PreGE2025 Balozi Dkt Nchimbi: Msingi wa sera za CCM utabakia kuwa ni maendeleo ya watu pamoja na amani na utulivu wa nchi

PreGE2025 Balozi Dkt Nchimbi: Msingi wa sera za CCM utabakia kuwa ni maendeleo ya watu pamoja na amani na utulivu wa nchi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2013
Posts
843
Reaction score
1,024
UCHAGUZI 2025: BALOZI NCHIMBI ATOA WITO

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi amesema kuwa msingi wa sera za CCM utabakia kuwa ni maendeleo ya watu pamoja na amani na utulivu wa nchi.

Balozi Nchimbi aliyasema hayo leo Jumapili, tarehe 6 Aprili 2025, alipokuwa akizungumza na mamia ya wananchi wa mji wa Songea katika maeneo ya Liziboni, Uwanja wa Majimaji na Mshangano, ambapo wananchi walikusanyika kwa hamasa kubwa kumsikiliza licha ya kuwa kwenye ziara nyingine za kikazi.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Katika eneo la Liziboni, Balozi Nchimbi alilazimika kusimamisha msafara wake ili kuzungumza na wananchi waliomsimamisha njiani akitokea Nyasa. Alitumia fursa hiyo kuwashukuru wananchi wa Songea kwa mchango wao mkubwa uliomuwezesha kufahamika kitaifa na kimataifa.

Katika Uwanja wa Majimaji, alihutubia umati mkubwa wa wananchi waliokuwa wakimsubiri wakati alipofika kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la ghorofa lenye fremu 50 za CCM Mkoa wa Ruvuma. Katika hotuba yake, aliwaomba wananchi wa Songea, mkoa mzima na nchi nzima kwa ujumla kujiandaa kushiriki kwa wingi Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba, 2025.

Akiwa Mshangano, ambako alizindua rasmi fremu 50 za tawi la CCM la eneo hilo, Balozi Nchimbi alisisitiza tena umuhimu wa ushiriki mkubwa wa wananchi katika uchaguzi mkuu, akieleza kuwa ni kwa njia hiyo ndipo maendeleo na ustawi wa taifa yanaweza kufikiwa kwa kasi na kwa manufaa ya wote.

Kwa ujumla, ziara ya Katibu Mkuu huyo ilionesha mapokezi makubwa ya wananchi na kiu ya kusikia mwelekeo wa chama chao kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

IMG-20250406-WA1414.jpg
IMG-20250406-WA1413.jpg
IMG-20250406-WA1444.jpg
 

Attachments

  • IMG-20250406-WA1436.jpg
    IMG-20250406-WA1436.jpg
    87.7 KB · Views: 25
  • IMG-20250406-WA1443.jpg
    IMG-20250406-WA1443.jpg
    151.9 KB · Views: 31
  • IMG-20250406-WA1410.jpg
    IMG-20250406-WA1410.jpg
    109.1 KB · Views: 28
  • IMG-20250406-WA1437.jpg
    IMG-20250406-WA1437.jpg
    68.7 KB · Views: 31
  • IMG-20250406-WA1409.jpg
    IMG-20250406-WA1409.jpg
    108.8 KB · Views: 30
  • IMG-20250406-WA1435.jpg
    IMG-20250406-WA1435.jpg
    118.2 KB · Views: 36
  • IMG-20250406-WA1445.jpg
    IMG-20250406-WA1445.jpg
    138.8 KB · Views: 32
Nani ameuangalia mkutano wa Lissu leo Nachingwea?! Uwanja ulitapika,na hakuna aliyesombwa na Mafuso hata mmoja.
 
Chama kina anzisha miradi ya kupata hela, kule wanaanzisha miradi ya tone kwa tone kila mwaka huku wakibadili jina la miradi
 
𝗨𝗖𝗛𝗔𝗚𝗨𝗭𝗜 𝟮𝟬𝟮𝟱: 𝗕𝗔𝗟𝗢𝗭𝗜 𝗡𝗖𝗛𝗜𝗠𝗕𝗜 𝗔𝗧𝗢𝗔 𝗪𝗜𝗧𝗢

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi amesema kuwa msingi wa sera za CCM utabakia kuwa ni maendeleo ya watu pamoja na amani na utulivu wa nchi.

