Balo la viatu vya Mtumba

Balo la viatu vya Mtumba

Nahisi wanaingiza kupitia zambia na uganda kama sijakosea.....kuna jamaa anafanya hii na anauza raba kali kwa elfu 9 tu ioa viatu ni vizuri sana....nitamuuliza kujua zaidi ila ninauhakika anachukulia mbeya sababu nimewahi mpokelea mzigo....

Naomba nitafute taarifa kwa anaaefanya kuhusu bei nitarudi.
Mimi pia ni mmojawapo,nasubiri taarifa yako mkuu
 
Kupoint ndio njia bora na ya uhakika kwa mtu anaefanya biashara za Mtumba (nguo na viatu)

Kununua baloo ambalo hujui ndani kuna nini huna tofauti na mtu anae BET anampa ushindi PSG angali anajua yupo kundi hatari sana.

ukifanya biashara ya mtumba ku point ndio njia salama na nafuu na uhakika 98% kula faida,uki point pair unapoint kitu tunaita SUMU yani unapoint kiatu kabla hujakfksha dukani ukiwa pale pale sokoni unavpanga vizuri kwenye begi Watu wanakupandia DAU.

Nakumbuka siku 1 huko nyuma nikiwa chuo kama kawaida yangu kwenda kununua viatu kwa ajili yangu binafsi nilipoint kiatu kimoja kikali sana kwa sh 7000 ila jamaa akaingia tamaa akasema nimpe 8000 nikampa,kile kiatu nilikiuza pale pale sokoni kwa 50,000 Japo kusema ukweli nilikiuza huku roho inaniuma kwanini sijakivaa hata mara 1 (niosheee)

Hadi na leo hiii na point viatu vya mwanangu, ni viatu ambavyo akivaa mtoto lazima uhisi ni toto la kishua,hadi leo hiii na point viatu vyangu binafsi nikiona tu nimeishiwa Nadamka siku 1 nawahi location nakuta nishaandaliwa mzigo wangu,nabeba nasepa.

KWANINI NAKUSHAURI KU POINT?

siku hizi wafanyabiashara hawataki hasara tena wameshachoka kula hasara kwahiyo baloo likiingia tu wanalirarua usiku usiku wanachambua nguo kali kali au viatu vikali vikali kisha balo linapigwa tena mkanda linakua kama lipo sealed halijaguswa.

wewe ukiliona unadhani halijaguswa ila ushachelewa wajanja zaidi yako wachalichana muda tuuu wakatoa vinavyowafaa,sasa wewe ukiwa mnunua Balo kila siku utalamba hasara na mwisho utaona biashara mbaya wakati si kweli kwamba biashara mbaya,katika biashara nzuri na zenye pesa ni biashara za nguo za mtumba za kike + viatu (aina zote) ukijua kupoint hii ni biashara ambayo ukiianza kuiacha utaiacha YESU akirudi.

Biashara ya kupoint raha n unapoint kitu kwa 3000 unakiuza 30,000 na anaeuziwa anaondoka anachekelea mpk jino la mwisho,ni biashara ambayo kwasiku unahitaji wateja wako wawili tu wafike dukani.

mTeja wa kwanza kanunua Raba uliyo ipoint kwa 5000 wewe unamuuzia 25,000 (20k faida)

mTeja wa pili kanunua sendo uliyoipoint kwa 8000 wewe unamuuzia 35,000 (27k faida)

ukipga Total ya faida kwa siku umeingiza 47,000 hivi unafikiri utakaa uache hiii biashara? Never ni Ujio wa Yesu tu ndio utakufanya uache hii biashara.

Baloo ni hasara katka pair utakazokuta kuna pair mbaya mbaya mbaya hata upewe bure huchukui,halafu mabalo mengine unakuta lina viatu namba ambazo hazina wateja namba zenye wateja wa PESA hukuti hata 1.

