Chief-Mkwawa
Platinum Member
- May 25, 2011
- 31,559
- 42,179
Unataka ulete ubishi wa kitoto sasa. Zidane aliibeba Madrid kwa mgongo wake Uefa na akafunga lile wonder goal na Leverkusen mwaka 2002.Upo Bongo halafu unaizungumza Dunia nzima. Ndoto za wachezaji wote Ulaya ni kushinda Ballon D'or na si FiFa. Fifa walishindwa moja kwa moja kuiangusha tunzo ya Ballon D'or kihadhi na ndio walipotumia kila mbinu mpaka wakaimeza. Na baada ya Blatter kupotea tu tu Ballon wakafanikiwa kujimegua.
Mkuu Dunia ya Football ipo Ulaya, Unapokua mchezaji bora wa ulaya maana yake ndio Dunia nzima. Kigezo cha kua haikujumuisha wachezaji wa nje ya ulaya pre 95 sio hoja nzito kabisa, Bado Fifa wanabakia kua wameanzisha tunzo 1991 na ni juzi tu.
Na Ballon D'or walishatangaza washindi wapya wanyuma wamiaka yote ambaye tunzo zilikua kwa wachezaji wa ulaya tu.
Halafu mkuu punguza mihemko, Zidane 2003 alikichafua nini? Unaukumbuka huo mwaka vizuri lakini? Hebu niambie kati ya Zidane na Nedved nani alikichafua?
Na vipi Schevchenko na Ronaldinho?
Na Sasa Hivi Dunia ya mpira ndio IPO ulaya Ila zamani mpira ulikuwepo America kusini ndio maana Brazil ama Uruguay zenye wachezaji wanaocheza America kusini tupu zilitawala kwa kipindi kirefu mataji ya Kombe la Dunia kuliko timu zote za ulaya combined.
Na siku zote mkuu huwezi ukaforce class, wachezaji wanaokumbukwa Ni wa Tuzo za FIFA, hakuna anaekumbuka Owen ama Nedved Kama top wa Dunia, wanaokumbukwa tu Kama wachezaji wazuri, Ila walioshinda Tuzo za FIFA ndio wanaokumbukwa Leo hii mtafute Mashabiki wowote wa soka mwambie Nedved alikuwa zaidi ya Zidane 2002 au mwambie Schevchenko alikuwa zaidi ya Ronaldinho 2004 Kama atakuelewa.
Na suala jengine mkuu unaamini Ni fair mchezaji wa America kusini anajua Kama Maradona ambaye amesajiliwa na timu ilioshika nafasi ya 18 kwenye ligi ya Italia, akaitoa toka nafasi ya 18 mpaka wakawa mabingwa wa Italia, na akabeba kombe la Dunia, Mafanikio yote hayo Tuzo akapewa Michael platini sababu tu Maradona amezaliwa nje ya Ulaya. Hio ndio Baloon D or.