Balozi Bwana: Aliyepigwa na raia wa Afrika Kusini, si Mtanzania

Balozi Bwana: Aliyepigwa na raia wa Afrika Kusini, si Mtanzania

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Kufuatia kusambaa kwa video kwenye mitandao ya kijamii ikimuonesha kijana anayedaiwa kuwa Mtanzania akishambuliwa nchini Afrika Kusini, Balozi wa Tanzania nchini humo, James Bwana, amesema uchunguzi umebaini kuwa mtu huyo si raia wa Tanzania.

Video hiyo, ambayo imekuwa ikisambazwa kwa wingi mtandaoni, inaonesha kijana huyo (ambaye Uraia wake bado haujawekwa wazi) akiwa ndani ya duka lake akitakiwa kuwasilisha nyaraka za kuthibitisha uhalali wa uwepo wake nchini humo. Katika kipande hicho, kijana huyo anaonekana akiwasilisha nyaraka hizo na kusisitiza kuwa ni halali.

Hata hivyo, muda mfupi baadaye, anaonekana kushambuliwa sehemu ya juu ya mwili wake na kuamriwa kufunga biashara yake.

Akizungumza na gazeti la Mwananchi Ijumaa, Machi 27, 2026, Balozi Bwana alisema ubalozi ulifuatilia tukio hilo mara baada ya video hiyo kuibuka, na kubaini kuwa kijana anayehusika si Mtanzania.

“Baada ya kufuatilia suala hili kwa kina, tumethibitisha kuwa mtu huyo si raia wa Tanzania,” alisema.

 
Back
Top Bottom