na mara nyingi wafunguaji mabalo usiku wanachomoaga pair za pesa ambazo ni namba kubwa kubwa kama 44,45 kuendelea hizo Pair ndio Pesa imelala na hutozikuta hizo pair popote paleee,zinatolewa mapemaaa Watu wenye miguu mikubwa hupata shida sana kupata viatu,sasa anapokuja dukan kwako akakukuta na kiatu kikali saizi yake Hata umwambie bei gani kama hela anayo "HAKIACHI"

nimejaribu kukwambia na kukuelezea umuhimu wa kupoint na kwanini,kwahiyo nadhani akili ukijumlisha na zako kichwani utakua umepata idea ya bora baloo au bora ku point.
Nimekuwa sana mkuu.Mimi kuna wakati nilienda Karume kutafuta bag la mtumba ambalo naweza kubebea laptop.Nikaingia ndani ndani kule,nikafika katika frame ya mzee moja hivi ana bag kali ambalo kiukweli liliukosha moyo wangu.Mzee akanipiga bei mbaya kuwa anauza 25,000/= duuuh nikaishiwa pozi.Ila nikakumbuka kuwa hawa machinga mara nyingi huwa wajanja,atakuwa ananitega.Nikakaza mzee,mwisho wa siku nikachomoa kwa 13,000/= nikamnunulia na kikombe kimoja cha kahawa cha 200.Baada ya pale nilinasa point moja aliposema kwamba,huwa wanadamka mapema wanaenda ku-point then wanarudi kupanga karume.kwa nilivyoelewa mimi,inaonekana huwa wana-point kwa bei rahisi sana.Changamoto niliyonayo sasa nilikujuwa wapi huwa wanaenda ku-point maana inaonekana ni maeneo yale yale ya Kariakoo.Mimi nikijuwa tu naanza biashara.
 
Unaweza tembelea Karume ukaona viatu mkuu then ukaomba uelekezwe wanapochukua.....ila andaa kipesa ili angalau upelekwe sehemu nzuri...

Ila ninachofaham kuhusu viatu vizuri vya mtumba ni vinapatikana sana mbeya na uganda, uganda ndio best place ukipata mzigo hautajuta.
Kati ya Uganda na Kenya kupi kuna viatu vizuri na vingi zaidi,,,mbona naona wabongo wengi pia wakienda kununua viatu Nairobi?
 
Kati ya Uganda na Kenya kupi kuna viatu vizuri na vingi zaidi,,,mbona naona wabongo wengi pia wakienda kununua viatu Nairobi?
Uganda panasifika sana kwa nguo grade nzur za mtumba but viatu ata mbeya vipo vzur mno kuna wadau weng tu ambao bado hawajawa na connection dar wanachukua sana mbeya alaf unakuta wanapenga mwenge ata jamaa wang amefanya sana hii kitu.
 
Nimekuwa sana mkuu.Mimi kuna wakati nilienda Karume kutafuta bag la mtumba ambalo naweza kubebea laptop.Nikaingia ndani ndani kule,nikafika katika frame ya mzee moja hivi ana bag kali ambalo kiukweli liliukosha moyo wangu.Mzee akanipiga bei mbaya kuwa anauza 25,000/= duuuh nikaishiwa pozi.Ila nikakumbuka kuwa hawa machinga mara nyingi huwa wajanja,atakuwa ananitega.Nikakaza mzee,mwisho wa siku nikachomoa kwa 13,000/= nikamnunulia na kikombe kimoja cha kahawa cha 200.Baada ya pale nilinasa point moja aliposema kwamba,huwa wanadamka mapema wanaenda ku-point then wanarudi kupanga karume.kwa nilivyoelewa mimi,inaonekana huwa wana-point kwa bei rahisi sana.Changamoto niliyonayo sasa nilikujuwa wapi huwa wanaenda ku-point maana inaonekana ni maeneo yale yale ya Kariakoo.Mimi nikijuwa tu naanza biashara.
Wannapoint hapo hapo karume usiku sana kuanzia saa 10 ikifika asubh wanapanga bei za kupiga na ilala wanapoint nguo alfajir pia ikifika asubh wanapanga bei za kawaida
 
Nahisi wanaingiza kupitia zambia na uganda kama sijakosea.....kuna jamaa anafanya hii na anauza raba kali kwa elfu 9 tu ioa viatu ni vizuri sana....nitamuuliza kujua zaidi ila ninauhakika anachukulia mbeya sababu nimewahi mpokelea mzigo....

Naomba nitafute taarifa kwa anaaefanya kuhusu bei nitarudi.
Vya Mbeya vinatoka Malawi nadhani! Ila kwa mtumba wao ni mkali sijapata ona yani! Viatu unakuta havijavaliwa vikaisha yani soli mpya raba mpya ni za kufua tu. Zile ukija bongo ukauza 20/20 unapiga hela kishenzi!

