Balo la viatu vya Mtumba

Balo la viatu vya Mtumba

viatu vya mbeya na ata mitumba ya nguo ya mbeya zote zinatoka dar.
Ila kinachofanyika wafanyabiashara weng wa mbeya wenye mitaji mikubwa wanasgiza direct China alaf haifunguliwi inaenda kufunguliwa mbeya so ujanja ujanja haiwi mkubwa sana ndio maana bado unakutana na vitu vizur kwa bei ndogo.

Dar balo linafunguliwa ikifika alaf muuzaji nae anachambua zake kwa washkaji wake ndio uje wewe lazma ukutane na lonya lonya. ila ata mbeya wanachambua kwanza ila haipiti kwenye mikono ya wengi.
Aisee Mbeya viatu vikali sana mzee af bei kitonga sana
 
Last week nilikwenda Mwanza kuulizia kuhusu Viatu

Jamaa mmoja akaniambia kufungulisha baloo grade 1 unatakiwa uchague pea zisizo pungua 30 na kila pea moja ataniuzia 12,000/pea

Ukichukua 30*12,000=360,000/=

Nikaona isiwe tabu nikaja kwa mshikaji wangu anauza Viatu pia nikaomba ushauri alichonijibu nikashangaa Sana

Mshikaji akaniambia ni bora ninunue robota ambalo ni shilingi 400,000/= na zinakaa pea kuanzia 50-55 ukizigawa 400,000/50=8000 sasa ukilinganisha bei ya yule mshikaji wa kufungulisha tayari kanipiga 4000 kwa kila pea na hapo ndo nikamkumbuka mentor wangu CONTROLA kwenye somo lake la kumkwepa Mtu wa kati aka dalali

Hapo kwenye robota lenye pea 50 Ukiondoa pea 30 ambazo utafungulisha zimebaki pea 20 ambazo kwenye laki 400,000-360,000=40,000 je hizo pea 20 akiuza 5000*20=100,000 kweli mjini ukiingia kichwa kichwa unanyolewa bila maji

Kila la kheri mkuu Jitahidi kufanya research kwanza ujiridhishe ndo ununue mzigo

Cheers
Kama unaanza biashara, huyo jamaa wa Mwanza amekupa ushauri mzuri kwa kuwa atakuuzia viatu ambavyo ni chaguo lako.

Robota ni kama kuingiza mkono gizani na unakuwa hujui kile utakachotoka nacho. Na niliwahi kusikia ili biashara isisumbue ni heri kununua robota zaidi ya mbili.

Kwa maana ya kwamba marobota yaweze kubebana, ikiwa kati yake ikiwa na viatu vibaya vingi.

Ova
 
Back
Top Bottom