bora zaidi kipindi hicho alifaa tuzo apewe yeye, na hii Ni point yangu kwamba Baloon D or haikuwa tuzo Bora ilikuwa Ni Tuzo ya kibaguzi na ilipokuja Tuzo ya FIFA ikaipiku Baloon D or.
 

Mkuu List haichagui miaka list inaonesha masahihisho ya tunzo hao ni washindi wapya wa hio miaka iliotajwa maana yake kwa miaka mengine washindi rasmi wanabaki kuwa ni wale wale.
Ila pia haiondoi washindi wa awali kutambuliwa kama ni washindi.

Mkuu hiyo tunzo ilikua ni kwa ajili ya watu wa ulaya tu kwahiyo hakuna sababu ya Maradona kulazimishwa kuingizwa. Ilipofika mda ikageuzwa ya wote ndio kila mtu kaingizwa. Na hiyo list niliokuekea ni masihihisho ya washindi ambayo inaonesha kua maradonna ni mshindi mara 2.
 
Bali Milan Walibeba Serie A, Italian Super Cup, European Super Cup na Shevchenko akiwa ndio Top Score wa Serie A.
Mkuu ukumbuke Ronaldinho mpaka 2003 Yupo psg na alivyokuja Barcelona aliwasaidia mechi 17 wakawa unbeaten na hata msimu wa 2004 unaanza na tuzo zinatolewa tayari Barca wanaongoza ligi kwa point 9.

Na pia Schevchenko kwa magoli tu alikuwa hampati Henry ambae alikuwa Ni wa Pili, kwenye hizo tuzo na utofauti wa kura ulikuwa mdogo baina Ya Ronaldinho na Henry, Ila Schevchenko aliachwa mbali Sana.

Kipindi hiki tuzo zilikuwa haziangaliwi umefunga magoli mangapi Bali umeisaidia vipi timu yako.
 

Mkuu unaweza kuwa umesahau, Barca ilimtimua kocha katikati ya msimu huku ikiwa kwenye nafasi ya 16, Pia ilikula kipigo cha 5 kutoka kwa mallorca Na Ronaldinho akiwa ndani. Mabadiliko ya kocha na Ujio wa Edger Davids ndio yaliobadilisha muelekeo wa Barca kwenye ule msimu. Kwa kusema Ronaldinho ndie alieyewasaidia basi si lugha nzuri.

Na mkuu Henry alikua akibebwa na Ufarnasa tu lakini hakua na sifa zakushindania tunzo mwaka wowote. Hayo magoli yake yote alikua akiyafunga EPL tu. Ulaya akimalizia makundini magoli yake. Shevchenko alikua ni power house Ulaya. Alibeba Champion league 2003 na alimaliza top score mara mbili Ulaya.

Ushindi wa Ronaldinho tunzo ya FIFA 2004 ni sawa na wa Ronaldo 1996. Yote ni kimuhmko tu. Na ndio mana Ballon D'or inazidi kuonekana bora mbele ya Fifa mana ina uafadhali kidogo katika tunzo zake. Fifa Mihemko imezidi mno. Mchezaji akishakua Super Star basi tunzo inamuhusu moja kwa moja.

Ila tunzo ya UEFA ambayo alishinda VVD kwangu mimi ndio naamini ndio tunzo bora kabisa yenye uwelewa mzuri kuliko zote hizi japokua nayo ina mapungufu yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…