Pfizer
JF-Expert Member
- Mar 25, 2021
- 819
- 1,093
Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe, Mhe. CP Suzan S. Kaganda, ametembelea ofisi za Mamlaka ya Bandari ya Tanzania (TPA) zilizopo mjini Harare na kufanya mazungumzo na Mwakilishi wa TPA nchini Zimbabwe, Bi. Kulthum Boma.
Ziara ya Mhe. Balozi Kaganda katika ofisi hizo ni sehemu ya hatua muhimu katika utekelezaji wa Sera ya Diplomasia ya Uchumi, ikilenga kutambua na kuendeleza mchango wa TPA katika usafirishaji wa mizigo kutoka bandari za Tanzania kwenda nchi za Kusini mwa Afrika, ikiwemo Zimbabwe.
Bi. Kulthum ameeleza kuwa ofisi hiyo, yenye jukumu la masoko na huduma kwa wateja, imekuwa na mchango chanya katika ongezeko la shehena ya mizigo inayoingia Zimbabwe kupitia bandari za Tanzania tangu kufunguliwa rasmi mwaka 2023.
Kwa upande wake, Mhe. Balozi Kaganda amepongeza mafanikio hayo na kusisitiza umuhimu wa ofisi hizo kushirikiana na Ubalozi katika kuandaa mikutano na wadau pamoja na wafanyabiashara nchini Zimbabwe, ili kutumia majukwaa hayo kutoa elimu na kuongeza uelewa juu ya matumizi ya bandari za Tanzania, hatua itakayochangia zaidi katika ukuaji wa pato la Taifa.