Sema kwa hali ya uchumi ni aheri viatu utarget ambavyo havizidi 15K kwa sasa
 
Wannapoint hapo hapo karume usiku sana kuanzia saa 10 ikifika asubh wanapanga bei za kupiga na ilala wanapoint nguo alfajir pia ikifika asubh wanapanga bei za kawaida
Ukienda hata saa 12 ama saa 1 bado unapata kwa bei poa tu,mbaya zaidi ikifika saa 3 ndipo madalali wa kuachiwa kazi ndio muda wao wakupiga
 
Wannapoint hapo hapo karume usiku sana kuanzia saa 10 ikifika asubh wanapanga bei za kupiga na ilala wanapoint nguo alfajir pia ikifika asubh wanapanga bei za kawaida
I get you Lucy.Bilashaka now nimeelewa vema.kumbe hakuna kulala mishe hizo,maana kwa usafiri wa Dar dooh[emoji42][emoji42]
 
Wannapoint hapo hapo karume usiku sana kuanzia saa 10 ikifika asubh wanapanga bei za kupiga na ilala wanapoint nguo alfajir pia ikifika asubh wanapanga bei za kawaida
Huwa unafanya hii biashara nahitaj kujua kitu hapa
 
Last week nilikwenda Mwanza kuulizia kuhusu Viatu

Jamaa mmoja akaniambia kufungulisha baloo grade 1 unatakiwa uchague pea zisizo pungua 30 na kila pea moja ataniuzia 12,000/pea

Ukichukua 30*12,000=360,000/=

Nikaona isiwe tabu nikaja kwa mshikaji wangu anauza Viatu pia nikaomba ushauri alichonijibu nikashangaa Sana

Mshikaji akaniambia ni bora ninunue robota ambalo ni shilingi 400,000/= na zinakaa pea kuanzia 50-55 ukizigawa 400,000/50=8000 sasa ukilinganisha bei ya yule mshikaji wa kufungulisha tayari kanipiga 4000 kwa kila pea na hapo ndo nikamkumbuka mentor wangu CONTROLA kwenye somo lake la kumkwepa Mtu wa kati aka dalali

Hapo kwenye robota lenye pea 50 Ukiondoa pea 30 ambazo utafungulisha zimebaki pea 20 ambazo kwenye laki 400,000-360,000=40,000 je hizo pea 20 akiuza 5000*20=100,000 kweli mjini ukiingia kichwa kichwa unanyolewa bila maji

Kila la kheri mkuu Jitahidi kufanya research kwanza ujiridhishe ndo ununue mzigo

Cheers
Uko so deep CONTROLA 👊🏿👊🏿👊🏿👊🏿
 
Nahisi wanaingiza kupitia zambia na uganda kama sijakosea.....kuna jamaa anafanya hii na anauza raba kali kwa elfu 9 tu ioa viatu ni vizuri sana....nitamuuliza kujua zaidi ila ninauhakika anachukulia mbeya sababu nimewahi mpokelea mzigo....

Naomba nitafute taarifa kwa anaaefanya kuhusu bei nitarudi.
Mkuu ulipata taarifa
 
Vya Mbeya vinatoka Malawi nadhani! Ila kwa mtumba wao ni mkali sijapata ona yani! Viatu unakuta havijavaliwa vikaisha yani soli mpya raba mpya ni za kufua tu. Zile ukija bongo ukauza 20/20 unapiga hela kishenzi!

Sema kwa hali ya uchumi ni aheri viatu utarget ambavyo havizidi 15K kwa sasa
viatu vya mbeya na ata mitumba ya nguo ya mbeya zote zinatoka dar.
Ila kinachofanyika wafanyabiashara weng wa mbeya wenye mitaji mikubwa wanasgiza direct China alaf haifunguliwi inaenda kufunguliwa mbeya so ujanja ujanja haiwi mkubwa sana ndio maana bado unakutana na vitu vizur kwa bei ndogo.

Dar balo linafunguliwa ikifika alaf muuzaji nae anachambua zake kwa washkaji wake ndio uje wewe lazma ukutane na lonya lonya. ila ata mbeya wanachambua kwanza ila haipiti kwenye mikono ya wengi.
 
Back
Top Bottom