HII POINT IMEPUUZWA KWA WINGI SANA! Hii ingekuwa sera No.1 ya nchi. Ni nafuu kufunga migodi kama madini yanaenda kusafishwa nje. TUNAIBIWA!!
Mkuu sio tu imepuuzwa miaka mingi ni kwasababu watu wameamua kujifanya hawajui kabisa kama kuna kitu hicho.
Mwaka 2006 baada ya JK kushinda Urais alipeleka timu ya watalaam Botswana kujifunza juu ya wanavyofaidika na madini, Binafsi nilipata faraja sana kwasababu nilijua watatoka na kitu huko na wakitoka na hicho kitu kitakuwa cha manufaaa, Kumbe mweee Khaaa!
De Beers Kampuni mbia wa kuchimba Almasi Botswana ndio wamekuwa wabia wetu wa Almasi ya Mwadui miaka mingi sana. Lakini nakwambia huko Botswana Terms ziko tofauti sana.
1. De Beers hawakupewa tenda pekee yao kuwa wawekezaji kwenye sekta ya madini, kilichotokea ni kuwa Serikali iliunda kampuni ambayo ni kama agence na hii agence imeunganisha share na De Beers kwa uwiano wa 50:50 na kampuni mpya inaitwa Debotswana ikiwa ni muunganiko wa majina mawili De Beers na Botswana
2. Kwa vila hizo kampuni mbili zina uwiano sawa wa hisa kwa hiyo top menejiment ipo sawa, yaani wana wakurugenzi wawili, menegers wili (mmoja wa De Beers and mwingine wa Botswana) mpaka level fulani.
3. Wafanyakazi wa kigeni imewekwa level ambayo ni mwisho kuajili, huwezi kuona sijui chini ya mgodi shift supervisor sijui plumber eti ni mgeni, hata mara moja, wageni ni kwenye nafasi ambazo kweli zinahitaji wageni na hakuna wenyeji wenye potentials za kujaza.
4. Wageni wote walioko kwenye senior position wanapewa wazawa chini yao kama wasaidizi wao na jukumu la kuwatrain ili waje wachukue nafasi za wageni siku wanaondoka.
5. Mgeni akishindwa kuprove kuwa mwenyeji aliyekuwa chini yake alimfundisha akaelewa, na ikaonekana kuwa mgeni hakutoa msaada kwa mwenyeji kuelewa ili aweze kuresume position yake siku mkataba ukiisha basi mkataba wake huwa hauwi re-newed ana mgeni mwingine anakuwa hired kujaza nafasi ya mgeni huyu aliyeshindwa kutekeleza wajibu wake wa kumtrain mwenyeji.
6. Mgawanyo wa rasilimali wanzopata ni De Beers wanachukua 60% na Botswana Government wanachukua 40%
7. Baada ya mgawo huo (60:40) De Beers wanatakiwa kulipa kodi, kwa hiyo katika asilimia zao 60 za mgao wakiwalipa kodi wanajikuta wanabaki na 50:50
8. Baada ya kodi wanatakiwa kulipa Mrahaba (ambazo ni kuendeleza maeneo ya jirani na jamii zinazozunguka mgodi) asilimia 3-5
9. mwisho wageni (De Beers) wanajikuta wanaondoka na kitu chini ya asilimia 50.
Kwa ujumla Botswana ni mfano wa kuigwa africa kwa jinsi walivyotumia madini yao, kuna maji safi yasiyokatika mjini Gaborone yanatoka kilomite 600 north karibu na Francis Town, angalia mabasi yao (mpaka yale marefu na hata ya ghorofa kama Uk) Bara bara four ways kila kilomita 50 kuanzia mwishoni mwa gaborone kwenda nje ya jiji. Mji mzima wa gaborone umezungushiwa barabara kubwa za four ways pembeni kwa ajili ya wale wenye haraka wasipite kati kati ya jiji na mgari ya city to city (Northen by Pass, Sourth bypass, east bypass)
Kuna umeme na maji mpaka vijijini kabisa kama Tutume ni mbali sana mji wa Francis Town lakini kuna umeme na maji safi,
Kila mtoto wa botswana anasomeshwa na serikali bure mpaka sekondari, baada ya hapo ndio kuna selection ya watoto wa kwenda University, secondary education ni universal.
Vitabu kila mwaka vinagawiwa kwenye mashule ya serikali na vilivyotumika tayari serikali huvikusanya na kuvipeleka private schools kwa hiyo hakuna anayekosa kitabu Botswana.
Kila kijiji kina dispensary (wenyewe wanaita clinic) na ambulance (labour inatoka nje ya nchi)
Serikali hubadri magari ya idara zake kila miaka minne, na mgari yalitumika huuzwa kwa mnada wa wazi kwa wakulima, first priority ni mkulima, hakuna suala la kujuana wala nini, mkulima anakuja na document zake anaonyesha kuwa yeye ni mkulima (kila mtu ana kitambulisho na anafahamika kwa chief wake, Kota)
Kwa ujumla Madini ya Botswana yameisaidia ile nchi, huwezi kujua kiasi gani wale jamaa wamefaidika mpaka ufike huko. Ndio maana sikubaliani na msemo "Miafrika ndivyo tulivyo" kwani wenyewe wakaumbia ukienda kwao kuwa africa ni North of Zambezi sio kwao, maana haya matatizo ya umaskini ni nyinyi.