Balozi Dr Suleiman: Unga unawamaliza Watanzania nchini China

Frank Wanjiru

Platinum Member
Joined
Apr 12, 2012
Posts
25,686
Reaction score
46,842
Balozi wa Tanzania nchini China, Dk Suleiman Haji Suleiman amesema dawa za kulevya zinaendelea kuwagharimu Watanzania wanaokwenda China, akieleza kuwa baadhi yao wamehukumiwa vifungo vya miongo kadhaa huku familia zao nchini zikipoteza mawasiliano nao na kuamini wamefariki dunia.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Makao Makuu ya Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalumu ya Kiuchumi Tanzania (Tiseza), jijini Dar es Salaam, leo Julai 14, 2026, Dk Suleiman amesema ubalozi umekutana na visa vingi vya Watanzania waliokamatwa kwa makosa ya dawa za kulevya na sasa wanatumikia adhabu katika magereza ya China kutokana na ukali wa sheria za nchi hiyo.

Ametoa mfano wa mama mmoja aliyefika kwenye banda la Ubalozi wa Tanzania wakati wa Maonesho ya Sabasaba akieleza kuwa aliarifiwa mwanaye aliyekuwa China amefariki akiwa gerezani.

“Baada ya kuchukua taarifa zake na kuzifuatilia, tulibaini kijana huyo yupo hai na anaendelea kutumikia kifungo chake. Anatarajiwa kumaliza adhabu mwaka 2031,” amesema.

Ameongeza kuwa wanawake wanaonekana kwa wingi kuwa miongoni mwa Watanzania wanaokamatwa kwa makosa hayo, akieleza kuwa wengi huingia kwenye mtandao huo baada ya kuanza safari za kawaida za biashara.

Ameonya kuwa sheria za China dhidi ya dawa za kulevya ni kali na hazitoi nafasi kwa anayebainika kufanya kosa hilo, hivyo amewasihi Watanzania wanaokwenda nchini humo kuwa waangalifu na kutokubali kubeba mizigo wasiyoifahamu kwa ahadi za kupata utajiri.
 
Sawasawa!
 
😁 jamaa awatanii kabisa. Safari yangu iliyopita kwenda China! Niliwanunulia Wenyeji wangu Kahawa toka hapa Tanzania.Kahawa ya Kopo. nilichukuwa kopo 6 😁. Ethiopia Bole Airport nilipita bila tatizo. China sasa!! Nili sachiwa mpaka nikachanganyikiwa...begi niliweka password lenye makopo ya kahawa- nilicheleweshwa for two hrs. Wakati wananipa begi langu nikaona wameweka mark ya pink - kwanza sikuelewa.Kwenye hii Safari nilikuwa na tembelea Viwanda kama 18 hivi vya aina mbali mbali kwenye miji zaidi ya 8 So after two days nilikuwa natakiwa panda domestic flight toka mji mmoja kwenda mwingine again nikashikiriwa kama lisaa hivi, maswali kibao,Begi likachelewa tena na nilipofika Hotel nilipolifunguwa begi nikakuta limepekuliwa na vitu wamevipanga tofauti na mimi nilivyovipanga... Hapo ikabidi yale makopo yote niyagawe kwa hawa wenyeji wangu wa huu mji wa pili.maana bado nilikuwa na domestic flights 5 mbele yangu.Kweli bwana...hii mbinu ilinisaidia.... Sikupata tena kupekuliwa kama gaidi na kucheleweshwa patiwa begi langu mpaka narudi TZ. Nimejifunza sinto baba any type of foodstuff to any where out of Tanzania again. Airports za China kwa waafrica sio powa kabisa
 
Back
Top Bottom