- Source #1
- View Source #1
Wakuu naona kumeanza kuchangamka kidogo, tupewe ufafanuzi tuelewe hii taarifa imekaaje
- Tunachokijua
- Balozi Ali Karume ni mwanadiplomasia wa Kitanzania na amewahi kuwa balozi wa Tanzania nchini Italia, Ujerumani na Ubelgiji na Mkuu wa Mabalozi wa Tanzania. Balozi Ali ni mtoto wa Rais wa kwanza wa Zanzibar, Sheikh Abeid Amani Karume na amekuwa mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) tangu kuanzishwa kwake mwaka 1977.
Madai
Kumekuwa na taarifa inayosambazwa katika mitandao ya kijamii ikieleza kuwa balozi Ali Karume amesema atachukua fomu ya Urais Zanzibar.
“BALOZI ALI KARUME asema atachukua form ya kugombea uraisi wa Zanzibar hakuna sheria ndani ya katiba ya CCM kumzuia yeye kuchukua form ya kugombea uraus wa Zanzibar. Asema kijana wa Mkuranga arudi kwao Mkuranga akagombee ubunge hata bandari ya Zanzibar imemshinda kuiendesha hii ndii imenisukuma kutaka kuchukua form ya kugombea uraisi wa Zanzibar.”
Uhalisia wa madai hayo
JamiiCheck imefuatilia na kujiridhisha kuwa taarifa hiyo si ya kweli.
Ufuatiliaji kwa njia ya mtandao na utafutaji wa maneno muhimu umebaini kuwa hakuna chanzo chochote cha kuaminika kilichoripoti taarifa hiyo. Kwa upande mwingine chama cha mapinduzi (CCM) kilishampitisha mgombea wake wa urais kwa upande wa Zanzibar ambaye ni Dkt. Hussein Ali Mwinyi.
Kwa upande wao ndani ya chama hakuna tena mchakato wa kuchukua fomu utakaotangazwa kwa sababu wameshakamilisha mchakato wa kumpata mgombea wao kwa nafasi ya urais
Itakumbukwa pia mwaka 2023, Balozi Karume alivuliwa uanachama kabla ya yeye mwenyewe kusema tena kuwa hatumbui jambo hilo la kuvuliwa uanachama
Aidha JamiiCheck imewasiliana na Balozi Ali Karume ambaye amekanusha pia taarifa hiyo, Balozi Ali amesema;
“Hiyo ni FAKE kwasababu siwezi kwenda kuchukua fomu ambayo haitolewi”