Balozi Hoyce Temu ahitimu Phd chuo kikuu SAUT

BabaMia

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2024
Posts
270
Reaction score
554
Hoyce Anderson Temu, aliyezaliwa Machi 1978 katika Hospitali ya Mount Meru mjini Arusha. Alianza safari yake ya masomo katika Shule ya Msingi Matemboni Old Moshi mkoani Kilimanjaro na kuhamia Arusha katika shule ya Msingi Uhuru na baadaye kujiunga na Shule ya Sekondari Arusha, ambako alifanya vizuri katika masomo yake, kabla ya kuchaguliwa kujiunga na Shule ya Sekondari ya Zanaki jijini Dar es Salaam.

Hakuishia hapo kwani aliendelea na masomo ya juu katika Chuo Kikuu cha Arizona State nchini Marekani, ambako alipata Shahada ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma. Baada ya kurejea Tanzania, alisoma na kuhitimu Stashahada ya Uzamili katika Mahusiano ya Kidiplomasia kutoka Kituo cha Mahusiano ya Kigeni kinacho julikana kwa sasa kama Chuo cha Dr Salim Ahmed Salim kilichoko Kurasini jijini Dar es Salaam. Nondo zikaendelea zaidi na akapata Shahada ya Uzamili katika Mawasiliano ya Umma kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino cha Tanzania (SAUT) kilichopo Mwanza.

Mnamo mwezi Mei 2021, aliteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan kuwa Balozi na Naibu Mwakilishi wa Kudumu katika Mashirika ya Kimataifa Geneva Uswisi. Wakati anateuliwa alikuwa anasoma Shahada ya Uzamivu katika mawasiliano ya umma kozi aliyo ianza mwaka 2018.

Disemba 2024, amefanikiwa vyema kuhitimu Shahada ya Uzamivu katika Mawasiliano ya Umma yaani ‘Doctor of Philosophy in Mass Communication’ katika chuo cha SAUT ambapo tafiti yake ilijikita kuangalia “Usawa (Equity) wa kijinsia katika nafasi ya uongozi katika makampuni ya vyombo vya habari nchini Tanzania”

Ikumbukwe Mlimbwende Hoyce alianza kujipatia umaurufu kitaifa mwaka 1999 baada ya kutwaa taji la Miss Tanzania akiwa na umri wa miaka 21, aliiwakilisha Tanzania vyema katika shindano la Miss World. Hiyo ndiyo historia fupi ya mlimbwende huyu ambaye sasa tunamwita Mh. Balozi. Dk. Hoyce Anderson Temu.
 
Attachments

  • 1734931003211.jpg
    1734931003211.jpg
    309.1 KB · Views: 10
  • 1734930997126.jpg
    1734930997126.jpg
    325.2 KB · Views: 7
  • 1734930987403.jpg
    1734930987403.jpg
    347.3 KB · Views: 14
  • 1734930980251.jpg
    1734930980251.jpg
    283 KB · Views: 8
Hoyce Anderson Temu, aliyezaliwa Machi 1978 katika Hospitali ya Mount Meru mjini Arusha. Alianza safari yake ya masomo katika Shule ya Msingi Matemboni Old Moshi mkoani Kilimanjaro na kuhamia Arusha katika shule ya Msingi Uhuru na baadaye kujiunga na Shule ya Sekondari Arusha, ambako alifanya vizuri katika masomo yake, kabla ya kuchaguliwa kujiunga na Shule ya Sekondari ya Zanaki jijini Dar es Salaam.

Hakuishia hapo kwani aliendelea na masomo ya juu katika Chuo Kikuu cha Arizona State nchini Marekani, ambako alipata Shahada ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma. Baada ya kurejea Tanzania, alisoma na kuhitimu Stashahada ya Uzamili katika Mahusiano ya Kidiplomasia kutoka Kituo cha Mahusiano ya Kigeni kinacho julikana kwa sasa kama Chuo cha Dr Salim Ahmed Salim kilichoko Kurasini jijini Dar es Salaam. Nondo zikaendelea zaidi na akapata Shahada ya Uzamili katika Mawasiliano ya Umma kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino cha Tanzania (SAUT) kilichopo Mwanza.

Mnamo mwezi Mei 2021, aliteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan kuwa Balozi na Naibu Mwakilishi wa Kudumu katika Mashirika ya Kimataifa Geneva Uswisi. Wakati anateuliwa alikuwa anasoma Shahada ya Uzamivu katika mawasiliano ya umma kozi aliyo ianza mwaka 2018.

Disemba 2024, amefanikiwa vyema kuhitimu Shahada ya Uzamivu katika Mawasiliano ya Umma yaani ‘Doctor of Philosophy in Mass Communication’ katika chuo cha SAUT ambapo tafiti yake ilijikita kuangalia “Usawa (Equity) wa kijinsia katika nafasi ya uongozi katika makampuni ya vyombo vya habari nchini Tanzania”

Ikumbukwe Mlimbwende Hoyce alianza kujipatia umaurufu kitaifa mwaka 1999 baada ya kutwaa taji la Miss Tanzania akiwa na umri wa miaka 21, aliiwakilisha Tanzania vyema katika shindano la Miss World. Hiyo ndiyo historia fupi ya mlimbwende huyu ambaye sasa tunamwita Mh. Balozi. Dk. Hoyce Anderson Temu.
Hongera zake.
Hebu tufafanulie safari yake kutoka zanaki secondary kwenda Arizona University.
Je alipataje hiyo scholarship.
hii ni kusadia wengine kujua mbinu za kupata scholarship
 
Bila shaka mdogo wangu Wema Sepetu na warembo wenzake wa zamani wana kitu cha kujifunza hapa.
 
  • Thanks
Reactions: FWC
Kuña mmoja sasa hivi kamaliza CPA hadi nilishangaa yaani kwa nature ya majukumu yake ni ngumu sana kufaulu.....alafu kuna mmoja sasa hivi anaitwa Advocate yaan pale law school kapitaje. Nimeamini viongozi wa nchi yetu wana AKILI SANA...
Umeonaaeee.....Wana vipaji vikubwa sana
 
Back
Top Bottom