Balozi Nchimbi aliyasema hayo leo Jumapili, tarehe 6 Aprili 2025, alipokuwa akizungumza na mamia ya wananchi wa mji wa Songea katika maeneo ya Liziboni, Uwanja wa Majimaji na Mshangano, ambapo wananchi walikusanyika kwa hamasa kubwa kumsikiliza licha ya kuwa kwenye ziara nyingine za kikazi.

Katika eneo la Liziboni, Balozi Nchimbi alilazimika kusimamisha msafara wake ili kuzungumza na wananchi waliomsimamisha njiani akitokea Nyasa. Alitumia fursa hiyo kuwashukuru wananchi wa Songea kwa mchango wao mkubwa uliomuwezesha kufahamika kitaifa na kimataifa.

Katika Uwanja wa Majimaji, alihutubia umati mkubwa wa wananchi waliokuwa wakimsubiri wakati alipofika kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la ghorofa lenye fremu 50 za CCM Mkoa wa Ruvuma. Katika hotuba yake, aliwaomba wananchi wa Songea, mkoa mzima na nchi nzima kwa ujumla kujiandaa kushiriki kwa wingi Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba, 2025.

Akiwa Mshangano, ambako alizindua rasmi fremu 50 za tawi la CCM la eneo hilo, Balozi Nchimbi alisisitiza tena umuhimu wa ushiriki mkubwa wa wananchi katika uchaguzi mkuu, akieleza kuwa ni kwa njia hiyo ndipo maendeleo na ustawi wa taifa yanaweza kufikiwa kwa kasi na kwa manufaa ya wote.

Kwa ujumla, ziara ya Katibu Mkuu huyo ilionesha mapokezi makubwa ya wananchi na kiu ya kusikia mwelekeo wa chama chao kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

#Mwisho
 

Attachments

  • IMG-20250406-WA0162.jpg
    IMG-20250406-WA0162.jpg
    168.8 KB · Views: 33
  • IMG-20250406-WA0160.jpg
    IMG-20250406-WA0160.jpg
    923.9 KB · Views: 27
  • IMG-20250406-WA0167.jpg
    IMG-20250406-WA0167.jpg
    806.2 KB · Views: 30
  • IMG-20250406-WA0171.jpg
    IMG-20250406-WA0171.jpg
    900 KB · Views: 32
  • IMG-20250406-WA0172.jpg
    IMG-20250406-WA0172.jpg
    843.2 KB · Views: 29
  • IMG-20250406-WA0161.jpg
    IMG-20250406-WA0161.jpg
    892.2 KB · Views: 30
  • IMG-20250406-WA0174.jpg
    IMG-20250406-WA0174.jpg
    782 KB · Views: 32
  • IMG-20250406-WA0170.jpg
    IMG-20250406-WA0170.jpg
    628.9 KB · Views: 27
  • IMG-20250406-WA0157.jpg
    IMG-20250406-WA0157.jpg
    619 KB · Views: 29
  • IMG-20250406-WA0166.jpg
    IMG-20250406-WA0166.jpg
    654.1 KB · Views: 34
  • IMG-20250406-WA0158.jpg
    IMG-20250406-WA0158.jpg
    590.6 KB · Views: 31
  • IMG-20250406-WA0156.jpg
    IMG-20250406-WA0156.jpg
    413.5 KB · Views: 26
  • IMG-20250406-WA0154.jpg
    IMG-20250406-WA0154.jpg
    652.8 KB · Views: 29
  • IMG-20250406-WA0151.jpg
    IMG-20250406-WA0151.jpg
    678.1 KB · Views: 30
  • IMG-20250406-WA0155.jpg
    IMG-20250406-WA0155.jpg
    452.6 KB · Views: 33
Mungu atusaidie kwa kweli atuvushe salama kwa hili ila kusema CCM ndio tegemeo letu sio kweli ni matusi makubwa kwa wananchi CCM mnatakiwa kuwa vinara wa kuruhusu demokrasia ya kweli mfano mabadiliko juu ya hii katiba kandamizi tuliyonayo ili kila Mwananchi ajihisi ni sehemu ya Nchi hii vinginevyo hizi ni propaganda mnatupanga ili muendelee kuneemeka
 
Back
Top Bottom